Niliweka 20 million fixed deposit I&M bank in 2017. Nilikuw napata 2M per year. Kesho ngoja nitafute form nikutumie PM
It's loss achana nayo. Kuna swali nimemukiza Thabit hajanijib mpaka leo. Ten million uweke kwa 10 years au mpaka ustaafu hata kama itaongezeka ukijumlisha na inflation Je thaman ya hela yako itakuwepo?
Unajua 10 million today is worth more than 10 million tomorrow. Wana finance wanaelewa hii Na ukuaji wa Tsh 1 ni mdogo mno. .
Samahani kama nitakuudhi Niko radhi kukosolewa
Mkuu, UTT ina Mifuko 5 ya uwekezaji ambayo wewe utachagua. Huyu ndugu alichagua Bond Fund ambayo inatoa gawio kwa mwekezaji aliewekeza 10m+ kwa kila mwezi. Kumbuka unalipwa 1 Tsh per kipande kila mwezi ilihali pesa yako inaongezeka. Hapa mtoa mada amesema iliongezeka by 30K kwa mwezi wake wa kwanza ambapo alilipwa 86K kama gawio.
So, mifuko mingine ina utaratibu wake, but mara nyingi kama sio mara zote Pesa yako itaongezeka by 1% kwa mwezi ambapo kwa mwaka utakuwa na 12% (minimum, kuna mingine inaenda mpaka 14% soma kwenye mobile app yao)
Ulipoweka 20M bank kwenye fixed acc, ulipata 2M kwa mwaka ambayo ni 10% ila kwa UTT ungepata around 12% ya pesa yako kwa mwaka.
Pia, UTT AMIS ina Compund interest effect kwa mwezi, mfano, ikiwa una 1M mwezi huu Faida yako kwa mwezi huu ni around 10K
Then next month ukaongeza 100k kwenye account yako basi faida yako itakuwa 11k kwa mwezi unaofuata.
Mfano, Bond Fund bei ya kipande kwa takribani miezi 6 iliopita ilicheza 114-115Tsh, inapanda na kushuka kulingana na namna wanavyolipa gawio.
Then Mfuko wa Ukwasi wenyewe hauna gawio bei ya kipande ilikuwa around Tsh 341 mwezi December wakati mwezi huu ni around Tsh 348. Unaweza ona tofauti.
Pia ninavyoona UTT ni uwekezaji wa Muda mrefu ili uone reasonable profit.
Kwa waajiriwa, unaweza kuitumia kama sehemu ya kujiwekea Akiba. Mfano kila mwezi unaweka 100k. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na mtaji wa biashara au pesa ya ujenzi wa nyumba yako. Kumbuka UTT wanapokea kuanzia 5K kwa mwezi. Hatuna Kisingizio
Tutafute maarifa, yapo ni suala la wewe kuchukua hatua.
Jaribu kumfuatilia Somebody Ndahan Mwenda, anafundisha kuhusu uwekezaji wa hisa na masoko ya mitaji
Soma kitabu cha The Richest Man in Babylon. Utayakuta haya
Salam