KERO Utolewe Ufafanuzi Juu ya Mfumo wa Utoaji Alama katika Mitihani ya Mtandaoni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ningependa kuwasilisha hoja yangu kwa Mamlaka ya Utumishi inayohusika na usimamizi wa mitihani ya mtandaoni kwenye usaili wa kuandika.

Kumekuwa na mkanganyiko wa matokeo ambapo mtihani wenye jumla ya maswali 50 unatoa alama kama 93 au 75. Kimantiki, ikiwa mtihani una maswali 50, tunatarajia kila swali liwe na alama 2, jambo ambalo lingepelekea jumla ya alama kuwa namba shufwa (even numbers) na si namba witiri au tasa (odd/prime numbers).

Ili kuleta uwazi na haki kwa watahiniwa, ninaomba Mamlaka itoe mwongozo wa kina kuhusu hili. Ikiwa kuna maswali yenye uzito mkubwa kuliko mengine, ni vyema alama hizo zikaonyeshwa mbele ya kila swali. Hatua hii itawasaidia watahiniwa kupanga muda wao vizuri na kuweka jitihada zaidi kwenye maswali yenye alama nyingi.

 
Ningependa kuwasilisha hoja yangu kwa Mamlaka ya Utumishi inayohusika na usimamizi wa mitihani ya mtandaoni kwenye usaili wa kuandika.
Pole sana mkuu.
Inauma sana kupata 75 halafu wa 76 anachaguliwa kwenda Oral
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…