Mazindu Msambule
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 7,510
- 6,877
Nadhani mshkaji katolea mfano hata wa ilivyokua Dar, watahiniwa ilikua sio lazima waje Dar, zone offices zilifanya kazi, why kipindi hiki utumishi from Dodoma hawakuona hilo? Kwanini zonal offices hazikufanya hiyo kazi badala ya kumtoa mtu mkoani huko na kumpeleka Dodoma? Fikira mtu atoke Kigoma kwenda kwa interview Dar?? Kweli??Ujinga wa meko kukimbilia Dodoma Mapema.
Utumishi kama wanataka hela za bure basi wapitis huu UziSahihi kabisa,
Ufuate pepa ya bure Dodoma lakini ugharamikie Guest House/Lodge siku 2 x 20,000 = 40,000/-.
Nauli Go & Return 22,000 x 2 = 44,000/-,
Kula njiani wakati wa Safari 10,000/-
Bodaboda za kutafuta ukumbi TZS 5,000/-
Au uletewe pepa Mkoa ulipo kwa gharama ya 5,000/- na nauli yako ya kwenda chumba Cha mtihani kipi bora?
Tena hapa Gharama nimeweka zile minimum kabisa
Hizi ndio athari za kukwepa kuchoma mishikaki ya 200. Au kuchoma mahindi stendi kwa kujivika taji la usomi!😅Wakuu Kwema?
Mimi kwa Sasa niko Dodoma kikazi, mnamo ijumaa Usiku alinipigia Jamaa yangu mmoja akaniambia mdogo wake kaja Dodoma kufanya Interview lakini kakosa pa kulala, hivyo anaomba nimu accommodate sababu kashatafuta chumba kakosa. Kwakua alienipigia ni Mshikaji wangu sana nkaona isiwe tabu, dogo atapata pa kulala na sehemu za Monde, Nyama Choma, na hata mambo mengine yale akitaka namuonyesha tu.
Dogo akafika saa nane usiku kachoka hoi anadai kadandia lift kaunga gari mbili mpaka pale. Akadai mtiti wa watu aliouacha Mbezi Stand ulikua sio wa kawaida, abiria wanapanda Saratoga wanalipishwa nauli mpaka 35,000/- wakati ki uhalali ni 20,000/- tu. Wengine barabaran wanasubiri Gari za lift.
Dogo akazidi kudai ashazunguka sana vyumba hakuna, eti kuna mpaka wadada waliokua wakilala kwenye vyumba vya wanaume ambao hawakua wao.
Yaan mtu anasikia mdada anaulizia mapokezi kuhusu chumba anatoka anamwambia mdada waunganishe tu nguvu hata wanaweza kupiga discussion usiku. Yaliyoendelea kwenye hizo "discussion" za kustukizana mie sikuwepo.
Asubuhi nkasema nimpeleke dogo huko Udom sababu Usafiri ulikua wa tabu Sana na ilikua Saturday sikua na mishe zingine. Njiani karibu na Njia Panda ya Social foleni ilikua ni kubwa ki Dodoma Dodoma, lakini tulifika. Nilichogundua wageni walikua ni wengi kwa kumbi zilizokua zikifanyia mitihani, wengi wao waliishia kulipia bodaboda mara mbili mbili wakati wanatafuta kumbi husika walizopangiwa. Kumbi zilikua hata 20 na zingine ziko umbali hata wa kutumia Gari au bodaboda.
Pale Udom kwa sasa chuo kimefungwa. Hakuna kantini, hakuna duka wala kiosk. Watu wametoka makwao (guest houses/lodges) toka alfajir hawajala wala kunywa chochote. Hata ukisikia kiu unafanya tu kumeza mate. Angalau kuishi kwangu Dom nafaham vijiji vya jirani na chuo hivyo dogo wake mshikaji nikampelekea wanapaita Nong'ona baada ya pepa ya Kwanza. Wengine niliona wakipiga mihayo tu, kadhaa nkatoka nao wengine wachache nkafanya kuwaambia tu.
Nje ya vyumba vya mitihani tahadhari ya Corona haikuwepo. Distance ya 1meter kati ya mtu na mtu haikuwepo Kabisa. Sio kwenye kusubiri tu, hata mistari ya foleni ya kukaguliwa hakukua na hii tahadhari. Ni kama mkazo uliwekwa kwenye barakoa tu, sio distance maintaining.
Kisha akaingiapepa ya pili, then tukarud town. Usafiri ulikua shida Sana, watu walipanda mpaka Toyo/Guta kurud mjini. Nilichukua kadhaa, wajawazito wawili na mmoja Dogo alisema anamjua wamemaliza nae. Kuhusu ugumu wa mtihani hilo namuachia dogo Mwenyewe ila watu walipata tabu kweli.
Lakina labda tufanye hesabu kidogo, Dogo anasema pepa ya Kwanza aliofanya waliitwa around 9,000 na ya pili hivyo hivyo nazan, tukiweka assumption kwamba wa huku ndio wa kule basi tuseme walikua hao hao 9,000. Na labda 2,000 hawakuja. Kwa ngazi ya Diploma (Wale Assistants) labda nao 3,000 hivi approximately. Hiv kweli Dodoma ina Guest houses za kutosha watu 10,000?? Guest/Lodge moja ikichukua wageni 10 basi zitahitajika guests 1,000 kubeba huu umati, zipo kweli hizi hapa Dodoma?
Dogo alihitajika kurudi jana,gari hakuna zimejaa. Sema kuna mdau mwenzangu hapa Job alikua anaenda Dar na Private nikamuombea lift. Dogo anasema jana njiani alikutana na watu wengi tu wakisimamisha magari kuomba lift. Jamaa aliekua nae alibeba watatu kwa 30,000 each. Mwenzake aliemuona kule Udom ali book na return kumbe.
Naandika huu uzi nikijiuliza swali moja tu, why ilikua lazima kuwajaza watu wote hawa Dodoma? Hakukua na uwezekano wa tume kutumia office zake za zonal? Mbona wakati tume Iko Dar es Salaam wale wa mikoani walishawahi kufanyia mitihani huko waliko? Si ni hata bas mngewaita Dodoma kipindi cha Oral wakiwa wameshachujwa wamebaki wachache? Ni Ubinafsi gani kwa wao kuokoa Gharama huku wakiwatesa watahiniwa kiasi kile?
TRA toka kitambo inajulikana ni sehemu yenye ulaji na dili chafu nyingi 😅Hmn bas watu hawakutafuta guest Sana mm nililal mitaa ya nyerere square nilikuta vyumba na vinginevyo vilikuwa havina watu. All in all watu walizid Sana kwasababu watu wanatamani Sana kufanya Kaz TrA
Duh kumbe na wewe uko kitaa mrembo? Pole sana aiseeMimi ni mhanga,umeongea ya ukweli Kabisa yani..
Ile asubuhi tuu kupata venue nimetumia 20k Kwa ajili ya boda tuu yani.
Dodoma was not ready for us.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Kwa taarifa yako kipindi cha Magufuli TRA ndio waliongezewa maradufuTRA sikuhizi basic salary 900k ndo watu wanakimbilia hiyo? TRA ilikuwa zamani before salary review ya Magufuli
Unafanya kazi TRA? Unajua salary review taasisi zipi ziliondolewa posho nyingi na mishahara ikapunguzwa? Magufuli aongeze mshahara? Hahahah hujui tu,uliza TPA,TPDC,TRA kilichowapataJambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Kwa taarifa yako kipindi cha Magufuli TRA ndio waliongezewa maradufu
Mkuu naongelea kitu nna uhakika nacho kwa TRA hizo taasisi zingine sina uhakikaUnafanya kazi TRA? Unajua salary review taasisi zipi ziliondolewa posho nyingi na mishahara ikapunguzwa? Magufuli aongeze mshahara? Hahahah hujui tu,uliza TPA,TPDC,TRA kilichowapata
nimekuelewa kaka shukrani.Bila shaka hujasoma mtiririko wa comments.
Pepa hailipiwi, kutokana na usumbufu ambao watu wanaupata jinsi alivyoelezea mleta mada, tunaona ni bora pepa zifanyike kwenye kanda halafu walipishwe kidogo ili kusaidia maandalizi ya huo mtihani(ukumbi, wasimamizi n.k)
Mfano mtu akiwa Dar akalipia 5,000/= tu akaletewa pepa Dar, ni nafuu kuliko na aende Dodoma ambapo atagharamia usafiri(go and return), malazi, chakula, n.k
Unafanya kazi TRA? Unajua salary review taasisi zipi ziliondolewa posho nyingi na mishahara ikapunguzwa? Magufuli aongeze mshahara? Hahahah hujui tu,uliza TPA,TPDC,TRA kilichowapata
Mwendo ndo ule ule mkuu izo review ni tishia tishia tu nyie wananchi na posho zikizotolewa ni ulaghai ila watu wanakula maisha kama kawaUnafanya kazi TRA? Unajua salary review taasisi zipi ziliondolewa posho nyingi na mishahara ikapunguzwa? Magufuli aongeze mshahara? Hahahah hujui tu,uliza TPA,TPDC,TRA kilichowapata
Kuokoa gharama zaidi, hata wasimamizi waliomba msaada UDOM na ile ya chuo cha Mipango waliwaomba huko Mipango!!Wakuu Kwema?
Mimi kwa Sasa niko Dodoma kikazi, mnamo ijumaa Usiku alinipigia Jamaa yangu mmoja akaniambia mdogo wake kaja Dodoma kufanya Interview lakini kakosa pa kulala, hivyo anaomba nimu accommodate sababu kashatafuta chumba kakosa. Kwakua alienipigia ni Mshikaji wangu sana nkaona isiwe tabu, dogo atapata pa kulala na sehemu za Monde, Nyama Choma, na hata mambo mengine yale akitaka namuonyesha tu.
Dogo akafika saa nane usiku kachoka hoi anadai kadandia lift kaunga gari mbili mpaka pale. Akadai mtiti wa watu aliouacha Mbezi Stand ulikua sio wa kawaida, abiria wanapanda Saratoga wanalipishwa nauli mpaka 35,000/- wakati ki uhalali ni 20,000/- tu. Wengine barabaran wanasubiri Gari za lift.
Dogo akazidi kudai ashazunguka sana vyumba hakuna, eti kuna mpaka wadada waliokua wakilala kwenye vyumba vya wanaume ambao hawakua wao.
Yaan mtu anasikia mdada anaulizia mapokezi kuhusu chumba anatoka anamwambia mdada waunganishe tu nguvu hata wanaweza kupiga discussion usiku. Yaliyoendelea kwenye hizo "discussion" za kustukizana mie sikuwepo.
Asubuhi nkasema nimpeleke dogo huko Udom sababu Usafiri ulikua wa tabu Sana na ilikua Saturday sikua na mishe zingine. Njiani karibu na Njia Panda ya Social foleni ilikua ni kubwa ki Dodoma Dodoma, lakini tulifika. Nilichogundua wageni walikua ni wengi kwa kumbi zilizokua zikifanyia mitihani, wengi wao waliishia kulipia bodaboda mara mbili mbili wakati wanatafuta kumbi husika walizopangiwa. Kumbi zilikua hata 20 na zingine ziko umbali hata wa kutumia Gari au bodaboda.
Pale Udom kwa sasa chuo kimefungwa. Hakuna kantini, hakuna duka wala kiosk. Watu wametoka makwao (guest houses/lodges) toka alfajir hawajala wala kunywa chochote. Hata ukisikia kiu unafanya tu kumeza mate. Angalau kuishi kwangu Dom nafaham vijiji vya jirani na chuo hivyo dogo wake mshikaji nikampelekea wanapaita Nong'ona baada ya pepa ya Kwanza. Wengine niliona wakipiga mihayo tu, kadhaa nkatoka nao wengine wachache nkafanya kuwaambia tu.
Nje ya vyumba vya mitihani tahadhari ya Corona haikuwepo. Distance ya 1meter kati ya mtu na mtu haikuwepo Kabisa. Sio kwenye kusubiri tu, hata mistari ya foleni ya kukaguliwa hakukua na hii tahadhari. Ni kama mkazo uliwekwa kwenye barakoa tu, sio distance maintaining.
Kisha akaingiapepa ya pili, then tukarud town. Usafiri ulikua shida Sana, watu walipanda mpaka Toyo/Guta kurud mjini. Nilichukua kadhaa, wajawazito wawili na mmoja Dogo alisema anamjua wamemaliza nae. Kuhusu ugumu wa mtihani hilo namuachia dogo Mwenyewe ila watu walipata tabu kweli.
Lakina labda tufanye hesabu kidogo, Dogo anasema pepa ya Kwanza aliofanya waliitwa around 9,000 na ya pili hivyo hivyo nazan, tukiweka assumption kwamba wa huku ndio wa kule basi tuseme walikua hao hao 9,000. Na labda 2,000 hawakuja. Kwa ngazi ya Diploma (Wale Assistants) labda nao 3,000 hivi approximately. Hiv kweli Dodoma ina Guest houses za kutosha watu 10,000?? Guest/Lodge moja ikichukua wageni 10 basi zitahitajika guests 1,000 kubeba huu umati, zipo kweli hizi hapa Dodoma?
Dogo alihitajika kurudi jana,gari hakuna zimejaa. Sema kuna mdau mwenzangu hapa Job alikua anaenda Dar na Private nikamuombea lift. Dogo anasema jana njiani alikutana na watu wengi tu wakisimamisha magari kuomba lift. Jamaa aliekua nae alibeba watatu kwa 30,000 each. Mwenzake aliemuona kule Udom ali book na return kumbe.
Naandika huu uzi nikijiuliza swali moja tu, why ilikua lazima kuwajaza watu wote hawa Dodoma? Hakukua na uwezekano wa tume kutumia office zake za zonal? Mbona wakati tume Iko Dar es Salaam wale wa mikoani walishawahi kufanyia mitihani huko waliko? Si ni hata bas mngewaita Dodoma kipindi cha Oral wakiwa wameshachujwa wamebaki wachache? Ni Ubinafsi gani kwa wao kuokoa Gharama huku wakiwatesa watahiniwa kiasi kile?
Pole sana. Ungeuliza humu JF kabla hujafika Dom. UDOM ni kubwa mno. Na kila college ina theatre zake tofauti.Mimi ni mhanga,umeongea ya ukweli Kabisa yani..
Ile asubuhi tuu kupata venue nimetumia 20k Kwa ajili ya boda tuu yani.
Dodoma was not ready for us.
Wao ni taasisi ya Serikali wanaopewa ruzuku ya kujiendesha, sio profit oriented organization. Wanapowatesa ”wateja" wao kwa nia ya kubana matumizi sio sawa.Kuokoa gharama zaidi, hata wasimamizi waliomba msaada UDOM na ile ya chuo cha Mipango waliwaomba huko Mipango!!
Written ingekuwa Dar tuu maana usafiri na shida zingine tungeokoa wadogo zetu