Utoto wa miaka ya 80's-90's ulikuwa raha sana

Hivi ya kusimulia Movie nimepata ujiko sana Primary, kuna.Wahindi waliweka bili ya maziwa HOME sasa ikifika Jioni inabidi tuwapelekee maziwa majumbani kwao, basi tunagombea na Mabroo zangu kupeleka maziwa,ukifika unakaa sebuleni unacheki MOVIE kwenye Runinga,kesho ukifika SHULE wanafunzi wanakuzunguka unawasimulia[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sema labda watoto wenu huko Dar mnawalea hivyo ndio maana unakuta vijana wengi wa huko ni mchele mchele yaani wamedebweda
Ila sisi huku bara mtoto wa miaka 7 anasoma shule ya msingi km 24 kutoka nyumbani amebeba mfagio, jembe, galoni ya maji, jiwe, mzigo wa nyasi, matete, fimbo nk.
Halafu yuko peku
Sisi huku bado watoto wanakunya porini na kuchambia chini kama babu zao[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu hawa ni kizazi kipya mkuu,hata life span yao ni fupi miaka 55 mkuu,enzi zile tunaenda ahule miguu chini yani mpaka unyayo unakuwa mgumu kama soli,hawa sa hivI wanakula raha tu.

Utakuta mtto wa kiume anavaa ndala na sox eti kuna baridi.enzi zetu we ukifanikiwa kuwa na rim ua baiskeli unakimbia nalo ukiendesha na ukichelewa ukakuta msosi umeisha unashinda njaa.

Siku hiziwanaendesha magari kwenye computer.
 
Watoto wetu wa leo hawajui kuishi kijamaa.Mmoja akinunua bagia,kapile au andazi wenzie wanamkimbiza na kumuomba awakatie.Kiroho poa wanagawiwa.Na wakati wa kula watoto wote hadi wa jirani wanawekewa pamoja msosi.Hapo ni mwendo wa kasi kutupia matonge mdomoni.Zubaa ulie hiyo.Nyama wanashikishwa mkononi kabisa.Kila mtu afe na chake.Unyonyaji ulipingwa hadi wakati wa kula.Hakuna mahot-pots!Hahahahaaa!Hapo ndiyo tuliona "uroda"!Siyo siku hizi neno uroda linatumika kumaanisha uhuniuhuni tu.
 
Umenikumbusha mbali sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kina Zena na Betina, Watoto mapacha, Madenge, na wale jamaa wa timu za mpira Bushmen na Maborn town.
Baadae ikaja Gazeti la Kiu kuna mwamba aliitwa Baba ubaya[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Zamani raha sana.Kwanza elimu ya kujitegemea ilifundishwa kwa vitendo kwelikweli.Kwa mfano,mtu akitaka kufunga ndoa alipaswa ajikusanyie fedha,chakula na mavazi kwa ajili hiyo.Siyo kuchangishanachangishana hadi mnagombana na kuhatarisha au kuuvunja udugu.Kila mwenye sherehe iwe harusu,kipaimara,komunio au vyovyote alijitegemea na kualika ndugu wafike kupata tumbuizo,chakula nk.
 
mnacheza kibaba na kimama mnagombania characters, mimi baba mwingine mimi mama kila mtu anataka kuwa baba na mama kwasababu kuna ile scene ya kulala mfanye mchezo mbaya,

nyingine, mnaenda kuiba mchele kwa mangi enzi hizo mchele mangi anaweka panado eti msitafune, wachaga bwana! basi mnaiba mchele alafu unawapeleka wachumba wanapika wali kwenye vifuu au yale makopo ya nyanya, aisee wali ulikuwa unatokea kweli na unanukia..

kwa watoto wakiume kulikuwa na mchezo wa gololi bwana, lakin huu mchezo ulikuwa kwenye zile late 90s mpaka 2000 uko... kwenye gololi kulikuna na misemo kama, mwamwiloo (wamwishoo), wakati, dungu (ligololi likubwa likubwa), mjoda, kadema, kila, lift double , kinyambii (gulu wa gololi) n.k kwenye gololi nilikuwa nawapuna sana aisee.

daah, zile enzi utoto ulikuwa raha sana, michezo ilikuwa kibao, ukirudi nyumbani upo hoi, kuoga utaki, kusinzia kwa sana unaamshwa na sahani ya bati ya wali na marage.



wakishua hamuwezi kunielewa
 
Enzi zile kama hujawahi kuanguka kwenye mti wa mazambarau bado bado hujacheza sawasawa
 
Kilometa 24 unazijua ama una andika tu inmladi
 
Kilometa 24 unazijua ama una andika tu inmladi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kwa kweli hata shuleni atakuta masomo yameisha
 
Kweli Mohtpots uchoyo tu, kama mchele unamwagwa wote kwenye sahani mnagombania ukiisha umeisha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Miaka hiyo ilikuwa na ukakamavu sana,

Nakumbuka mtaani tulikuwa tunagombanishwa (ngumi), unaweza gombanishwa hata na aliyekuzidi umri ili tu upigwe,

Unachorwa mstari alafu mwenzio anaambiwa avuke ule mstari aje upande wako ,akivuka tu unaambiwa huyu(aliyevuka mstari) anamtomba mama ako hapo lazima ujae sumu urushe ngumi na ndipo zinapoanzia.

Ukipigwa ukarudi kwenu umevimba au umechubuka unakandwa na majimoto ya chumvi hakuna cha bandeji wala plaster,

Kuna wale wababe wa mitaa utashangaa anaanza kukudai deni hewa, akikukuta na hela mfukoni anachukua, na hilo deni haliishi mpaka uweze kumfua/kumtimba,

Tukienda mtoni kuogelea unaweza ibiwa nguo zako ukiwa majini ili urudi kwenu uchi, au nguo zako zikapakwa upupu ili ukianza kuwashwa wenzio waanze kucheka, au ile unasukumiwa kwenye kina kirefu ili upige vikombe,

Kifimbo cheza ukisahau kushika fimbo unachapwa, Kimputu ukiinama tu unapigwa teke la matakoni na linaweza pita hadi kwenye pumbu, tobo dunda ukipigwa tobo unapigwa mpaka ukashike kitu mlichokubaliana na wenzako, Punja hii ukiwa na kitu mkononi kikipunjwa kikadondoka chini sio chako tena kinakuwa cha aliyekupunja (hii ni michezo unayo-join kwa hiyari yako)...
 
Umenikumbusha mbali sana[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kina Zena na Betina, Watoto mapacha, Madenge, na wale jamaa wa timu za mpira Bushmen na Maborn town.
Baadae ikaja Gazeti la Kiu kuna mwamba aliitwa Baba ubaya[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna mechi moja hiyo ya derby Kati ya Bush stars naborn town kina.Humo mapung'o wa bush stars alikuwa anaupiga mwingi vby mno,alafu bush stars hawavai jezi wanacheza tumbo wazi [emoji28]

Mara nyingi mechi Yao ilikuwa haiishi,lazima kutokee fujo au nyuki watande uwanjani[emoji28]..magazeti ya zamani yalikuwa yanafurahisha sn

Ukifungua ndani zaidi unakutana na Stori za kina Irene mwamfupe,sultan tamba.Irene alikuwa na Stori zake ukisoma unaweza kwenda kupiga nyeto maana unasoma huku mashine inasimama asee,enzi hizo hakuna kuangalia pilau,unakuwa na ugumu mwaka mzima haujatomber[emoji28][emoji28].siyo siku hizi unadownload porn kwenye simu[emoji28]

Maisha yamebadilika sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Kuvua samaki kwa nyavu au ndoano
Kupigana
kucheza mipira ya lailoni
kuiba njiwa, kuku, samaki wale wa mapambo,
kucheza goroli
kucheza kibundiki bunduki
kutengeneza magari ya mbao au mabua,
kuchezea udongo
kimama ma na kibaba baba
komborela
kudandia magari
kuiba pipi, dukani kwa mangi
kutega ndege, kuwinda porini
kupanda juu ya miti, na kufanya kama gari..


Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Hatari sana...hata kutega ndege kwa ulimbo hawawezi, maana zamani unaweza kurudi Home na njiwa pori na mama akawatumia kama mboga ya kulia Ugali mchana
Niliwateketeza sana hao viumbe kwa njia mbali mbali! Ilikuwa raha sana. Siku hizi nikiona wazungu wanakuja kufanya sport hunting au fishing, na mie najiona kumbe sikuwa nawaonea hao viumbe!
 
Dah mkuu hayo yote umetaja kama tulikuwa wote. Gazeti la sani mm nilikuwa najua dk love pimbi,lodi lofa na progesa ndumilakuwili ni watu real na wanakaa Dar. Utoto huu dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…