Utoto wa miaka ya 80's-90's ulikuwa raha sana

Shuleni hasa ya msingi kunauzwa mihogo na supu ya mapupu [emoji108]

Unanunua supu ya mapupu na makwasukwasu kwenye kibakuli unachanganya na mihogo yako kwa kuipasuapasua tamuuuu [emoji14][emoji14][emoji14]
 
Wauza ubwabwa maharagwe sasa,

Unakuta mchafuuuu mmama amejaa masagamba miguuni lakini ubwabwa wake mtaamu!

Basi ikasemekana wengine ubwabwa unakuwa mtamu sababu anapikia kwa kutumia Maji ya kuchambia.

Wanasema mtu mchafu vile iweje ubwabwa wake uwe mtamu? [emoji3]

Kumbe katika level ya primary wanafunzi wanakuwa na uelewa fulani wa mambo na kuweza ku-reason
 
Wazee utawasikia vijana wa siku hizi sjui vipi ila enzi zetu......
Imagine ukimbizane na mpira wa mabox pekupeku wakati mchina karahisisha mpira hata 20000 unapata 😅😅
Zamani mwanamke mzungu hakupaswa kutoka nje ya nchi yake bila escort ya mwanaume ila dunia ya leo utasikia solo female (traveler) hahitaji ruksa kusafiri
 
Hili nalo ni la kujivunia enzi zenu ?
 
Halafu zamani ukitaka kumuita kijana kwa mbali unapiga Mluzi(mbinja) kwa kuweka vidole viwili mdomoni au unashika lips ya chini. Kama ni msichana anapita na unataka kumuita kiaina ufanya Ksiiiii!!, Ksiiiii!!
 
Hili nalo ni la kujivunia enzi zenu ?



Kwangu mimi naam! [emoji106]

Kwani mpaka wa mambo ya kujivunia unaanzia wapi na kuishia wapi labda?

Pengine jambo analoweza kujivunia mtu au watu fulani kwa mwingine linaweza kuwa kinyume chake!
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Daaah umenikumbusha mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…