Uturuki: Kundi la kigaidi La PKK limetangazwa kuvunjwa na kuweka silaha chini

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Kundi la kigaidi la PKK, ambalo limehusika na mapigano ya zaidi ya miongo minne na kuwaua zaidi ya watu 40,000, limetangaza kuwa limevunjwa na kuweka silaha chini

Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) kimetangaza Mei 12 kufutwa kwake na kumalizika kwa zaidi ya miongo minne ya mapambano ya silaha dhidi ya serikali ya Uturuki hiyo ni kwa mjibu wa shirika la habari la ANF linalounga mkono Kurd

"Kongamano la 12 la PKK limeamua kuvunja muundo wa shirika la PKK na kukomesha njia yake ya mapambano ya silaha," kundi hilo limetangaza katika taarifa yake baada ya kufanya kongamono lake wiki jana

Tangazo la PKK la kujivunja linatii wito wa mwanzilishi wake Abdullah Ocalan, ambaye amefungwa kwenye kisiwa karibu na Istanbul tangu 1999

Katika taarifa amewataka wapiganaji wake mnamo Februari kupokonya na kusitisha mapigano

Katika barua, Ocalan ameitaka PKK kufanya kongamano ili kurasimisha uamuzi huo.

Siku chache baadaye, uongozi wa PKK umekubali wito wa Ocalan, na kutangaza kusitisha mapigano.

Katika hotuba yake mnamo Mei 10, Rais Recep Tayyip Erdogan amedokeza kuwa habari juu ya kuvunjwa zinaweza kuja wakati wowote, akiongeza kuwa serikali yake imedhamiria "kuokoa nchi kutoka kwa janga la ugaidi".

PKK, ambayo inatambulka kama kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, imekuwa ikifanya uasi tangu 1984.

Lengo lake la asili lilikuwa kuchonga nchi kwa Wakurdi, ambao ni karibu asilimia 20 ya watu milioni 85 wa Uturuki.
 
Labda wakifanya wote hivyo tutaanza kuskliza mahubiri ya dini yao, vinginevyo tunawaona wote magaidi, mimi kwangu hata ndugu ukishajiunga hiyo dini kuanzia hapo nakuona gaidi la kufa tu.
 
Kundi la kigaidi la PKK, ambalo limehusika na mapigano ya zaidi ya miongo minne na kuwaua zaidi ya watu 40,000, limetangaza kuwa limevunjwa na kuweka silaha chini

Chama cha Wafanyakazi wa Kurdistan (PKK) kimetangaza Mei 12 kufutwa kwake na kumalizika kwa zaidi ya miongo minne ya mapambano ya silaha dhidi ya serikali ya Uturuki hiyo ni kwa mjibu wa shirika la habari la ANF linalounga mkono Kurd

"Kongamano la 12 la PKK limeamua kuvunja muundo wa shirika la PKK na kukomesha njia yake ya mapambano ya silaha," kundi hilo limetangaza katika taarifa yake baada ya kufanya kongamono lake wiki jana

Tangazo la PKK la kujivunja linatii wito wa mwanzilishi wake Abdullah Ocalan, ambaye amefungwa kwenye kisiwa karibu na Istanbul tangu 1999

Katika taarifa amewataka wapiganaji wake mnamo Februari kupokonya na kusitisha mapigano

Katika barua, Ocalan ameitaka PKK kufanya kongamano ili kurasimisha uamuzi huo.

Siku chache baadaye, uongozi wa PKK umekubali wito wa Ocalan, na kutangaza kusitisha mapigano.

Katika hotuba yake mnamo Mei 10, Rais Recep Tayyip Erdogan amedokeza kuwa habari juu ya kuvunjwa zinaweza kuja wakati wowote, akiongeza kuwa serikali yake imedhamiria "kuokoa nchi kutoka kwa janga la ugaidi".

PKK, ambayo inatambulka kama kundi la kigaidi na Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, imekuwa ikifanya uasi tangu 1984.

Lengo lake la asili lilikuwa kuchonga nchi kwa Wakurdi, ambao ni karibu asilimia 20 ya watu milioni 85 wa Uturuki.
Abdallah Ocalan alikamatiwa Nairobi Kenya kama Colonel Besigye tu. Kenya siyo nzuri kujificha kwa mtu yeyote ambaye ni adui wa nchi yake
 
Back
Top Bottom