Utunzaji wa nywele za asili

Utunzaji wa nywele za asili

nyoa bwana we!raha ya mwanaume umkumbatie sogo lake unalimassage hv halina nywele khaa mie siwez!
Hahahahaaa....umenifurahisha...but ntaonekanaje sasa with that deliberate baldness??Church wakinigomea kufunga ndoa bse ya nywele ndefu ndo ntanyoa labda..U made my day kwa kweli.
 
Hahahahaaa....umenifurahisha...but ntaonekanaje sasa with that deliberate baldness??Church wakinigomea kufunga ndoa bse ya nywele ndefu ndo ntanyoa labda..U made my day kwa kweli.


ahahha have a good evening sir
 
Asante kipenzi, Shea butter naitumia sana tu ila sasa inaishia, nambie hii naipata wapi? Nilonayo nililetewa from abroad. Halafu ni original?



Unaweza chukua zote. But kama ni kuhusu kuchana nywele kwasbb ya kipilipili bas chukua leave in conditioner peke ake. unaweza ukachanganyia na product nyingne za shampoo au mafuta.

Pia kwa matokeo mazur ununue na shea butter ya nywele. Ni mafuta mazito kwa ajili ya nywele unapaka kwenye nywele yanasaidia nywele ambazo ni kavu zikae na mafuta mda mrefu.

Ukipaka leave in unachana unakuja unapaka shea butter ndo yanakuwa mafuta yako ya nywele lakini pia hata mwilini yanatumika. Ni mafuta mazur sana
 
Dawa ya kipilipili ni conditioner ...kuna ile deep conditioning unapakaa unavaa kofia ya plastic then after 30mins unaosha..baada ya nywele kukauka kidogo imean ziwe na unyevu kwa mbali paka sasa leave in conditioner yako ambayo hii unakaa NATO tu kama mafuta yaani hata uwe na kipilipili vipi nywele inakua laini ..cha muhimu tu ni consistency yaani kama unafanya kula baada ya wiki basi iwe hivyo sio unafanya Leo afu unarudia tena baada ya mwezi hautapata matokeo mazuri ..product ambazo Mimi huwa kutumia ni aunt Jackie's (conditioners) na cantu(shampoo) ..
 
Asante kipenzi, Shea butter naitumia sana tu ila sasa inaishia, nambie hii naipata wapi? Nilonayo nililetewa from abroad. Halafu ni original?
Kama upo dar. Mwenge stand utapata hyo shea butter
 
Themommythebest, post: 24202299, member: 333828"]Auntie Jackies ni bei poa ila nzuri sanaaaa... Tena ukiwa na seti nzima utapenda. Mii nina dry hair lakini with aunt Jackies zimekuwa laini hadi nazionea raha. Try that maa[/QUOTE]
Zinapatikana wapi, na gharama zake zipoje?Niliwahi ambiwa zinanunuliwa oonline?
 
Themommythebest, post: 24202299, member: 333828"]Auntie Jackies ni bei poa ila nzuri sanaaaa... Tena ukiwa na seti nzima utapenda. Mii nina dry hair lakini with aunt Jackies zimekuwa laini hadi nazionea raha. Try that maa
Zinapatikana wapi, na gharama zake zipoje?Niliwahi ambiwa zinanunuliwa oonline?[/QUOTE]
Mwenge
 
Asante nina nywele nyingi alafu ndefu pia kavu mno Yaani nikinyoosha na blow dryer lazima niumwe kichwa hata nikipass siku 1 tuu hizoo [emoji16] nitajaribu hizo product maana nlichoka nikasema naeka relaxer this December
Plz don't.

Paka avocado oil, na Fanya treatment ya kitunguu maji na alovela utanipa jibu ndani ya nusu saa
 
Mimi nina rules kadhaa nimejiwekea kwa nywele zangu natural na nimeona maendeleo kwa kweli...mwanzo ilikuwa zikirefuka tu nanyoa ili ziwe fupi iwe rahisi kuchana na kustyle...lakini nimejifunza cha kufanya ili nywele ziwe laini, zichanike vizuri na kunyooka

1. Fanya conditioning (tunaitaga steaming)
Nywele zinafubaa kwa kukosa matunzo jamani. Fanya deep conditioning kila wiki mara 1 na kila unapotaka kusuka fanya deep conditioning kabla. Deep conditioner zinauzwa madukani au unaweza kufanya ya asili kwa kutumia mix ya ndizi, parachichi, asali, yai na mafuta ya nazi.

Conditioner unakaa nayo dk 30 hadi 40 then unaosha.

2. Mafuta hayazipi nywele unyevu bali yanasaidia kuhifadhi unyevu. Kitu kinachofanya nywele zinakuwa ngumu na kupata tabu kuchanika na kunyooka ni kukosa unyevu.

Kosa tunalofanya wengi ni kudhani mafuta yatazipa nywele zetu unyevu. Unyevu unapatikana kwenye maji au kuna bidhaa zinauzwa zenye kutoa unyevu kwa nywele (Moisturizers au leave in conditioners)

Hivyo kama mzururaji juani kama mimi hakikisha kila asubuhi au jioni unanyunyizia nywele yako maji au unapaka moisturizer yako au leave in halafu unapaka mafuta ya chaguo lako kwa juu ili kuhifadhi unyevu. Achana na habari za nywele ukiweka maji zinanuka, ni myth tu labda ziwe chafu. Kama si mzururaji unaweza kufanya hivi kila baada ya siku 2 au 3...

3. Chana nywele kwa kuzigawa kwenye mafungu. Jamani mimi nilikuwa kinara wa kusema "nywele zangu hazichanikiii". Lakini tatizo lilikuwa ni kulazimisha kuzichana tu randomly mara chana imeingia hapa imetokea kule.

Gawa nywele zako hata sehemu zisizopungua 4 kisha kwa kila fungu paka leave in yako na mafuta yako, chana. Ukimaliza suka kisection chako au kibane kisivurugike hamia kwingine.

Maisha mepeeesiiiii

4. Usilale na nywele natural bila kuzisuka mabutu. Hutokufa, utaamka nazo lakini huo mfungano utakaokutana nao asubuhi utazichukia.

Zisuke mabutu nywele zako kabla hujalala hasa kwa wenye ndefu, atleast wenye fupi wanaweza kulala nazo hvohvo. Kisha jifunge kitambaa au vaa kofia.

5. Google jinsi ya kuzistyle nywele zako wewe mwenyewe. Jamani mimi naamini katika theory ya mkono mbaya. Kuna watu wana mikono mibaya kwa nywele, akikushikashika nywele zinadhoofu.

Minimize ishu za saluni, style nywele zako mwenyewe.

Na kuna styles nyingi nzuri sana kwa nywele za asili, Hebu cheki hizi hapa chini

Professional-Natural-Hairstyle-for-4C-Hair-Flat-Twist-Updo-The-Kink-and-I.jpg


mop4.jpg


Front-and-Pony-Puff.jpg


NB:

Nimeona kuna mtu hapo juu anasema ukipaka leave in au products za Aunt Jackies nywele zako zinakuwa kama umeweka dawa; Sijui ana nywele aina gani ila kwa wenye kipilipili kile concord chenyewe naomba nipingane nae, ni nzuri, zinarahisisha uchanaji na nywele zinakuwa laini ila sio kama umeweka dawa; asije fanya watu mkawa na matarajio ya juu sana halafu mkaja kumuita muongo.

Natumia Leave In Conditioner yao inaitwa Quench, Kuna Leave-in detangler ya watoto inaitwa Knot having it(hii nilinunua tu kwa kupenda rangi ila kwakweli haina ulazima), natumia na detangler inaitwa Knot on My Watch na Defining Curl Custard yao ya Curl La La.

Hizi products ni NZURI SANA. Yani nywele unachana vizuri, ukitaka kufanya style zile za kusokota halafu unafumua zinabaki na mawimbi, ukitaka kupaka tu halafu unaacha nywele zinaonekana mawimbi yake ya asili, ni wewe tu na bei zake ni affordable sana 15000 tu.

Kwa mnaopenda kunyoosha nywele bila kutumia blow dryer angalieni video hiyo..



Wasalaam.
 
Back
Top Bottom