Hapo mkuu umenena vizuri!! Ki ukweli wenye bar/grocery nawaonea huruma sana kwani leseni ina masharti kibao, kufungua ndio hiyo jioni, ulipe pango, tra, leseni, halafu kuna mtu ana kibanda tu, hasumbuliwi yeye toka asubuhi hadi asubuhi anauza tu, na wala hasumbuliwi kisa ana kitambulisho cha 20,000 na wengine hawana hata hicho kitambulisho. Kisa mambo ya siasa, mbona zamani haya kuwepo? Ni awami hii tu, sheria hazina umuhimu bali ni matakwa ya kiongozi!! Siku moja nilimsikia trafic mmoja anazungumzia kuhusu hao wafanya biashara wa pembeni mwa barabara akasema kisheria, ni marufuku, ila kwakiwa wameambiwa wawaache hawana jinsi, japo ni hatari sana!!!