UTT AMIS naona kwenye account yangu ya UTT hela imeongezeka kidogo

Hbr wandugu. Juzi nimefanikiwa kuitoa hela yangu UTT. Imechukua siku 2 tu bond fund kunilipa tokea nijaze form. Biashara yangu imekaa sawa sasa naiingiza huko. Niliwaambia UTT nimehifadhi tu fedha zangu na si kufanya biashara na UTT sema watu ni vichwa ngumu. All in all nimefurahi mno kujifunza kitu kipya. Sasa nimeijua vzr bond fund ya UTT. Km kuna mtu atakua na maswali aje inbox.

Thanks
 
Na nyongeza ni kwamba.

Kwa miezi 9 niliyohifadhi nimevuta 795,000/=
Kwa miezi 9 niliyohifadhi nimpata 199,000/= kwa kupanda kwa thamani ya vipande

TOTAL= 994,000/=

Yani nimepata 994,000/= kwa kihifadhi tu huko. Benki nisingepata kitu km ningehifadhi.

But sijui km nilikosea kufanya hii kitu maana biashara zangu ziliyumba kwa miezi hiyo.

Nasubiri kukosolewa[emoji6]
 
Samahani , Uliweka Kiasi gani huko UTT ?
 
Mi sijui hesabu

Umeweka 10mil

Kila mwezi unapata 80,000
Mwaka mmoja unapata 960,000
Miaka 10 =9,600,000

Au nimekosea wakuu??

Basi kaiweke benki mkuu.

Tatizo la watu humu ndani wanadhani kila mtu anaeenda kuweka pesa zake UTT anafanya biashara.

Mimi nina milioni 100 zangu, sina muda wa kufanya biashara na sina kipawa cha business, naiweka Liquid fund na kila mwezi inakua inaongezeka by 1 M, tofauti na nikiweka benki (hata kama ni FDA) haiongezeki kwa rate hiyo.


UTT sio biashara. Mwenye talanta ya biashara ni wastage of time kuweka pesa zako UTT, nenda kafanyie biashra pesa yako ikue kwa rate unayotaka wewe
 

Mjinga ni mtu asiyejua kitu ila mpumbavu ni mtu asiyetaka kujua hata baada ya kujuzwa
 
Umeongea ukweli wewe ni kama Mimi nimetia huko 150, sina muda wa kufanya biashara Wala hobby, nilijenga nyumba Kwa milioni 200 Kwa miaka 5 ikaisha , nimeweka mpangaji analipa laki nne Tena Kwa taabu , Bora ikae utt mana biashara Ina wenyewe
 
Uliweka sh ngapi????
 
mi ikifika tu 100mil naacha kibarua Cha serikari, maana nitakuwa teali hela ya pension nimepata 100mil, na gawio langu nakula 900K kama now navyopokea.. muda ninaotumia kuja kibaruanii, naubadilisha nautumia katika sekta nyingine.

Sasa mkuu umeitoa pesa yote 10mil, unauhakika utaipandishaa na hautoipoteza?

Maana Mimi siwazi kutoa pesa UTT nitakufa nitaziachaa, labda nikifikishaa miaka 70.
 

Iv UTT mtu akikufa,ndgu wanapata access ya kutoa uwekezaji wake?mana sijaona kwnye terms zao….anaejua tafadhali
 
Uko mfuko gani?
Mfuko upi wa UTT una faida kubwa na risk free?
 
Ingekuwa unawekeza kwa usd ingekuwa sana,tatizo shiling yetu yenyewe inashuka thamani.
Ukikaa useme uache miaka kadhaa unakuwa ni upuuzi tu
 

Inshallah tuombe mungu. Niliweka UTT wkt biashara iko vibaya. Now biashata iko vzr nahitaji kufanya biashara. Km biashara itakua hovyo tena tairudisha this around najua taweka nyingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…