UTT una thamani zaidi ya Trillion 1.5

UTT una thamani zaidi ya Trillion 1.5

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Mfuko wa wa uwekezaji wa pamoja a.k.a UTT mnamo tarehe 16/ 6 /2023 uliweza kufikisha thamani ya Shillingi Trillion moja na nusu (1,500,000,000,000/=).

Yaan kwa ufupi,mfuko huu umefika hadhi sawa na benki kubwa kama CRDB,NMB au kampuni ya wapendwa TBL...

Ndani ya mfuko huu kuna mifuko 6
1. Umoja Fund
2. Wekeza maisha
3. Watoto fund
4. Jikimu Fund
5. Liquid fund
6. Bond fund

Ukipata mda ujifunze juu ya Masoko ya mitaji....

1. UMOJA FUND - Ni mfuko wa kwanza kuanzishwa na UTT-AMIS mnamo mwaka 2005. Mtu binafsi, taasisi (za kidini pia) vikundi vinaruhusiwa kuwekeza pia.
50% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye hisa na 50% kwenye hatifungani za serikali/makampuni
Kima cha chini cha kuwekeza ni kwanzia vipande 10

2. WEKEZA MAISHA - Ndiyo mfuko wa pili kuanzishwa na UTT-AMIS mnamo mwaka 2007, lengo la mfuko huu ni kukuza mtaji na pia kutoa bima ya maisha/afya kwa wawezaji, fidia za ulemavu/gharama za mazishi.
Uwekezaji wa vikundi hauruhusiwi, pia huwezi kutumia vipande vya mfuko huu kama amana katika kupata mkopo taasisi za kifedha kama vile benki.
Hakuna ukomo wa kuwekeza lakini ukomo wa Bima ni TZS 25,000,000 tu kwa mwekezaji anayepata shida ya kiafya na akapatiwa matibabu kwa Bima ya mfuko

3. WATOTO FUND, Ni mfuko maalum kwaajili ya watoto chini ya umri wa miaka 18, ambao ni kwaajili ya kuandaa kesho yao iliyo bora.
Uwekezaji unaweza fanywa kwa jina la mtoto mwenyewe, na kima cha chini cha kuanza ni TZS 10k tu, na anaweza kuwa anaendelea kuongeza uwekezaji kwa kiwango cha kuanzia TZS 5k tu na nakuendelea

4. JIKIMU FUND, Ni mfuko kwaajili ya wawekezaji wanaotaka kupata kipato kila mara (gawio) huku wakiendelea kukuza mtaji wao.
35% ya fedha za mfuko huu huwekezwa kwenye hisa, 65% kwenye hatifungani za serikali/kampuni na FDR
Kupata gawio la kila baada ya miezi 3 unapaswa kuwekeza TZS 2m na gawio la kila mwaka ni TZS 1m

5. LIQUID FUND, Ni mfuko kwaajili ya wanaotaka kuwekeza kipato chao cha ziada kwa lengo la kukuza ukwasi. Mfuko unajualikana kama mfuko wa ukwasi
Kima cha chini cha kuwekeza ni kwanzia TZS 100k kwa mara ya kwanza na baada ya hapo waweza kuwa unaongeza TZS 10k tu na kuendelea.
100% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye soko la fedha na hatifungani za serikali na kampuni.

6. BOND FUND, Ulianzishwa mwaka 2019 na 90% ya fedha za mfuko huu zinawekezwa kwenye hatifungani.
Kima cha kuanza kuwekeza kwenye mfuko huu ni TZS 50k kwa lengo la kukuza mtaji pekee.
Pia kupata gawio la baada ya miezi 3 ni kuwekeza TZS 10m kwa mkupuo, na baada ya miezi 6 ni TZS 5m kwa mkupo. Kila kipande hupata gawio la TZS 1/Mwezi
Kwa ujumla UTT-AMIS ni sehemu salama kuwekeza kwasababu kila mfuko una meneja wake ambaye ana wajibu wa kulinda pesa za wawekezaji wa mfuko.
Pia, UTT-AMIS wanatoa riba ya wastani wa 12% mpaka 14.5% kwa kile ulichowekeza mwekezaji.
Imeandaliwa na kuandikwa na

Ndahani N. Mwenda
&
Greaterthan
 
najitahidi kuuelewa huu mfuko but akili yangu imegoma 😵‍💫
Ni kwa ajili ya watu ambao sio RISK TAKER, kumwambia mjasiriamali aweke milioni 100 kila mwaka iwe inaleta milioni 15, au 7.5 kila miezi sita hakuelewi. Wakati akiagiza mzigo wa milioni 100 China, siku 90 imezaa mara mbili. 90% ya hiyo trillion 1.5 ni fedha za kifisadi kutoka serikalini na private sector. Mafisadi wengi hawataki usumbufu wa kuwekeza mtaani.
 
Ni kwa ajili ya watu ambao sio RISK TAKER, kumwambia mjasiriamali aweke milioni 100 kila mwaka iwe inaleta milioni 15, au 7.5 kila miezi sita hakuelewi. Wakati akiagiza mzigo wa milioni 100 China, siku 90 imezaa mara mbili. 90% ya hiyo trillion 1.5 ni fedha za kifisadi kutoka serikalini na private sector. Mafisadi wengi hawataki usumbufu wa kuwekeza mtaani.
1.So mfanyakazi wa serikalini afanye Ufisadi serikalini halafu akaweke fedha kwenye mfuko uliopo chini ya wizara ya fedha unaosimamiwa na benki kuu ambapo una unagnishwa na taarifa zako za Benki na NIDA

2.Unajua hata hiyo Trillion 1.5 ni nini na imepatikana vipi...?

3.Unajua hata namna ambavyo UTT inatengeneza faida....?

4.So kwa akili yako,kila pesa ya mfanya biashara huwa inaenda kwenye biashara,,,yaan mda wote ana current assets...?

5.Je,kila mtu ana mda wa kwenda china,mda wa kufanya biashara?

Tumia mda wako kujifunza zaidi....
 
Mfuko wa wa uwekezaji wa pamoja a.k.a UTT mnamo tarehe 16/ 6 /2023 uliweza kufikisha thamani ya Shillingi Trillion moja na nusu (1,500,000,000,000/=).

Yaan kwa ufupi,mfuko huu umefika hadhi sawa na benki kubwa kama CRDB,NMB au kampuni ya wapendwa TBL...

Ndani ya mfuko huu kuna mifuko 6
1. Umoja Fund
2. Wekeza maisha
3. Watoto fund
4. Jikimu Fund
5. Liquid fund
6. Bond fund

Ukipata mda ujifunze juu ya Masoko ya mitaji....
Hapo ni mfuko gani mzuri kwa uwekezaji🤔
 
najitahidi kuuelewa huu mfuko but akili yangu imegoma 😵‍💫
Haina haja ya kuwa na haraka....
Ukipata mda tembelea ofisi zao pale sukari house....tembelea websites yao....

Lakini pia jifunze juu ya mutual funds
 
Tuna dunda dunda tangu January this year mpk sasa mm n familia yangu tumekata nusu mwaka!! Tukisubili 6 month ya kufunga mwaka. Mambo sio haba kabisa. Na project zingine zikiendelea kwa amani kabisaa.








KAZI ni kipimo cha UTU
 
Another form of forex(forex in another version)
Yan kanakwamba unafananisha Mutual fund na FOrex,,,inaonesha ni jinsi hauna elimu ya uwekezaji mkuu....
Take your time jifunze kwa
  • youtube
  • articles
  • online courses
na hii siyo kwako tu,hata kwa watu wako wa karibu.
 
Nimeanza mwezi huu nimeweka milioni 30 Cash, matumaini yangu nifunge mwaka na milioni 50. Kuna mfuko wa Liquid naona thamani ya kipande inapanda kila kukicha hivyo ongezeko la fedha pindi thamani inavyopanda naiona vizuri kabisa.

Ushauri kama una fedha ambayo unajua huna mpango nao kwa sasa iweke tu huko utakuja nishukuru baadae..
 
najitahidi kuuelewa huu mfuko but akili yangu imegoma 😵‍💫
 
Back
Top Bottom