Mkuu, mnada wa mwaka huu wa Treasury bond za muda wa miaka 20 za BOT zimetangazwa kwa riba ya 15.49%. Sasa unavyosema "Government Bond wakitoa zaidi ya 10% achana nayo, ni ishara serikali haina uwezo wa kulipa" nashindwa kukuelewa. Toka miaka ya nyuma hizi Treasury bond huwa zinachezea 16% ila saivi ndio kama riba yake imepungua.
Inawezekana hati fungani za Benki kuu zinaanzia Tshs 1M, ila ukiwa na hela ndogo chini ya Tshs 1M, bado unaweza kuzinunua kupitia UTT. Wao wanakusanya hela za pamoja then wanaenda kununua hati fungani BOT. Mfuko wa UTT ambao lengo lake ni kununua hatifungani unaitwa BOND FUND. Sasa unasemaje UTT hawahusiki na hati fungani na huku wanawekeza huko?.
Uko sahihi kusema UTT ni mutual fund (mfuko wa pamoja), ila swali ni wanawekeza wapi? (Mpaka sasa kuna mifuko 6 na kila mfuko una sehemu yake ambayo fedha zilizokusanywa pamoja zinaenda kuwekezwa)
N.B
MFUKO WA HATI FUNGANI WA UTT, 90% YA HELA ZINAZOKUSANYWA LENGO NI KUWEKEZWA KWENYE HATI FUNGANI (Bank, BOT, Mashirika n,k)
View attachment 3019699