Utumbo wa ng'ombe biashara inayodhalaurika yenye faida karibia na mtu anaemiliki bajaji 1 au zaidi ya bodaboda 1, Inahitaji mtaji mdogo

Utumbo wa ng'ombe biashara inayodhalaurika yenye faida karibia na mtu anaemiliki bajaji 1 au zaidi ya bodaboda 1, Inahitaji mtaji mdogo

RUSTEM PASHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2016
Posts
4,707
Reaction score
11,365
Hasa kwa vijana wanaokaa DSM ambapo biashara ya nyama(bucha) haifungamani na utumbo.

Kwa wale wenye mitaji midogo pungufu ya laki 6 ningeomba kidogo wajaribu kufanya uchunguzi wa biashara ya utumbo.

Ukiwa na shillingi laki 6, nenda katengeneze kabati lakio laki 2, Muzani laki moja na nusu, eneo lakuuzia elfu 10 kwa mwezi, nenda kanunue utumbo. Bei ya utumbo kwa kg 1 wanauza elfu moja miatano machinjioni, wewe ukishauchukua uza elfu tatu kwa kg 1 ingawa sehemu zingine wanauza elfu 4 kwa kg 1, mwanzoni patakuwa na changamoto lakini wakishazoea utapiga pesa kiasi.

Ukiuza kwa siku kg 20 utakuwa na faida ya elfu 30 au elfu 25 kwahiyo hapo utakuwa umejiongezea kipato kwa kiasi Fulani.Kuhusu pakuuweka ukibaki ongea na mwenye bucha atakuhifadhia kama ukibaki.

Mimi binafsi nilimpa kazi hii kijana na kwa wiki ananipa elfu 50 ,kwa mwezi laki 2.Hiki kibiashara kufikia sasa kinanilipia kodi ya chumba,umeme,maji kwa mwezi halafu mie nahangaika na mambo mengine.

Leo nimefungua banda la 2 la utumbo nimemuweka pia kijana mwingine, nimeona changamoto nindogo sana kulingana na biashara nyingine ndogondogo zakuwapa vijana wasimamie.

Changamoto hapa nikuamka mapema saa kumi na kuufata machinjioni, ingawa ukimpa kijana ataufata yeye mwenyewe.

Pia ukiweza uza na supu ya utumbo(hii mada ya siku nyingine).

Asenteni.
 
Hii biashara inalipa kwa dar,mikoani huwezi fanya
Tatizo watu hawajui kuwa nyama inapaswa iuzwe kivyake na utumbo kivyake. Unataka kusema mikoani watu hawanywi supu au kila mmoja ana uwezo wa kununua nyama. Mbezi beach hakuna anayeuza utumbo wakati watu tunautafuta kila asubuhi wapi.

Pale Ushirombo mara nyingi tukipita asubuhi kuna kibanda cha supu ya utumbo wa mbuzi na chapati. Ukifika saa nne tayari imeisha. Nadhani hata ya ng'ombe ipo ila mimi huwa napenda utumbo wa mbuzi.
Hata vijijini siku hizi vijana jioni wanapenda supu wakati wa kukata maji yao hivyo tuchangamkie hii kitu.
Big up mleta mada.
 
Back
Top Bottom