Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam imetoa wito mzito kwa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, kutofika katika ofisi yoyote ya CCM ndani ya mkoa huo kuchukua fomu ya kuwania tena ubunge kwa mwaka 2025.
Msimamo huo umetolewa siku ya Jumanne na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Nasra Mohamed Ramadhani, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa vijana wa chama hicho hawapo tayari kumuona Gwajima akijitokeza tena kugombea kupitia tiketi ya CCM.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
UVCCM imemtuhumu Gwajima kwa kuwa na msimamo wa kupinga Serikali na chama kwa kujificha, huku akiendelea kunufaika kisiasa kupitia CCM. Wamedai ni wakati wa kila mwanachama kuamua wazi yuko upande upi badala ya kushambulia taasisi kutoka ndani.