Haiihitaji Akili nyingi sana ukirejea Kuangalia ile Video ya Mtukanaji wa Iringa kujua kuwa Jamaa ( Mtukanaji ) yupo Frustrated mno na kwamba kuna Taarifa alishadokezwa ndiyo maana nae kaona amalize hasira zake za mwisho mwisho kwa Raia wa Iringa.
Kuna Watu wakiteleza na Kukuomba Msamaha kweli kwa Rekodi zao unaweza Kuwasamehe, ila kwa Mtu kama Mtukanaji huyu Juha wa Iringa tena akijua ana Mamlaka na Mwakilishi wa Mama na rekodi zake ni mbaya Wilayani hapo hata aombe Msamaha vipi Watanzania hatumsamehi.
Na ningemuona Mtukanaji ana Akili ( ambazo kwa bahati mbaya hana ) baada tu ya Kuomba Msamaha Kinafiki vile mwishoni angetangaza Kujiuzuru kwa manufaa ya Umma na Kukengeuka kinyume na Maadili ya Uongozi lakini lenyewe na Pua lake Kubwa kama Vitumbua vya Mwananyamala limejiona liko sawa tu.
Mama mruhusu basi Gerson Msigwa aweke hadharani hiyo List yako mpya kwani za chini ya Kapeti ( japo naendelea kuzihakiki ) zinasema umekula Vichwa vya Kisarawe, Moshi, Arumeru, Gairo, Iringa kwa hili Tukanaji Juha na Mbeya.