Uuzaji pombe hovyo sasa ni hatari kwa jamii. Vibanda vingi mtaani/stendi kila sehemu wanauza pombe

Mkuu...inasikitisha sana na cha ajabu in kwamba hakuna mtetezi huko serikalini...kila mtu amekua manafiki wa kutupwa...ni machozi ya Samaki ndani ya Maji kwa wafanya biashara halali.
 
Saiv hizo pombe ndio Habari ya mjini bodaboda, bajaji, wapiga Debe etc wanashutua kila wakati kwa kupimiwa ...viroba Vimerudi kwa staili nyingine? Lengo la viroba kuzuiliwa ilikuwa nini?
 
Kinachokera zaidi hivyo vifremu vinavyouza pombe havina vyoo, wanajisaidia hovyohovyo
 
Sio kila kitu kuiita serikali iingilie kati, kama wanywaji hawawezi kujicontrol basi serikali haitaweza kufanya lolote maana shida inaanzia kwenye akili za wanywaji.
Acha upoyoyo wewe wanywaji wa viroba walivyoshindwa kujicontrol serikali ilifanya nini?
 
Acha kuingilia starehe za watu
Mbn nyie show zenu za bongo fleva hatusiingilii

Ova
 
Hakuna ajira tangu rais jpm aingie madaraka hali ni mbaya ndugu
Wastaafu wengine wameamua kupika gongo hawajalipwa chochote hali ni ngumu sana
 
kwahio wewe unapata uchungu wao kufanya biashara hio au uchungu kua wanafanya pembezoni mwa barabara
 
kwahio wewe unapata uchungu wao kufanya biashara hio au uchungu kua wanafanya pembezoni mwa barabara
Kwa akili kama hizi, acha watawala wazidi kufanya wanachotaka tu, kwani nimeeleza kuwa biashara ya vileo ina sheria zake, ila kwa sasa hazifanyi kazi,kutokana na siasa, unakuja na mipasho!!!
 
Acha unaa,hao wenye vibanda wana vitambulisho vya ujasiri mali,we shida yako nini hata kama kuna pombe ya sh.200?
Watu ndio starehe zao,ungeishauri serekali iboreshe maisha ya mtanzania mmoja na kuongeza fursa za ajira,sonoma ingepungua watu waache kulewa ovyo.
 
Acha upoyoyo wewe wanywaji wa viroba walivyoshindwa kujicontrol serikali ilifanya nini?
Baada ya serikali kucontrol mambo gani yamebadilika? Huwezi kulazimisha mtu afanikiwe kama mwenyewe hataki kufanikiwa. Kila kitu serikali iingilie kati ina maana tuna taifa la wajinga wasioweza kujicontrol wenyewe mpaka msaada wa serikali?
 
Acha watu walewe wasahau shida zao wewe!
Pombe haswa kwa wanawake huwa wanajiachia sana mnapokuwa kitandani hata maswala ya kinga hawajali
Yaani hata kama anasiri zake atakuambia tu ujauzito wa ghafla ndio huwa wanaupatia hapo
 
Maisha magumu watu wanajishikiza popote wanapoona panapatikana
hata mlo mmoja, pigika kwanza ndio utajua kama wako sawa au hawako sawa,
"Aliyeshiba hamjui mwenye njaa"
 
Kwa akili kama hizi, acha watawala wazidi kufanya wanachotaka tu, kwani nimeeleza kuwa biashara ya vileo ina sheria zake, ila kwa sasa hazifanyi kazi,kutokana na siasa, unakuja na mipasho!!!
sio mipasho, wewe kwa moyo huo na roho hio hautafika popote maishani.
wewe unashiba na kusaza na kujamba haumjui mwenye njaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…