SI KWELI Uturuki haitaruhusu Iran igawanywe, tutachukua hatua kali kama tulivyofanya Syria

SI KWELI Uturuki haitaruhusu Iran igawanywe, tutachukua hatua kali kama tulivyofanya Syria

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kumekuwepo na chapisho linalosambaa kwenye mitandao ya kijamii, hususan Facebook, likidai kuwa Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan, ametoa kauli kali kuhusu Iran.

Chapishi hilo limechapishwa katika ukurasa wa Athumani Seiph Amri ambapo Erdoğan anadaiwa kusema kuwa Uturuki haitaruhusu Iran kugawanywa, na kwamba itachukua hatua za kijeshi kama ilivyofanya nchini Syria endapo kutakuwa na jaribio lolote la kuivuruga au kuigawa Iran, ikiwemo kupitia makundi ya Wakurdi au njia nyingine.

Chapisho hilo linaeleza zaidi kuwa Erdoğan alitoa onyo kwa Marekani na Israel, akisisitiza kuwa yeyote atakayejaribu kugawa Iran au kuingilia uhuru wake atakabiliwa na majibu makali kutoka kwa Uturuki.
Uturuji.jpg
 
Tunachokijua

Uhalisia wa madai hayo

Baada ya kufanya uchunguzi kwa kutumia mbinu za utafutaji wa maneno muhimu (keyword search), hakuna ushahidi wowote kutoka vyanzo rasmi kuthibitisha kauli hiyo.

Vyombo vikubwa vya habari vya Uturuki kama Anadolu Agency, TRT News, Hürriyet, na Cumhuriyet havijaripoti tamko lolote rasmi linaloonyesha kuwa Erdoğan ametishia kuchukua hatua za kijeshi kuhusiana na kugawanywa kwa Iran au kuingilia moja kwa moja vita vinavyoendelea.

Kando na hilo ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo imepotoshwa kutokana na kile ambacho kinaendelea mashariki ya kati

Kwa upande mwingine, ripoti za kimataifa zinaonyesha kuwa mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati umeongezeka. Kwa mujibu wa Reuters, kombora la balistiki lililorushwa kutoka Iran liliingia katika anga ya Uturuki tarehe 30 Machi, ingawa hakukuwa na uthibitisho kuwa lililenga Uturuki moja kwa moja.

Aidha, tangu kuanza kwa mvutano huo, msimamo rasmi wa Uturuki umekuwa ni kujiepusha na kuingia moja kwa moja vitani. Erdoğan alinukuliwa na Anadolu Agency akisema kuwa nchi yake inachukua tahadhari kubwa na inaendelea kuhimiza suluhisho la kidiplomasia ili kupunguza mgogoro katika eneo la Mashariki ya Kati.
Back
Top Bottom