Utoto wa miaka ya 80's-90's ulikuwa raha sana

Hapa kwenye gazeti la Sani umibamba sana... Nikiwa darasa la tano, Kuna jamaa yangu alikuwa anakuja sana na gazeti hili....stori ya mapung'o mcheza mpira... Kuna jamaa yangu mpaka sasa mtaani pale anaitwa jina hili maana alimpenda sana Mapung'o....

Loh... Umenikumbusha mbali...
 
Sio kwamba wewe una angalau ya maisha au uko mjini? Je watoto wa kule kijijni nao wana maisha kama watoto wako wa kidijitali?
 
Nilikuaga najua Mapung'o anaishi Dar na muda si punde angelamba usajiri kwenye moja ya vilabu vya kariakoo maana alikua anaupiga mwingi sana
 
Nilikuaga najua Mapung'o anaishi Dar na muda si punde angelamba usajiri kwenye moja ya vilabu vya kariakoo maana alikua anaupiga mwingi sana
Hahaha..mapung'o ana kitovu km honi za wale jamaa wa lambalambašŸ˜…šŸ˜…

Kitovu kimezungukwa na nywele utadhani inzi wapo kwenye kikao,zamani watu walikuwa Wanachora katuni bwana
 
Sasa kama hata manati mtoto wa leo hajui kuitengeneza, anaona tu ikiuzwa unategemea nn?

Kila kitu anachotumia ni ready made kutoka viwandani.
 
Nakumbuka mambo ya mechi uwanja wa Taifa...ilikuwa lazima kuingia uwanja wa Taifa kukiwa na mechi..shamba la bibi...ingawa tulikua hatupewi hela yeyote na wazazi.. Nazikumbuka njia tatu za kuzamia:
1. Kuruka ukuta ndala mkononi
2. Kuomba kumsukuma mlemavu kwenye wheelchair ili uingie naye halafu mbeleni unamtosa na unatimua mbio
3.Kama Yosso
Mechi inatumia mpira mmoja tu ....ukitoka nje ya uwanja inabidi kusubiri walio nje waurushe ndani...au ukiangukia kwa mashabiki wanaweza wakaushikilia ili kupoteza muda kama timu yao imeshinda...
Dah ilikuwa raha sana
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]au unaingia muda wa fungulia mbwa,dakika 5 kabla mpira haujaisha
 
Zamani kulikuwa na maonesho ya cultural troupes (kibisa) siku za sikuu ,

Mfano ; Kile cha kina mzee Jangala .

Siku hizi naona kimyaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…