BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Maeneo ya Kinzudi
Walianza kwenye viwanja vilivyo mabondeni, makazi ya watu na sasa wanamwaga kwenye mito iliyochimbika baada ya mvua kukatika.
Adha, hii ilianzia Salasala, Kinzudi na sasa wamehamia Mivumoni na Marobo mitaa ya Tegeta kwenye mabonde na mito midogomidogo.
Matokeo yake ni harufu mbaya sana pamoja na Wadudu na kushamiri kwa vimelea vya magonjwa, madhara yake ni mabaya sana kwa sasa na baadae.
Kwa sasa Mivumoni kwenye korongo la kuelekea Marobo hakufai kwa harufu, wadudu pamoja na uharibifu mkubwa sana wa mazingira yanayozunguka makazi ya watu.
Hawa jamaa hawasikii la kuambiwa ikionekana kushirikiana na serikali za mitaa husika hasa ya Mivumoni.
Maeneo ya Kinzudi