Utuaji ndege wasimamisha mechi ya Azam na Dodoma jiji

Wakati wa ndege kutua usiku rubani huongozwa na taa zinazomwonyesha mwanzo na mwisho wa uwanja ikiwa ni pamoja na pembeni runway ilipoishia. Ni tofauti na mchama ambapo huongozwa na ile mistari myeupe iliyochorwa kwenye njia ya ndege kutua.

Sasa turudi kwanini taa za uwanja wa mpira kuzimwa.

Taa zinazimwa kwa vile zinaweza kumchanga dereva wa ndege (rubani) asijue upi ni uwanja halisi wa ndege na anaanzia wapi kushuka. Ukiangalia Uwanja wa ndege na Uwanja wa mpira vipo karibu vikitenganishwa na round about tu. Hivyo inahatarisha usalama wa ndege kutua usiku wakati taa za uwanja wa mpira zikiwaka.

Uwanja wa ndege Mwanza upande mmoja unaishia ziwani kama ilivyo kwa uwanja wa Bukoba na Entebbe Uganda. Kuna wavuvi wa dagaa walipanga karabai zao ziwani zikampoteza maboya rubani na kutua ziwani akidhani ni taa za kuongoza ndege. Bahati pia ilikuwa ni ndege ya mizigo.

Sasa kwa usalama pia wa wachezaji wa mpira na mashabiki wao hapo Dodoma, ilikuwa muhimu kuzima taa maana ingesababisha rubani atue Jamhuri Stadium na kuleta maafa.

Ni hivyo tu.
Maelezo mazuri kama ni hivyo walikuawa sahihi maana viwanja vipo karibu sana.
 
Wakati mechi ya Azam na Dodoma jiji inaendelea hapa uwanja wa Jamhuri Dodoma. Linatokea tangazo la waendesha uwanja kuwa taa zote za uwanjani zitazimwa Ili ndege itue kwenye uwanja ulio karibu na uwanja huo Wa mpira.

Hii imekaaje kisheria?
Tanzania ni channel ya futuhi
 
Wakati wa ndege kutua usiku rubani huongozwa na taa zinazomwonyesha mwanzo na mwisho wa uwanja ikiwa ni pamoja na pembeni runway ilipoishia. Ni tofauti na mchama ambapo huongozwa na ile mistari myeupe iliyochorwa kwenye njia ya ndege kutua.

Sasa turudi kwanini taa za uwanja wa mpira kuzimwa.

Taa zinazimwa kwa vile zinaweza kumchanga dereva wa ndege (rubani) asijue upi ni uwanja halisi wa ndege na anaanzia wapi kushuka. Ukiangalia Uwanja wa ndege na Uwanja wa mpira vipo karibu vikitenganishwa na round about tu. Hivyo inahatarisha usalama wa ndege kutua usiku wakati taa za uwanja wa mpira zikiwaka.

Uwanja wa ndege Mwanza upande mmoja unaishia ziwani kama ilivyo kwa uwanja wa Bukoba na Entebbe Uganda. Kuna wavuvi wa dagaa walipanga karabai zao ziwani zikampoteza maboya rubani na kutua ziwani akidhani ni taa za kuongoza ndege. Bahati pia ilikuwa ni ndege ya mizigo.

Sasa kwa usalama pia wa wachezaji wa mpira na mashabiki wao hapo Dodoma, ilikuwa muhimu kuzima taa maana ingesababisha rubani atue Jamhuri Stadium na kuleta maafa.

Ni hivyo tu.
Teknolojia iliyopo leo bado rubani atachanganywa na taa? GPS na ILS hazitamuonyesha path sahihi ya airport?

Taa za runway si zina utaratibu na rangi maalum na kuna zile PAPI pembeni? Unaweza kuzichanganya na taa za uwanja wa mpira ambao ni 100m na wakati runway zinaenda mpaka 3km
 
Rubani alikua amelewa
 
Sasa ni wakati wa huu uwanja wa ndege kuhama hapa mjini kati jamani..kuna siku ndege imenipitia kichwani shwaaaa....
Sasa si mara moja moja uwe unatembea ili uangalie ule uwanja mkubwa wa ndege wa Msalato umefikia hatua gani!!

Unaishi Dodoma, ila muda wote unafungiwa ndani kama kuku wa kisasa! Wewe Kalpana vipi bhana!! Uwe unanitafuta kwa siri nikija Dodoma, nikupeleke mnadani ukale nyama za kuchoma.
 
Wakati wa ndege kutua usiku rubani huongozwa na taa zinazomwonyesha mwanzo na mwisho wa uwanja ikiwa ni pamoja na pembeni runway ilipoishia. Ni tofauti na mchama ambapo huongozwa na ile mistari myeupe iliyochorwa kwenye njia ya ndege kutua.

Sasa turudi kwanini taa za uwanja wa mpira kuzimwa.

Taa zinazimwa kwa vile zinaweza kumchanga dereva wa ndege (rubani) asijue upi ni uwanja halisi wa ndege na anaanzia wapi kushuka. Ukiangalia Uwanja wa ndege na Uwanja wa mpira vipo karibu vikitenganishwa na round about tu. Hivyo inahatarisha usalama wa ndege kutua usiku wakati taa za uwanja wa mpira zikiwaka.

Uwanja wa ndege Mwanza upande mmoja unaishia ziwani kama ilivyo kwa uwanja wa Bukoba na Entebbe Uganda. Kuna wavuvi wa dagaa walipanga karabai zao ziwani zikampoteza maboya rubani na kutua ziwani akidhani ni taa za kuongoza ndege. Bahati pia ilikuwa ni ndege ya mizigo.

Sasa kwa usalama pia wa wachezaji wa mpira na mashabiki wao hapo Dodoma, ilikuwa muhimu kuzima taa maana ingesababisha rubani atue Jamhuri Stadium na kuleta maafa.

Ni hivyo tu.
Na hii sio mara ya kwanza kutokea haya. Hata mechi iliyopita aliyocheza Dodoma home ilikua hivi hivi pia.

Ratiba za ndege zinajulikana. Kama ndege hiyo hupita hapo muda huo huo kila siku basi bodi ya ligi i-adjust ratiba za mechi za Dodoma Jiji ili ziendane na hizo ratiba za ndege.

Mechi iliyopita ilisimama kama dakika 10 hivi maana zinaanza kuzimwa ndege ikiwa mbali kabisa na mpaka ipite labda itue kabisa ndio muendelee. Hapa ni kama halftime ingine hii.

Kuna siku hata taa zitazimwa watu wakiwa kwenye movie ya goli. Yaan mnasubiri mpira utoke nje ndio mzime na hautoki na ndege ndio inakaribia mnaamua kuzima hivyo hivyo.
 
Shark umetoa hoja kubwa Sana. Kwamba vipi taa ziwe zinatakiwa kuzimwa wakati mojowapo ya timu iwe kwenye harakati za kufunga goli?
 
Ndugu zanguni muamishe kimojawapo hapo, isije siku ikatua uwanjani kwenye vichwa vya watu itakuwa ni kesi nyingine
 
Teknolojia iliyopo leo bado rubani atachanganywa na taa? GPS na ILS hazitamuonyesha path sahihi ya airport?

Taa za runway si zina utaratibu na rangi maalum na kuna zile PAPI pembeni? Unaweza kuzichanganya na taa za uwanja wa mpira ambao ni 100m na wakati runway zinaenda mpaka 3km
🤣🤣😂
Elezea vizuri injinia. Mwisho wa siku utakuja kuuliza mbona taa za mji wa Dar hazizimwi ndege ikiwa inatua?

Wewe elewa hivyo tu kwa sasa taa za uwanja zinazimwa kwasababu ndege inatua. Tambua wakati wa ndege kutua na kupaa anaefanya kazi kubwa ni rubani na sio auto pilot na maGPS na ma LS.

Lete ujuaji wako sasa kama hatutashudia ndege inatua golini kwa Dodoma jiji siku hiyo.

Ulishawahi kusikia ndege imeshindwa kutua, tena mchana kwasababu ya hali mbaya ya hewa dereva/rubani haoni runway inaanzia wapi aanze kushuka. Au ruban kaishusha ndege nyuma ya inapoanzia runway. Kama ingekuwa anategemea hizo GPS na LS wakati wa kutua, katika hali mbaya ya hewa kwanini aamue kutafuta sehem nyingine ya kwenda kutua?

Hii hutokea sana kwa abiria wanaoenda Bukoba. Wasafiri wa mara kwa mara wa ndege kwenda Bukoba hiki ninachokisema watakuwa wanakielewa vizuri zaidi
 
Back
Top Bottom