Mbona unasubiri majibu yao? Ndio uone nini? Ndio uone tukiangamizwa? Ndio uone tukipigwa risasi? Halafu utahisi vipi? Utafurahi ukiona tukipigwa marisasi? Mkuu usilete ligi kwa haya mambo. Sio mambo yote ya kuleta ligi. Nakuomba tu.
Halafu sijui mbona unasupport magaidi. Kila mtu anastahili kuchukia magaidi maana gaidi hana upendo au loyalty na mtu yeyote. Gaidi akipewa amri auwe mama yake basi atafanya hivyo. Akipewa amri aje afanye mashambulizi Tanzania basi atafanya hivyo. Kwa hivyo Gaidi sio rafiki yako na atakugeuka siku moja.