Uturuki ilivyozuia mpango wa siri wa Mossad na CIA kupindua serikali ya Iran

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
24,661
Reaction score
40,890
Gazeti la New York Times imeripoti mpango uliokuwa umesukwa na Mossad kwa ushirikiano wa karibu na CIA wa kutumia vikundi vya waasi wa kikurdi huko Iran na Iraq ili kushambulia na kupindua serikali ya Iran.

Mipango hii pia ilihusisha kumtumia Rais mstaafu wa Iran Mohammed Ahmedinejad kama kiongozi wa kisiasa wa mapinduzi hayo ya kijeshi kama yangefanikiwa.

Taarifa inaeleza vikao vilifanyika kati ya Rais Ahmedinejad na viongozi wakuu wa Mossad kwenye maeneo tofauti tofauti duniani kwa mwavuli wa "makongamano ya mazingira".

Mpango huu ulibuniwa kama Plan B baada ya maandamano yaliyoandaliwa na Mossad kufeli mapema mwaka huu baada ya silaha alizotoa Rais Trump kushindwa kuwafikia waandamanaji waliokua wameandaliwa kwa mapinduzi.

Hivyo basi, Mossad na CIA zikaamua kutafuta "magaidi" wa jamii ya kurdi ikiwemo Kurdistan Free Life Party (PJAK), Kurdistan Freedom Party (PAK) na Komala. Vikundi hivi vilipatiwa pesa na silaha na intelijensia yote waliyotaka. Vyote hivi vilipangwa kushambulia kutokea upande wa Iraq.

702750.jpeg

​
Hata hivyo mpango huu ulifeli kabla hujaanza baada ya Uturuki kupitia Rais Erdogan kutoa msimamo kwamba wataingia vitani upande wa Iran kwa kutoa ndege-vita na makombora mazito kupambana na uvamizi huo wa wakurdi.

Ikumbukwe wakurdi ni tishio kwa serikali ya uturuki kwani wana mpango wa kuunda taifa huru inayohusisha baadhi ya ardhi ya uturuki na wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya uturuki kwa miaka mingi sasa. Hivyo Uturuki haipo tayari kuona Iran inadondokea mikononi mwa adui zake wakubwa wa ndani.

Kwa hofu ya kwamba Uturuki ina jeshi kubwa na imara hivyo kuingia kwake vitani kungetishia uwepo wa Israel ikabidi Trump amuombe Erdogan asiingie vitani kwa ahadi ya kutovamia tena Iran kwa wanajeshi wa kikurdi.

Source: The New York Times

Note: Tulisema Israel na US ndio wafadhili wakubwa wa ugaidi leo imekua wazi. Hata maandamano waliyodai ni ya raia yalikua yameanzishwa na CIA-Mossad na sio raia.

Cc Proved MALCOM LUMUMBA 100 others
 
Iran mjinga sana ,badala ya uwaze kujenga nchi unawaza jinsi gani ya kutengeneza makundi ya kigaidi ya kuisumbua Israel.

Ila safari hii katepeta hasa,maana kapigwa kianzia gaza hadi lebanoni,bado tu wale wavaa vipedo wa Yemen
 
Huu ndio unafiki tunaopinga, hii mada tu inaeleza jinsi Israel na US zilivyofadhili vikundi vya kigaidi vya kikurdi. Kumbuka PKK iko listed kama kikundi cha kigaidi na CIA so kuwasaidia affiliated groups za wakurdi ili kupindua Iran ni automatically kufadhili ugaidi.

Je kwanini hampingi Israel kufadhili magaidi mashariki ya kati?
 
Ila safari hii katepeta hasa,maana kapigwa kianzia gaza hadi lebanoni,bado tu wale wavaa vipedo wa Yemen
Hata Israel inafadhili unaowaita magaidi au hujui Rais wa sasa wa Syria ambaye alikua kiongozi wa Al Qaeda alipewa msaada wa kivita na US-Israel ili kupindua nchi. Ila kwa sababu kasaidiwa na israel ni halali ila ingekua Iran imemsaidia mtu wa Al Qaeda ingeitwa baba wa ugaidi duniani.

Wewe unawaita wavaa vipedo ila hao hao ndio hutumika na Israel kama "washirika".
 
Wakurdi Kwa ujumla wao Mimi wala siwalaumu, wao wanatafuta namna ya Ku survive...Wakurdi ndio jamii ambayo inaishi in survival mode muda wote na miaka yote Hadi sasa. US hafai kabisa.
Wakurdi kiukweli wanastahili taifa lao ila sasa hii ya kutumika na nchi zenye mabifu yao ndio itawachelewesha.

Kurdi waliwahi pewa silaha za US kupambana na ISIS huko Syria na Iraq ila baada ya kushinda wakasalitiwa na hao hao marekani walipoondoa msaada wao na wakaachwa watandikwe na majeshi ya Assad.
 
Wanawatumia then wanawaacha, inakuwa ni cycle ya kutumika Tu.
 
Wakurdi kiukweli wanastahili taifa lao ila sasa hii ya kutumika na nchi zenye mabifu yao ndio itawachelewesha.

Kurdi waliwahi pewa silaha za US kupambana na ISIS huko Syria na Iraq ila baada ya kushinda wakasalitiwa na hao hao marekani walipoondoa msaada wao na wakaachwa watandikwe na majeshi ya Assad.
Wakurd wapo Irak, Syria, Uturuki taifa lao litakuwa wapi?
 
Iran mjinga sana ,badala ya uwaze kujenga nchi unawaza jinsi gani ya kutengeneza makundi ya kigaidi ya kuisumbua Israel.

Ila safari hii katepeta hasa,maana kapigwa kianzia gaza hadi lebanoni,bado tu wale wavaa vipedo wa Yemen
Umeielewq hoja Iliyopo mezani !?
 
Gazeti la New York Times imeripoti mpango uliokuwa umesukwa na Mossad kwa ushirikiano wa karibu na CIA wa kutumia vikundi vya waasi wa kikurdi huko Iran na Iraq ili kushambulia na kupindua serikali ya Iran.

Mipango hii pia ilihusisha kumtumia Rais mstaafu wa Iran Mohammed Ahmedinejad kama kiongozi wa kisiasa wa mapinduzi hayo ya kijeshi kama yangefanikiwa.

Taarifa inaeleza vikao vilifanyika kati ya Rais Ahmedinejad na viongozi wakuu wa Mossad kwenye maeneo tofauti tofauti duniani kwa mwavuli wa "makongamano ya mazingira".

Mpango huu ulibuniwa kama Plan B baada ya maandamano yaliyoandaliwa na Mossad kufeli mapema mwaka huu baada ya silaha alizotoa Rais Trump kushindwa kuwafikia waandamanaji waliokua wameandaliwa kwa mapinduzi.

Hivyo basi, Mossad na CIA zikaamua kutafuta "magaidi" wa jamii ya kurdi ikiwemo Kurdistan Free Life Party (PJAK), Kurdistan Freedom Party (PAK) na Komala. Vikundi hivi vilipatiwa pesa na silaha na intelijensia yote waliyotaka. Vyote hivi vilipangwa kushambulia kutokea upande wa Iraq.

Hata hivyo mpango huu ulifeli kabla hujaanza baada ya Uturuki kupitia Rais Erdogan kutoa msimamo kwamba wataingia vitani upande wa Iran kwa kutoa ndege-vita na makombora mazito kupambana na uvamizi huo wa wakurdi.

Ikumbukwe wakurdi ni tishio kwa serikali ya uturuki kwani wana mpango wa kuunda taifa huru inayohusisha baadhi ya ardhi ya uturuki na wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kigaidi ndani ya uturuki kwa miaka mingi sasa. Hivyo Uturuki haipo tayari kuona Iran inadondokea mikononi mwa adui zake wakubwa wa ndani.

Kwa hofu ya kwamba Uturuki ina jeshi kubwa na imara hivyo kuingia kwake vitani kungetishia uwepo wa Israel ikabidi Trump amuombe Erdogan asiingie vitani kwa ahadi ya kutovamia tena Iran kwa wanajeshi wa kikurdi.

Source: The New York Times

Note: Tulisema Israel na US ndio wafadhili wakubwa wa ugaidi leo imekua wazi. Hata maandamano waliyodai ni ya raia yalikua yameanzishwa na CIA-Mossad na sio raia.

Cc Proved MALCOM LUMUMBA 100 others
Hii ya Ahmedinajad kuhusika wanadai ni conspiracy mkuu
 
Back
Top Bottom