Uungwana: DC wa Iringa Mjini, Richard Kasesela aomba radhi kutokana na kuteleza kwa ulimi wake

Uungwana: DC wa Iringa Mjini, Richard Kasesela aomba radhi kutokana na kuteleza kwa ulimi wake

Mtumiaji wa madawa ya kulevya huwa anafanya maamuzi ama matendo ya ajabu sana anapokuwa kwenye mzubao wa ulevi (drunken stupour).

Lkn baada ya madawa haya kupungua nguvu mwilini na akili kurejea ktk hali yake ya kawaida hujutia.

Sasa DC Kasesela, kabla hajasamehewa autangazie umma kwamba anatumia kilevi gani?

Inaonesha, alipokuwa akiongea na wananchi alikuwa siyo Richard Kaseslela peke yake, kulikuwa na kitu kingijne cha ziada akilini mwake.

Kumsamehe Richard Kasesela ni dharau kwa wananchi aliowatukana kwamba watulize makalio.

Kiongozi mjifunze unyenyekevu kwa wananchi.
 
Lini aliwahi kutukana tena??
Unamfananisha na Sugu?
 
Mtumiaji wa madawa ya kulevya huwa anafanya maamuzi ama matendo ya ajabu sana anapokuwa kwenye mzubao wa ulevi (drunken stupour).

Lkn baada ya madawa haya kupungua nguvu mwilini na akili kurejea ktk hali yake ya kawaida hujutia....
Umeandika kama vile kila MTU anajua alichofanya huyocDC
 
Macho yake jinsi yalivyo itakuwa anatumia kitu cha Afande Sele
 
Haiihitaji Akili nyingi sana ukirejea Kuangalia ile Video ya Mtukanaji wa Iringa kujua kuwa Jamaa ( Mtukanaji ) yupo Frustrated mno na kwamba kuna Taarifa alishadokezwa ndiyo maana nae kaona amalize hasira zake za mwisho mwisho kwa Raia wa Iringa.

Kuna Watu wakiteleza na Kukuomba Msamaha kweli kwa Rekodi zao unaweza Kuwasamehe, ila kwa Mtu kama Mtukanaji huyu Juha wa Iringa tena akijua ana Mamlaka na Mwakilishi wa Mama na rekodi zake ni mbaya Wilayani hapo hata aombe Msamaha vipi Watanzania hatumsamehi.

Na ningemuona Mtukanaji ana Akili ( ambazo kwa bahati mbaya hana ) baada tu ya Kuomba Msamaha Kinafiki vile mwishoni angetangaza Kujiuzuru kwa manufaa ya Umma na Kukengeuka kinyume na Maadili ya Uongozi lakini lenyewe na Pua lake Kubwa kama Vitumbua vya Mwananyamala limejiona liko sawa tu.

Mama mruhusu basi Gerson Msigwa aweke hadharani hiyo List yako mpya kwani za chini ya Kapeti ( japo naendelea kuzihakiki ) zinasema umekula Vichwa vya Kisarawe, Moshi, Arumeru, Gairo, Iringa kwa hili Tukanaji Juha na Mbeya.
 
Waambie Mods wakusaidie kubadili title, "unavuta” badala yake umeandika "ubavuta," nadhani sababu 'n’ na 'b’ zimekaribiana kwenye keyboard.
 
Huo ndio uungwana na mkumbuke yule mwananchi nae alikua anamtukana
Dc alisema "lazima waandae utaratibu wa bajaji kupanda na kushuka, kwasababu tumebanwa kimataifa...."
Mwananchi akajibu hamjabanwaaa

Katukwana nini hapo?
 
Haiihitaji Akili nyingi sana ukirejea Kuangalia ile Video ya Mtukanaji wa Iringa kujua kuwa Jamaa ( Mtukanaji ) yupo Frustrated mno na kwamba kuna Taarifa alishadokezwa ndiyo maana nae kaona amalize hasira zake za mwisho mwisho kwa Raia wa Iringa...
Unazunguzia AFISA MATUSI mkoa wa Iringa au yupi?
 
Back
Top Bottom