Mko poa walimbwende ?
Ngoja niwape darasa kidogo
Kimsingi uvaaji wa nguo fupi kwa wanawake pia ni fasheni ya mjini....nazungumzia gauni fupi,kimini au kikaptula(kichupi)...ila nazungumzia zaidi vimini na magauni mafupi......
1/Mazingira yanaruhusu?
Kabla hujavaa kimini au gauni fupi jiulize kwanza unaenda ofisini,sehemu ya ibada,starehe au kitaani tu au utapanda daladala?.....ukijiridhisha wewe jipigie tu kimini chako !!
2/Una miguu ?
Kuvaa tu kinguo kifupi wakati una miguu mibaya ni sawa na kujidhalilisha tu....km unajijua unatembelea mikono usivae vazi hili !!!
3/Kiatu kirefu ndio mwake
Ili utoke bomba na gauni fupi au kimini hakikisha unavaa kiatu kirefu , lakini kimini pia kinaweza kuvaliwa na flat shoes kikaeleweka....utaonekana wa kijanja !!!
4/Epuka kuinamainama
Ukivaa vazi fupi kamwe usitake kuinama unaweza kujikuta mali zako zinabaki nje.....Njia bora wakati unaokota/kuchukua kitu ni kuchuchumaa tu !!!
5/Kaa kwa staha
Wakati wa kukaa hakikisha unapishanisha miguu badala ya kuachanisha au kuitanua....utakaa uchi !!
6/Uvaaji wa kaptula fupi/kichupi
*huvaliwa chumbani au sehemu ya starehe
*Inapendeza ukivalia top au blauzi
*hakikisha miguu yako ipo soft
Mwanamitindo wa Uswaz
The Bitoz