Utoto wa miaka ya 80's-90's ulikuwa raha sana

Enzi hizo TV mnaangalia wikiend kwenye Banda la video tena inatoka mjini,Leo TV kila nyumba

Kuna siku mnakaa mnaamua kuhadithiana muvi za kina anord ya Jeni au komando kipensi,au jet li na maiko(tai chi ) alafu msioiona mnakuwa makini kusikiliza[emoji28]..leo nikienda Kwa bro watoto wake wakiniona wanalilia niwape simu wacheze gemu,dah namaind sn

Ukiwa na gazeti la sani unaenda nalo skuli Kisha anapewa mtu mmoja anayesoma vizuri anawasomea huku mmemzunguka..enzi hizo kina kipepe,sokomoko,mapung'o,ndumilakuwili,madenge wanatamba na wengi wetu hizi katuni tukidhani ni watu halisi na wanaishi dar
Hapa kwenye gazeti la Sani umibamba sana... Nikiwa darasa la tano, Kuna jamaa yangu alikuwa anakuja sana na gazeti hili....stori ya mapung'o mcheza mpira... Kuna jamaa yangu mpaka sasa mtaani pale anaitwa jina hili maana alimpenda sana Mapung'o....

Loh... Umenikumbusha mbali...
 
Nikiwa Home nikiwaangalia watoto wangu naona kama utoto wao hauna kashikashi nyingi kama enzi zangu. Nikikumbuka enzi zile malezi yake kama jeshini vile..na taarifa nyingi tulikuwa tunafichwafichwa.

Mfano

(1) Akizaliwa mtoto Home, mnadanganywa mama ameenda kumnunua mtoto hospitali.

(2) Shuleni likipita gari la msalaba mwekundu, mwanafunzi mmoja akapiga yowe Mumianiiiii, nyonya damuuu, basi siku hiyo shule hamna masomo tena ni mbio kila kona.

(3) Kuna siku tulifungiwa maandazi kwenye gazeti la lugha la kiarabu mbaba mmoja akatutisha msile mtakuwa vichaa hiyo ni QURAN hiyo tukayatupa maandazi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

(4) Mkitaka mpira wa miguu basi inabidi mkaokote Lylon kwenye maduka ya wahindi mtengene mpira ndio mcheze.

Lakini hawa Makamanda wetu wa Kidigitali Daah mambo yao soft sana, mpira wanataka uwanunulie dukani, hawajui hata Manati kazi yake nini, [emoji1787][emoji1787][emoji1787]hata kuchomwa na miba za mbigiri miguu haziwachomi kutwa wamevaa viatu, hata mafunza miguuni hayawaingii.
Sio kwamba wewe una angalau ya maisha au uko mjini? Je watoto wa kule kijijni nao wana maisha kama watoto wako wa kidijitali?
 
Enzi hizo TV mnaangalia wikiend kwenye Banda la video tena inatoka mjini,Leo TV kila nyumba

Kuna siku mnakaa mnaamua kuhadithiana muvi za kina anord ya Jeni au komando kipensi,au jet li na maiko(tai chi ) alafu msioiona mnakuwa makini kusikiliza😅..leo nikienda Kwa bro watoto wake wakiniona wanalilia niwape simu wacheze gemu,dah namaind sn

Ukiwa na gazeti la sani unaenda nalo skuli Kisha anapewa mtu mmoja anayesoma vizuri anawasomea huku mmemzunguka..enzi hizo kina kipepe,sokomoko,mapung'o,ndumilakuwili,madenge wanatamba na wengi wetu hizi katuni tukidhani ni watu halisi na wanaishi dar
Nilikuaga najua Mapung'o anaishi Dar na muda si punde angelamba usajiri kwenye moja ya vilabu vya kariakoo maana alikua anaupiga mwingi sana
 
Hahaha..mapung'o ana kitovu km honi za wale jamaa wa lambalamba😅😅

Kitovu kimezungukwa na nywele utadhani inzi wapo kwenye kikao,zamani watu walikuwa Wanachora katuni bwana
 
Sasa kama hata manati mtoto wa leo hajui kuitengeneza, anaona tu ikiuzwa unategemea nn?

Kila kitu anachotumia ni ready made kutoka viwandani.
 
Nikiwa Home nikiwaangalia watoto wangu naona kama utoto wao hauna kashikashi nyingi kama enzi zangu. Nikikumbuka enzi zile malezi yake kama jeshini vile..na taarifa nyingi tulikuwa tunafichwafichwa.

Mfano

(1) Akizaliwa mtoto Home, mnadanganywa mama ameenda kumnunua mtoto hospitali.

(2) Shuleni likipita gari la msalaba mwekundu, mwanafunzi mmoja akapiga yowe Mumianiiiii, nyonya damuuu, basi siku hiyo shule hamna masomo tena ni mbio kila kona.

(3) Kuna siku tulifungiwa maandazi kwenye gazeti la lugha la kiarabu mbaba mmoja akatutisha msile mtakuwa vichaa hiyo ni QURAN hiyo tukayatupa maandazi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

(4) Mkitaka mpira wa miguu basi inabidi mkaokote Lylon kwenye maduka ya wahindi mtengene mpira ndio mcheze.

Lakini hawa Makamanda wetu wa Kidigitali Daah mambo yao soft sana, mpira wanataka uwanunulie dukani, hawajui hata Manati kazi yake nini, [emoji1787][emoji1787][emoji1787]hata kuchomwa na miba za mbigiri miguu haziwachomi kutwa wamevaa viatu, hata mafunza miguuni hayawaingii.
Nakumbuka mambo ya mechi uwanja wa Taifa...ilikuwa lazima kuingia uwanja wa Taifa kukiwa na mechi..shamba la bibi...ingawa tulikua hatupewi hela yeyote na wazazi.. Nazikumbuka njia tatu za kuzamia:
1. Kuruka ukuta ndala mkononi
2. Kuomba kumsukuma mlemavu kwenye wheelchair ili uingie naye halafu mbeleni unamtosa na unatimua mbio
3.Kama Yosso
Mechi inatumia mpira mmoja tu ....ukitoka nje ya uwanja inabidi kusubiri walio nje waurushe ndani...au ukiangukia kwa mashabiki wanaweza wakaushikilia ili kupoteza muda kama timu yao imeshinda...
Dah ilikuwa raha sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]au unaingia muda wa fungulia mbwa,dakika 5 kabla mpira haujaisha
 
Zamani kulikuwa na maonesho ya cultural troupes (kibisa) siku za sikuu ,

Mfano ; Kile cha kina mzee Jangala .

Siku hizi naona kimyaa!
 
Back
Top Bottom