Utoto ulikufanya uone kila kitu kinawezekana ulipokua umegundua sio rahisi?

Utoto ulikufanya uone kila kitu kinawezekana ulipokua umegundua sio rahisi?

tamu 3

Member
Joined
Dec 11, 2024
Posts
88
Reaction score
216
Mimi nikiwa mdogo nilikuwa najua baba na mama mzazi wao ni mmoja
.
Mimi nilijua baba alikuwa mzembe kutojenga ghorofa mbona wenzake wamejenga?

Mimi nilikuwa najua baba hatupendi kwanini hanunui nyama kila siku?

Nilikuwa nawalaumu baadhi ya NDUGU kwanini hawarutembelei?


Nilikuwa nawaonea wivu sana wanaume waliooa nilijua wanafaidi sana

Mimi nilijua mtu akifa atafufuka kweli toka nazaliwa hakuna hata mmoja aliyefufuka kijijini kwetu

..ongeza zako
 
Kama miaka 30 yani sijui nilikua nai hukuliaje, nikisikia mtu ana 30, nilijua ni mkubwa sanaa
 
"Nilikuwa nawaonea wivu sana wanaume waliooa nilijua wanafaidi sana" Na hapo ulikua mtoto binti tamu tatu ila ulikua unawaonea wivu wajomba zako na baba zako wanavyowapelekea moto shangaz zako na mamazo. Duuh kaz kwelikweli
 
Nilidhani ukitaka mtoto unapewa Bure na hospital kama unavyopewa vyandarua vya msaada

Kumbe kupata mtoto mpaka ufanyemzabzab
 
Nilimuuliza mzee wangu kwanini hakununua maeneo potential miaka ya 90' ambayo sasa hivi ushuani ambapo watoto sasa hivi tungekua na mali??

Akajibu kua yeye kazaliwa kijijini hakua na ujanja wa kujua kukua kwa miji na faida ya viwanja,yeye kaja dar kimara kuna mashamba,..so kwa kwa mimi nilie zaliwa mjini nina advantage ya kujifunza na kutofanya makosa kama yake... so me now nanua mapori kila ninapo pata fursa na kibunda...so sure BABA YAKO ALIKUA MZEMBE KUTOJENGA GHOROFA
 
Back
Top Bottom