Muungano wa vilabu vya waandishi wa Habari nchini(UTPC),wameingia kwenye mvutano mkali la waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro baada ya kuzuia mkutano wao usifanyike.
Mkutano huo uliokuwa umepangwa kufanyika kesho ,umepigwa pini na UTPC kwa madai ya kuwepo kwa hisia Kali kutoka kwa waandishi hao.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa Leo na kamati ya mpito ya chama Cha waandishi wa habari mkoani humo(MECKI),UTPC imetishia kuifuta kwenye orodha ya wanachama wake endapo mkutano huo utafanyika.
Hata hivyo baadhi ya waandishi wamekuja juu wakitaka UTPC kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Klabu hiyo kwani ipo kwa mujibu wa Katiba .
Mkutano huo ulikuwa.utoe hatima ya viongozi wa Klabu hiyo(katibu na mweka hazina) wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi mkubwa wa mamilionj ya fedha .
Wanatuhumiwa kughushi nyaraka za malipo na kukomba mamilioni ya fedha ikiwamo majina bandia ya waandishi wa habari .
"Hatuwezi kuendelea na viongozi wanatuhumiwa kufuja fedha ,tunataka watupishe kwanza ",amesema mwandishi mmoja .
Hii hapa Taarifa ya kuahirishwa kwa mkutano huo .
TAARIFA MAHSUSI
Kama tulivyowataarifu asubuhi ya leo.
Tulipokea barua ikitoa ushauri wa MSISITIZO wa kuahirisha mkutano mkuu kama maelekezo ya barua yao ya awali ilivyokuwa.
Ndani ya barua hii ya leo, kuna maudhui yanayoashiria klabu itachukuliwa hatua endapo itakiuka maagizo hayo ambayo barua inasema tutakuwa tumekiuka Katiba ya UTPC na MoU kati ya MECKI na UTPC.
Tumetafakari sana hiki kinachoendelea, faida na madhara yatakayoipata MECKI kama itafanya mkutano huo na kamati imeamua kusitisha mkutano mkuu uliokuwa ufanyike kesho Desemba 2,2024 licha ya maandalizi yote muhimu kukamilika, hadi hapo mtakapojulishwa tena baada ya mvutano huu unaoonekana kupatiwa ufumbuzi.
Tunaomba muwe watulivu.
Edwine Lamtey
KAIMU MWENYEKITI
Kusoma majibu ya UTPC, soma hapa ~ UTPC yatoa majibu kuhusu madai kuwa imezuia Mkutano wa Waandishi wa Habari Mkoani Kilimanjaro