Utunzaji wa nywele za asili

Nadhani Ni vizuri zaidi kuanzia juu kuchambua zilizoshikana uelekee chini.
Baada ya hapo ndo uanze chini kuelekea juu..kuanzia chini kwenda juu moja kwa moja naona inakata nywele zaidi...
 
nami labda nikushuhudie kitu nilichogundua katika dawa ya mega, dawa ya mega ukiianza nywere inakua nzuri sana na inajaa ila ukiiweka kama ma4 na kuendelea nywele zinakatika hasa ukitoka kuosha ukichana unaona kabisa nywere zinaishia kwenye kitana.. mi kwa sasa nimeachana nayo imenifanya ninyoe nirudi katika nywere za asili naweka.
 
Suka style za twende kilioni mara nyingi nywele itaota tu,make sure u steam n moisturize frequently
Usiweke dawa,nyepesi manake rahisi kuchana
Madawa waachie wenye nywele ngumu
Chagua shampoo,steaming, conditioner na mafuta aina moja stick to them,nywele kukatika yawezekana haina mafuta, I know Blue Magic ni mazito yanakaa kwny nywele so hamna breakage
Ama check hawa naturalista's instagram ni wengi sikuiz uone products zao,wengi nywele zao ziko very healthy
 
Nywele zangu nyepesi na kipilipili nisipoweka dawa hazivutii
 
Namna ya kujaza nywele kwa njia za asili

Hilo linawezekana kwa kufanya yafuatayo.

  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
  2. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
  3. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
  4. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
  5. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako.


Chanzo: muungwana
 
ila nywele inakuwa kacha kacha!mie ndo steaming yangu lakini nimeacha!...nywele inakuwa kavu sana sana
 
Ngoja na mimi nikajaribu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…