greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
Mfuko wa wa uwekezaji wa pamoja a.k.a UTT mnamo tarehe 16/ 6 /2023 uliweza kufikisha thamani ya Shillingi Trillion moja na nusu (1,500,000,000,000/=).
Yaan kwa ufupi,mfuko huu umefika hadhi sawa na benki kubwa kama CRDB,NMB au kampuni ya wapendwa TBL...
Ndani ya mfuko huu kuna mifuko 6
1. Umoja Fund
2. Wekeza maisha
3. Watoto fund
4. Jikimu Fund
5. Liquid fund
6. Bond fund
Ukipata mda ujifunze juu ya Masoko ya mitaji....
1. UMOJA FUND - Ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na UTT-AMIS mnamo mwaka 2005. Mtu binafsi, taasisi (za kidini pia) vikundi vinaruhusiwa kuwekeza pia.
50% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye hisa na 50% kwenye hatifungani za serikali/makampuni
Kima cha chini cha kuwekeza ni kwanzia vipande 10
2. WEKEZA MAISHA - Ndiyo mfuko wa pili kuanzishwa na UTT-AMIS mnamo mwaka 2007, lengo la mfuko huu ni kukuza mtaji na pia kutoa bima ya maisha/afya kwa wawezaji, fidia za ulemavu/gharama za mazishi.
Uwekezaji wa vikundi hauruhusiwi, pia huwezi kutumia vipande vya mfuko huu kama amana katika kupata mkopo taasisi za kifedha kama vile benki.
Hakuna ukomo wa kuwekeza lakini ukomo wa Bima ni TZS 25,000,000 tu kwa mwekezaji anayepata shida ya kiafya na akapatiwa matibabu kwa Bima ya mfuko
3. WATOTO FUND, Ni mfuko maalum kwaajili ya watoto chini ya umri wa miaka 18, ambao ni kwaajili ya kuandaa kesho yao iliyo bora.
Uwekezaji unaweza fanywa kwa jina la mtoto mwenyewe, na kima cha chini cha kuanza ni TZS 10k tu, na anaweza kuwa anaendelea kuongeza uwekezaji kwa kiwango cha kuanzia TZS 5k tu na nakuendelea
4. JIKIMU FUND, Ni mfuko kwaajili ya wawekezaji wanaotaka kupata kipato kila mara (gawio) huku wakiendelea kukuza mtaji wao.
35% ya fedha za mfuko huu huwekezwa kwenye hisa, 65% kwenye hatifungani za serikali/kampuni na FDR
Kupata gawio la kila baada ya miezi 3 unapaswa kuwekeza TZS 2m na gawio la kila mwaka ni TZS 1m
5. LIQUID FUND, Ni mfuko kwaajili ya wanaotaka kuwekeza kipato chao cha ziada kwa lengo la kukuza ukwasi. Mfuko unajualikana kama mfuko wa ukwasi
Kima cha chini cha kuwekeza ni kwanzia TZS 100k kwa mara ya kwanza na baada ya hapo waweza kuwa unaongeza TZS 10k tu na kuendelea.
100% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye soko la fedha na hatifungani za serikali na kampuni.
6. BOND FUND, Ulianzishwa mwaka 2019 na 90% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye hatifungani.
Kima cha kuanza kuwekeza kwenye mfuko huu ni TZS 50k kwa lengo la kukuza mtaji pekee.
Pia kupata gawio la baada ya miezi 3 ni kuwekeza TZS 10m kwa mkupuo, na baada ya miezi 6 ni TZS 5m kwa mkupo. Kila kipande hupata gawio la TZS 1/Mwezi
Kwa ujumla UTT-AMIS ni sehemu salama kuwekeza kwasababu kila mfuko una meneja wake ambaye ana wajibu wa kulinda pesa za wawekezaji wa mfuko.
Pia, UTT-AMIS wanatoa riba ya wastani wa 12% mpaka 14.5% kwa kile ulichowekeza mwekezaji.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Ndahani N. Mwenda
&
Greaterthan