Utunzaji wa nywele za asili

mamii umeeleza hadi raha .shukrani sana
 
Wanawake bana!..baadhi yenu nywele huwa zinatoa harufu mbaya sababu huwa hamwoshi vichwa.
 
Asante sana dear, nimekupenda buree! Umeeleza vizuri sana
 
1. Kwanza kabisa unatakiwa kuosha nywele zako vizuri kwa kutumia shampoo ambayo imetengenezwa kwa ajili ya natural hair (nywele asili) au kama utatumia shampoo iliyotengenezwa kwa ajili ya nywele zenye dawa basi jaribu kutumia shampoo yenye conditioner. Hii itasaidia nywele zako kuwa laini na kuzuia zisiwe kavu baada ya kuziosha.

2. Pili ni kupaka mafuta nywele zako, zifanye nywele zako zivutie kwa kuzipaka mafuta ya maji kama vile mafuta ya nazi, olive oil, jojoba oil au castor oil kwasababu mafuta haya hulainisha ngozi ya kichwa, kufanya nywele zikue vizuri na kuzuia mba. Mafuta ya mgando hutengeneza mba kwenye nywele za asili kwa urahisi sana tofauti na nywele zenye dawa.

3. Pia usisahau kuzifanyia steaming nywele zako kwa mwezi hata mara 2, tumia steaming products kwa ajili ya natural hair au fanya steaming ya yai ni nzuri sana kwa kurutubisha nywele za asili. Osha nywele zako na shampoo kisha koroga yai na paka kichwani kwenye ngozi, Vaa kofia ya plastic kwa dakika 45, kisha osha vizuri.

4. Kitu kingine ni kuzichana vizuri nywele zako, nywele za kiafrika ambazo hazijawekwa dawa zina asili ya kujisokota au nyingine ni kipilipili hivyo mara nyingi huwa zinafungana, hivyo wakati wa kuchana inabidi uwe mwangalifu zisikatike, tumia chanuo ambalo ni pana na hakikisha umepaka hair lotion (hair moisturizer / pink lotion) kwenye nywele na mafuta ndio uanze kuchana taratibu. Wakati wa kulala jaribu kusuka mabutu na kuvaa kofia ili nywele zisijifunge au kujisokota.



Chanzo; Hivisasa blog
 
Asante, umenipa jibu la tatizo langu. Nilikuwa najiuliza kwanini ninapata mba sana kumbe ni kwa ajili ya kupaka mafuta ya mgando kwenye ngozi....
 
Shukrani.
Ukirudi tusaidie kujua shampoo na mafuta mazuri kwa nywele za asili. Ukiweka orodha itakuwa safi ili mtu achague. Ungekuwa na muda ungeelezea uzuri na ubaya wa shampoo na mafuta utakayoorodhesha.
 
Kumbe kuna shampoo kwa ajili ya natural hair!!!
Ni kama ipi hiyo? Sijawahi kujua, najua shampoo shampoo tu
 
Hivi Miss Zomboko kakimbilia wapi jamani! Mbona kaanzisha mada halafu haonekani!
 
Pia wakati wakulala inashauriwa, kufunga kitambaa materia ya satin (silk) ili nywele sifungane na pia vinatunza unyevu nyevu.
 
Habarini??
Natumaini mu wazima,

Leo ngoja tujadili kidogo steaming asilia ambayo unaitengeneza mwenyewe na kuboresha afya na muonekano Wa nywele zako

Mahitaji;-

parachichi
yai la kuku Wa kienyeji
Asali (Ukikosa tumia mafuta ya nazi au olive)

Hatua
;-

i/;- chukua parachichi lako likate toa ile nyama ya ndani weka kwenye chombo ili utengeneze mchanganyiko wako

ii/;- chukua yai lako pasua chukua kiini tu cha yai lako changanya na parachichi

iii/;-chukua asali yako pima vijiko viwili au vitatu vikubwa changanya kwenye ule mchanganyiko koroga Hadi vyote vichanganyike vizuri

# Unaweza kutumia blenda kusaga vitu vyote hivi kwa pamoja kupata uji mzito na laini.

Baada ya hapo osha nywele zako pakaa huo mchanganyiko na ukae kwenye steamer muda kadhaa na baadae uzioshe hapo utakuwa umeboresha nywele zako kiasili zaidi ni hayo tu!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…