Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
UUME WAKO SIO RAFIKI YAKO. NI ADUI MPAKA UJIFUNZE KUUDHIBITI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
* Uliwahi kujiuliza Kwa Nini siku hizi huwezi kujisimamia? Huwezi kujiamrisha?
Maisha yanahitaji Malengo, malengo huhitaji Mipango na mikakati, Mikakati huhitaji Focus, nidhamu. Nidhamu tunazungumzia Uadilifu na maadili.
* Kabla hujaanza mambo ya kukimbizana na sketi, kuwaza papuchi ulikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufanikiwa kwenye Maisha na mipango yako Kwa asilimia 80%.
Hii inamaanisha ukiweza kudhibiti uume wako unauhakika WA asilimia 80% kutoboa.
* Kuna msemo maarufu unaosema, "Mwanaume anaanguka pale anapokosa maarifa, si pale anapokosa nguvu." Katika maisha ya mwanaume, hakuna kitu kinachoweza kumuangusha haraka kama kushindwa kudhibiti tamaa, na chanzo kikuu cha tamaa hiyo ni uume wake mwenyewe.
Kwa wengi, uume huonekana kama chombo cha fahari, silaha ya ushindi wa kiume, au tiketi ya kupendwa. Lakini ukweli mchungu ni kwamba, uume wako si rafiki yako hadi pale utakapoijua na kuidhibiti nguvu yake.
* Vijana wengi hushindwa kunielewa Kwa nini Robert anapenda kuzungumzia mada za wanawake na mada za Mahusiano.
Ni Kwa sasabu mtego mkuu wa Mwanaume upo Kwa Mwanamke lakini kupitia natural device iitwayo uume wake.
Sio Kila Mwanamke ulale naye.
Kadiri unavyojiingiza kwenye ngono ndivyo unavyopotea kwenye ramani kama Mwanaume aliyefanikiwa.
Mwanaume asiyeweza kuudhibiti uume wake posibility ya kushindwa kwenye Maisha kwa asilimia 80% hasa kiuchumi.
Na watakaofanikiwa kiuchumi, akishindwa kudhibiti uume wake hawezi kuwa na Furaha katika Familia yake. Hivyo automatic atapoteza Furaha ya Maisha,
* Kila siku kama TaikonMaster nasisitiza. Usitoe pesa kwaajili ya Ngono. Hakuna Faida hata moja.
Utoe pesa kununua magonjwa?
Utoe pesa kupata dhambi?
Utoe pesa Yako kujiunganisha na Mikosi na laana za kiroho na wanawake?
Utoe pesa Yako kuiangusha Familia yako? Mkeo na watoto, Really?
Utoe pesa Yako kujipa stress za kuletewa mimba zisizotarajiwa?
Smartman, alpha Male, watibeli hatupo Hivyo.
Lazima ujue haya kama utashindwa kudhibiti Uume wako;
1. Uume Bila Nidhamu Unakugeuza Mtumwa
Tazama wanaume waliopoteza heshima zao, familia zao, mali zao, hata maisha yao, chanzo kimeanzia kwenye tamaa zisizodhibitiwa. Uume usipodhibitiwa unakuamuru, unakuteka, unakudhalilisha.
Uume usiodhibitiwa utakufanya:
a) Kufukuzwa kazi baada ya kuchukua rushwa ya ngono.
b) Kuambukizwa magonjwa kwa sababu ya uhusiano wa harakaharaka.
c) Kuishi kwa hofu ya mimba za nje na kesi za malezi.
d) Kupoteza mawasiliano na Muumba wako.
Uliwahi kujiuliza why these days your not capable to connect, to concentrate kumwomba Mungu wako kama zamani.
Zinaa ina- disconnect waya wako na falme za rohoni.
Wanaume wachafu(wafanya zinaa) nafsini Huwa watupu.
Kwa sababu dhambi zingine utazifanya nje ya mwili wako lakini zinaa unaifanya kwenye mwili wako na ipo connected Moja Kwa Moja kwenye nafsi Yako.
Elewa, mwili ma nafsi zipo connected, Haya!
2. Utukufu wa Mwanaume Upo Kwenye Kujizuia
Utapoingia Kwenye mafunzo ya kijeshi, kijasusi, warrior, mafunzo ya uanaume( nguvu,utawala) Moja ya mafunzo utafunzwa kujizuia, kujidhibiti.
Kujizuia kihisia, kimwili, kiroho na kiakili.
Ngono ipo kwenye mwili na hisia za mwili. Ngono itakupa Raha lakini sio Furaha. Nilishafafanua tofauti ya Maneno hayo. Kama hukusoma tafuta hiyo Mada.
Ngono si adui kama utafanya kwa uadilifu. Tamaa si dhambi kama utaidhibiti. Bali kuishi kama mtumwa wa uume wako ni laana. Mwanaume anayejua kusema hapana, hata anapowashwa, ugwadu unapompanda, ni mwanaume wa heshima, wa nidhamu na wa mafanikio.
Elewa Wanaume huongoza na kiutawala uume wao. Wavulana huongozwa na uume wao.
3. Dhibiti Uume Wako kwa Akili na Maadili
Njia ya kujenga maisha bora ni kuamua kuwa na nidhamu binafsi:
a) Epuka starehe za haraka zinazokupeleka kwenye uharibifu.
b) Jifunze kuthamini ndoa au mahusiano yenye heshima.
c) Fanya maamuzi kwa akili, si kwa kusukumwa na tamaa ya mwili.
4. Tumia Nguvu Zako Kwa Maendeleo
Kisaikolojia, unakuwa kile ambacho unapeleka au kutumia nguvu na muda mwingi kukifanya. Unakuwa kile unachokipa attention.
Kifalsafa, Yesu alisema ajionavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo.
Ukijiona huwezi kujizuia ni kwamba huwezi kujizuia. Ukijiona unaweza, ni wazi unaweza.
So, kumbe ni suala la mind setting.
Nguvu ya kiume si kwa kuharibu bali kwa kujenga. Badala ya kutumia nguvu yako kutafuta kila sketi inayopita:
a) Jenga biashara.
b) Soma vitabu.
Soma makala za kina TaikonMaster ninakuhakikishia Makala kama zangu zimekapimwa, zikatolewa hesabu ambayo kila mtu atapata Faida. Kulingana na mazingira yake, umri, hadhi, wakati na akili yake.
c) Fanya kazi zenye tija.
Haya umeshafanya kazi za kipato, umerudi home labda huna chakufanya, usiwe mjinga kuanza kuwaza mangono ngono. Fanya kazi Kwa jamii hata kama hazikupi pesa lakini zitakupa jina, heshima na legacy. Ihudumie jamii Yako.
Tumia utaalamu wako kuihudumia jamii Kwa namna ya entertainment kama unapenda entertainment, Dini kama mtu WA dini, michezo kama mtu WA michezo.
d) Jenga familia yenye furaha.
My friend, hakuna kitu kizuri kama kuwa na Familia kwenye hii Dunia.
Kosa vyote usikose Familia.
Lakini vitu vizuri vyote vinahitaji kujengwa, kupiganiwa Kwa jasho na Damu, Sacrifice.
Kujenga Family it's your full time Job.
Huwezi kujenga Familia yenye furaha Kwa kuwaza mangono ngono kama mwanaume usiyeelewa maana ya Ufalme, Mfalme na kutawala.
Familia inajengwa na Heshima, Upendo, Haki, Kweli, Akili, Kujitoa(Sacrifice) Kwa maana ya kuna wakati kuna mambo itakupasa uyaache kwa sababu ya mustakabali wa make/mume na watoto wako.
Wewe ni Mwanaume, King, mungu katika level ya familia. Jitahidi kuonyesha uungu wako.
Jitahidi kuwa mtakatifu hasa Kwa watu wako(Familia Yako, wazazi, ndugu jamaa na marafiki na Taifa lako)
Jitahidi kuwa mwenye Haki kama Mungu Baba.
Jitahidi uwe mwenye Upendo.
Jitahidi mwenye Akili kama Baba.
Jitahidi kuonyesha Ukweli Kwa sababu ndio Nuru ya Maisha, ndio Njia ya future.
Hivyo ndivyo wababa na wanàume huwa. Huko ndio kuwa Mfano wa Mungu Baba, mwenye uweza atakayekupa Uwezo,
Mwenye upendo wa agape atakayekupa Upendo.
Mwenye Utakatifu atakayekutakasa.
Mwenye Nguvu na Mamlaka yote atakayekupa kutawala sio tuu Maisha yako Bali hata viumbe aliokuzawadia kama Mke, watoto na watumishi na watu wako.
Mambo haya huzaliwi nayo.
Elewa, mtu hazaliwi na discipline (nidhamu) Bali hujifunza na ku-practice Kila mara mwishowe Huwa Hivyo.
Elewa mtu hazaliwi na confidence (kujiamini) kujiamini ni matokeo ya kujifunza, kuwa mahiri na uzoefu.
Kufikia hapa TaikonMaster Hana la ziada.
Mungu mwenye nguvu, yule aliyekuumba na Wala SI mwingine, akupe uwezo wa kujitambua thamani yako. Kisha uamue kuchagua kuwa Bora.
Acha nipumzike sasa!
Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam