mnacheza kibaba na kimama mnagombania characters, mimi baba mwingine mimi mama kila mtu anataka kuwa baba na mama kwasababu kuna ile scene ya kulala mfanye mchezo mbaya,
nyingine, mnaenda kuiba mchele kwa mangi enzi hizo mchele mangi anaweka panado eti msitafune, wachaga bwana! basi mnaiba mchele alafu unawapeleka wachumba wanapika wali kwenye vifuu au yale makopo ya nyanya, aisee wali ulikuwa unatokea kweli na unanukia..
kwa watoto wakiume kulikuwa na mchezo wa gololi bwana, lakin huu mchezo ulikuwa kwenye zile late 90s mpaka 2000 uko... kwenye gololi kulikuna na misemo kama, mwamwiloo (wamwishoo), wakati, dungu (ligololi likubwa likubwa), mjoda, kadema, kila, lift double , kinyambii (gulu wa gololi) n.k kwenye gololi nilikuwa nawapuna sana aisee.
daah, zile enzi utoto ulikuwa raha sana, michezo ilikuwa kibao, ukirudi nyumbani upo hoi, kuoga utaki, kusinzia kwa sana unaamshwa na sahani ya bati ya wali na marage.
wakishua hamuwezi kunielewa