Utunzaji wa vifaranga

Utunzaji wa vifaranga

neggirl

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2009
Posts
4,849
Reaction score
2,132
Hureeeeeee
Wafugaji wenzangu leo nina furaha sana..katika safari hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji niliyoanza mwezi wa nane mwaka huu.

Leo nimefanikiwa kupata vifaranga 23. Mpango nilionao ni kuwa vifaranga hawa walelewe na mama mmoja (wameanguliwa na mama wa wawili). Huu ni ujuzi niliojifunza katika uzi wa Kubota. Hofu yangu kubwa: je mama mmoja ataweza kuwatunza na kuwapatia joto vifaranga hawa bila nyongeza ya joto la jiko au taa?

pili..kwa ufahamu niliopata kwa kujisomea vifaranga wanahitaji chakula starter, glucose, antibiotic..na baada ya siku 7 chanjo ya new castle ikifatiwa na gumboro baada ya siku 14.

tafadhali wapendwa wafugaji naombeni jibu kwa swali la kwanza..na sehemu ya pili naomba kama kuna jambo lingine naweza kufanya kwa ajili ya uhai wa vifaranga hawa..

Plziiiiiii njooni Chasha Poultry Farm Mama Joe Kubota GAZETI.. atal

Update..

Heri ya mwaka mpya wajasiriamali. Nashukuru Mungu nimeuona.. na hii ndio update ya kuku wangu. Vifaranga wamekua sana mwezi mmoja na wiki kadhaa, nimejifunza mengi.. na kwa sasa nina changa moto ya ugonjwa(Nakazana na matibabu kwa sasa), but sikati tamaa.

Update ..18/2/2015

Shikamoo mdondo ,Shikamoo ufugaji ...
Mapambano yanaendelea... aluta continue hakuna kurudi nyuma.

Hii ni update ya maendeleo ya vifaranga wangu. Kwa kipindi cha January - February, wameugua sana. Na kati ya vifaranga 44 wamekufa 16 hadi sasa. Walikuwa wamekuwa kweli umri wa miezi mitatu. Tatizo kubwa ni mdondo,nina hofu huenda niliuziwa chanjo ilioharibika ama nilharibu mwenyewe kwenye kuandaa. Ingawa chanjo hii niliwapa kwa awamu 2 (wki ya 1 na ya 3)na wakati wa kuugua nimewapa dawa kulingana na ushauri wa watalaamu. Vifo vinakatisha tama but hakuna kushindwa.
 
Attachments

  • 1415376095684.jpg
    1415376095684.jpg
    83.2 KB · Views: 584
hongeraaa swali lako naona umeuliza ukiwa umeisha mnyang'anya mmoja vifaranga. Kwa kuangalia, je mama ana umbo la kuwafunika wote bila shida? Kama hapana waongezee joto. Ingawa si mtaalamu sana kwa hawa ila ukiwa nao karibu watapona tu. Karibu mammy
 
Asante sana Mama Joe..nilitizama hilo katika kuchagua yupi awalee.

Nashukuru kwa ushauri wa Mr. Mangi nimerudi kwa uzi wa Kubota na nimepata mengi ikiwemo majibu ya swali langu.. kwa kuwa nilisoma mda mrefu na nilianza kusahau.

Mbarikiwe
 
Last edited by a moderator:
mnyang'anye huyo mama vifaranga,tafuta mabox mawili,moja kubwa la vifaranga kushinda mchana na jingine dogo sana ambalo watakuwa wanalala usiku,ikipita wiki moja hamna haja ya kuwawekea joto,joto lao wenyewe linatosha,kitu cha msingi ni kuwapa chick starter na vitamin,hii itakusaidia kuku wako arudi kweny kutaga haraka
 
Mkuu asante kwa ushauri wako. Ingawa siwezi mnyang'anya huyo mmoja kwasababu sina umeme kwa ajili ya kuwapa joto..na sina nafasi ya kuweka joto kwa kupitia chemli au jiko.
 
hongeraaa swali lako naona umeuliza ukiwa umeisha mnyang'anya mmoja vifaranga. Kwa kuangalia, je mama ana umbo la kuwafunika wote bila shida? Kama hapana waongezee joto. Ingawa si mtaalamu sana kwa hawa ila ukiwa nao karibu watapona tu. Karibu mammy

Mama Joe, mm vfaranga wangu wanakufa balaa naomba msaada wa nn cha kufanya kuepusha vfo... kila nkienda kuwacheki cfarijiki...
 
pole sana ni aina gani? Umewatenga peke yao au? Check floor haitishi unyevu au ubichi? Ila unatakiwa uwape glucose, cotrim, amintotal au broiler booster kwenye maji na chakula kiwe starter tu. Unawalisha nini?
 
Mama Joe naomba unisaidie kujua haya yafuatayo:
1. vifaranga wa kuku wa kienyeji nao huwa wanapatiwa hiyo chick starter?
2. Glucose huwa inatolewa kwa kipimo gani kwa vifaranga? Nikiwa namaanisha kijiko kimoja kwa lita ngapi?
3. Upi ni mpangilio sahihi wa chanjo kwa vifaranga hasa hasa newcastle na coccidiosis? Sehemu zingine wanasema newcastle siku ya 3 halafu coccidiosis siku ya 7 wakati wengine inakuwa ni kinyume chake, yaani coccidiosis siku ya 3 halafu newcastle siku ya 7.

Naomba msaada tafadhali ili na mimi nipate kuelimika zaidi.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Wikolo, sorry naingia usiku, kwakweli kuku wote wanafanana japo kienyeji hustahimili magonjwa kuliko hybrids hivyo kuwalisha chakula bora huwasaidia kuwa na afya njema na kuwajengea kinga zaidi kwa magonjwa. Waweza punguza gharama kwa kuwapa leftovers na majani kwa wingi lakini kwa siku wapate starter kidogo maana ni mlo kamili. Kuhusu glucose hii kwakweli ni kuwaongezea nguvu vikiwa vidogo hata nguvu havina kusogea kwenye maji, mimi huambiwa kijiko cha chakula kimoja au viwili kutegemea na walivyo dhaifu kwa lita kumi za maji. Hapo kwenye chanjo naona umechanganya, Newcastle ni chanjo ambayo hutolewa siku ya tatu hadi ya saba kisha kurudiwa siku ya ishirini na moja. Amrolium ni dawa ya coccidiosis ila hutumika kama chemoprophylaxis yaani kinga kuanzia siku ya saba ikiaminika kuwasaidia kwa dose ndogo kuwajengea kinga wanapokutana na wadudu. Hivyo endapo vifaranga wataumwa coccidiosis kabla ya siku saba au ugonjwa umo ktk kuku wengine basi hupewa dose kabla ya siku saba.
 
Kulingana na nyuzi mbalimbali nilizosoma humu na vijarida..
Siku ya kwanza vifaranga wanapewa glucuse na chanjo ya newcastle ni siku ya saba kurudia siku ya 21, chanjo ya gumboro siku ya 14 kurudia siku ya 28.

duka la mifugo nilikonunua glocuse.. walinielekeza kijiko kikubwa cha chakula kwa maji lita 2. pia walishauri wapewe antibiotic jina nimesahau kwa siku tano.

Bado naendelea kujifunza..
Nikiwatizama vifaranga wangu nahamasika sanaaa
 
Hizi ni baadhi ya picha ya kinachojiri ..credit nying kwa jukwaa la ujasiriamali
 
Attachments

  • 1420281598211.jpg
    1420281598211.jpg
    71.2 KB · Views: 314
  • 1420281651634.jpg
    1420281651634.jpg
    98.1 KB · Views: 314
  • 1420281677160.jpg
    1420281677160.jpg
    111.2 KB · Views: 310
  • 1420281776495.jpg
    1420281776495.jpg
    103.8 KB · Views: 287
Hureeeeeee
Wafugaji wenzangu leo nina furaha sana..katika safari hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji niliyoanza mwezi wa nane mwaka huu.

Leo nimefanikiwa kupata vifaranga 23. Mpango nilionao ni kuwa vifaranga hawa walelewe na mama mmoja (wameanguliwa na mama wa wawili). Huu ni ujuzi niliojifunza katika uzi wa Kubota. Hofu yangu kubwa: je mama mmoja ataweza kuwatunza na kuwapatia joto vifaranga hawa bila nyongeza ya joto la jiko au taa?

pili..kwa ufahamu niliopata kwa kujisomea vifaranga wanahitaji chakula starter, glucose, antibiotic..na baada ya siku 7 chanjo ya new castle ikifatiwa na gumboro baada ya siku 14.

tafadhali wapendwa wafugaji naombeni jibu kwa swali la kwanza..na sehemu ya pili naomba kama kuna jambo lingine naweza kufanya kwa ajili ya uhai wa vifaranga hawa..

Plziiiiiii njooni Chasha Poultry Farm Mama Joe Kubota GAZETI.. atal

Update..

Heri ya mwaka mpya wajasiriamali. Nashukuru Mungu nimeuona.. na hii ndio update ya kuku wangu. Vifaranga wamekua sana mwezi mmoja na wiki kadhaa, nimejifunza mengi.. na kwa sasa nina changa moto ya ugonjwa(Nakazana na matibabu kwa sasa), but sikati tamaa.

Nimependa sana kuona UZI wa KUBOTA aliouandaa kwa muda mrefu kidogo ukitendewa haki kwa vitendo, kwakweli MUNGU AMBARIKI aendelee na moyo wa kutusaidia vijana.
 
Last edited by a moderator:
Hureeeeeee
Wafugaji wenzangu leo nina furaha sana..katika safari hii ya ufugaji wa kuku wa kienyeji niliyoanza mwezi wa nane mwaka huu.

Leo nimefanikiwa kupata vifaranga 23. Mpango nilionao ni kuwa vifaranga hawa walelewe na mama mmoja (wameanguliwa na mama wa wawili). Huu ni ujuzi niliojifunza katika uzi wa Kubota. Hofu yangu kubwa: je mama mmoja ataweza kuwatunza na kuwapatia joto vifaranga hawa bila nyongeza ya joto la jiko au taa?

pili..kwa ufahamu niliopata kwa kujisomea vifaranga wanahitaji chakula starter, glucose, antibiotic..na baada ya siku 7 chanjo ya new castle ikifatiwa na gumboro baada ya siku 14.

tafadhali wapendwa wafugaji naombeni jibu kwa swali la kwanza..na sehemu ya pili naomba kama kuna jambo lingine naweza kufanya kwa ajili ya uhai wa vifaranga hawa..

Plziiiiiii njooni Chasha Poultry Farm Mama Joe Kubota GAZETI.. atal

Update..

Heri ya mwaka mpya wajasiriamali. Nashukuru Mungu nimeuona.. na hii ndio update ya kuku wangu. Vifaranga wamekua sana mwezi mmoja na wiki kadhaa, nimejifunza mengi.. na kwa sasa nina changa moto ya ugonjwa(Nakazana na matibabu kwa sasa), but sikati tamaa.
Hongera kiongozi, ila napenda kukushauri kitu kimoja kama una umeme tengeneza kibanda ambacho hakiingizi baridi uwe unavitunzia huko na hao mama zao rudisha kwa jogoo waendelee kutaga. Kwanza ni economical kwa sababu ukimruhusu kuku awalee hao vifaranga atakuwa anamwaga chakula hovyo hovyo. Ila kama ni vifaranga peke yao vinakuwa na displine.
 
Hongera mkuu mtoa mada. kazi ya mikono yako Mungu ataibariki!
 
Hongera kiongozi, ila napenda kukushauri kitu kimoja kama una umeme tengeneza kibanda ambacho hakiingizi baridi uwe unavitunzia huko na hao mama zao rudisha kwa jogoo waendelee kutaga. Kwanza ni economical kwa sababu ukimruhusu kuku awalee hao vifaranga atakuwa anamwaga chakula hovyo hovyo. Ila kama ni vifaranga peke yao vinakuwa na displine.
mkuu asante sana kwa ushauri wako, nitaufanyia kazi. Pamoja
 
Back
Top Bottom