Financial Freedom
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 1,246
- 2,299
TRA sikuhizi basic salary 900k ndo watu wanakimbilia hiyo? TRA ilikuwa zamani before salary review ya Magufuli
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili nililiona aisee, watu hawajui ramani ya majengo ilivyo. Wakiona majengo mlimani tu wanaenda kuulizia kama ndio hapo.Mimi ni mhanga,umeongea ya ukweli Kabisa yani..
Ile asubuhi tuu kupata venue nimetumia 20k Kwa ajili ya boda tuu yani.
Dodoma was not ready for us.
Labda wamefuata wazo la wakubwa wao (Serikali), lakini haikua lazima kuanzia Dodoma katika hatua hizi za awali. Wangewaita hata kwenye hatua za mbele wakiwa wachache.Sekretarieti ina viongozi vilaza sijui kwanini bado wapo kazini....wazo la kuhamia Dodoma lilikuwa la kijuha sana
Poleni kwa usumbufu jman, Ila kwa mawazo yangu mimi kufanya mtihani dar bora Dodoma kwa sababu Dodoma ni katikati, hata kama unatoka mkoa gani ulazima wa kufika siku hiyo upo hata kwa kuchelewa, tofauti na dar ambapo mikoa mwingine inatumika siku mbili.Hmn bas watu hawakutafuta guest Sana mm nililal mitaa ya nyerere square nilikuta vyumba na vinginevyo vilikuwa havina watu. All in all watu walizid Sana kwasababu watu wanatamani Sana kufanya Kaz TrA
Love story tena kaka, nilikua nina issues nyingi za kuandika about that event. Sikua msahiliwa lakini that day nilipata muda mrefu Sana wa ku study Yale matukio.Mwana ulivotiririka utadhan love story hahaha
Poleni kwa usumbufu jman, Ila kwa mawazo yangu mimi kufanya mtihani dar bora Dodoma kwa sababu Dodoma ni katikati, hata kama unatoka mkoa gani ulazima wa kufika siku hiyo upo hata kwa kuchelewa, tofauti na dar ambapo mikoa mwingine inatumika siku mbili.
Na kuhusu Suala la kutafuta venue, ni koss la msailiwa kwa sababu unapojiandaa kwa interview yoyote inabidi ufahamu sehemu ya kufanyia mtihani kabla ya siku yenyewe.
All in all tunawaombea matokeo mema
Brother kwa aliekuwepo pale Mazingira yalikua ni magumu ajabu. Ni kama kupeana adhabu fulan au kukomoana hivi. Mimi nilishiriki lile zoezi ingawa sikua msahiliwa nimeona.Dar ni mbali kidogo lkn watu wengi wana ndg na jamaa Dar kuliko huko Dom hivyo hata gharama za kulala lodge zinakua hazipo tofauti kabisa na Dom na pia Dar imaweza ku accommodate hao maelfu ya watu at a go.Dodoma ni utopolo.
Unaongea kirahisi tu,mtu ametoka huko mkoani ameingia jioni,atoke hapo lodge akodi boda kutafuta huo ukumbi arudi nayo tena na hio boda mpk lodge hizo gharama unajua ni sh. Ngapi na kesho asubuhi apande tena bodaboda kwenda na kurudi tena?
kwani pepa zinalipiwa?Hawajataka kupiga pesha.
Hapo tukikadiria matumizi ni 10M tu kwa zonal moja (mathalani Dar) kwa kuandaa pepa, ukumbi, wasimamizi, inayobaki(40M) ni kibindoni
Bila shaka hujasoma mtiririko wa comments.kwani pepa zinalipiwa?
Daahh2016.Nilishasafir kwakuunga unga ivo nikafika dar asubuh kutoka Arusha nafika kimara ikabidi nishike boda Hadi kingamboni interview ilikua pale chuo Cha Mwl Nyerere.napanda Panton nafika nakutana na watu washapiga pepa na stl ndo inaondoka na wasimamizi
Sahihi kabisa,Bila shaka hujasoma mtiririko wa comments.
Pepa hailipiwi, kutokana na usumbufu ambao watu wanaupata jinsi alivyoelezea mleta mada, tunaona ni bora pepa zifanyike kwenye kanda halafu walipishwe kidogo ili kusaidia maandalizi ya huo mtihani(ukumbi, wasimamizi n.k)
Mfano mtu akiwa Dar akalipia 5,000/= tu akaletewa pepa Dar, ni nafuu kuliko na aende Dodoma ambapo atagharamia usafiri(go and return), malazi, chakula, n.k
Sijaelewa kitu apaWakuu Kwema?
Mimi kwa Sasa niko Dodoma kikazi, mnamo ijumaa Usiku alinipigia Jamaa yangu mmoja akaniambia mdogo wake kaja Dodoma kufanya Interview lakini kakosa pa kulala, hivyo anaomba nimu accommodate sababu kashatafuta chumba kakosa. Kwakua alienipigia ni Mshikaji wangu sana nkaona isiwe tabu, dogo atapata pa kulala na sehemu za Monde, Nyama Choma, na hata mambo mengine yale akitaka namuonyesha tu.
Dogo akafika saa nane usiku kachoka hoi anadai kadandia lift kaunga gari mbili mpaka pale. Akadai mtiti wa watu aliouacha Mbezi Stand ulikua sio wa kawaida, abiria wanapanda Saratoga wanalipishwa nauli mpaka 35,000/- wakati ki uhalali ni 20,000/- tu. Wengine barabaran wanasubiri Gari za lift.
Dogo akazidi kudai ashazunguka sana vyumba hakuna, eti kuna mpaka wadada waliokua wakilala kwenye vyumba vya wanaume ambao hawakua wao.
Yaan mtu anasikia mdada anaulizia mapokezi kuhusu chumba anatoka anamwambia mdada waunganishe tu nguvu hata wanaweza kupiga discussion usiku. Yaliyoendelea kwenye hizo "discussion" za kustukizana mie sikuwepo.
Asubuhi nkasema nimpeleke dogo huko Udom sababu Usafiri ulikua wa tabu Sana na ilikua Saturday sikua na mishe zingine. Njiani karibu na Njia Panda ya Social foleni ilikua ni kubwa ki Dodoma Dodoma, lakini tulifika. Nilichogundua wageni walikua ni wengi kwa kumbi zilizokua zikifanyia mitihani, wengi wao waliishia kulipia bodaboda mara mbili mbili wakati wanatafuta kumbi husika walizopangiwa. Kumbi zilikua hata 20 na zingine ziko umbali hata wa kutumia Gari au bodaboda.
Pale Udom kwa sasa chuo kimefungwa. Hakuna kantini, hakuna duka wala kiosk. Watu wametoka makwao (guest houses/lodges) toka alfajir hawajala wala kunywa chochote. Hata ukisikia kiu unafanya tu kumeza mate. Angalau kuishi kwangu Dom nafaham vijiji vya jirani na chuo hivyo dogo wake mshikaji nikampelekea wanapaita Nong'ona baada ya pepa ya Kwanza. Wengine niliona wakipiga mihayo tu, kadhaa nkatoka nao wengine wachache nkafanya kuwaambia tu.
Nje ya vyumba vya mitihani tahadhari ya Corona haikuwepo. Distance ya 1meter kati ya mtu na mtu haikuwepo Kabisa. Sio kwenye kusubiri tu, hata mistari ya foleni ya kukaguliwa hakukua na hii tahadhari. Ni kama mkazo uliwekwa kwenye barakoa tu, sio distance maintaining.
Kisha akaingiapepa ya pili, then tukarud town. Usafiri ulikua shida Sana, watu walipanda mpaka Toyo/Guta kurud mjini. Nilichukua kadhaa, wajawazito wawili na mmoja Dogo alisema anamjua wamemaliza nae. Kuhusu ugumu wa mtihani hilo namuachia dogo Mwenyewe ila watu walipata tabu kweli.
Lakina labda tufanye hesabu kidogo, Dogo anasema pepa ya Kwanza aliofanya waliitwa around 9,000 na ya pili hivyo hivyo nazan, tukiweka assumption kwamba wa huku ndio wa kule basi tuseme walikua hao hao 9,000. Na labda 2,000 hawakuja. Kwa ngazi ya Diploma (Wale Assistants) labda nao 3,000 hivi approximately. Hiv kweli Dodoma ina Guest houses za kutosha watu 10,000?? Guest/Lodge moja ikichukua wageni 10 basi zitahitajika guests 1,000 kubeba huu umati, zipo kweli hizi hapa Dodoma?
Dogo alihitajika kurudi jana,gari hakuna zimejaa. Sema kuna mdau mwenzangu hapa Job alikua anaenda Dar na Private nikamuombea lift. Dogo anasema jana njiani alikutana na watu wengi tu wakisimamisha magari kuomba lift. Jamaa aliekua nae alibeba watatu kwa 30,000 each. Mwenzake aliemuona kule Udom ali book na return kumbe.
Naandika huu uzi nikijiuliza swali moja tu, why ilikua lazima kuwajaza watu wote hawa Dodoma? Hakukua na uwezekano wa tume kutumia office zake za zonal? Mbona wakati tume Iko Dar es Salaam wale wa mikoani walishawahi kufanyia mitihani huko waliko? Si ni hata bas mngewaita Dodoma kipindi cha Oral wakiwa wameshachujwa wamebaki wachache? Ni Ubinafsi gani kwa wao kuokoa Gharama huku wakiwatesa watahiniwa kiasi kile?