Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Hii ndio taarifa yao .naiweka kama ilivyo pasipo kuweka neno langu hata moja wala nukta.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma umelaani vikali matukio yote ya utekaji na uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini, ikiwemo kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mzee Ally Kibao.
Wakizungumza leo 09 Septemba, 2024 Jijini Dodoma Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdulhabib Mwanyemba amesema matukio hayo yanahatarisha Amani na Utulivu na kuutaka Umma kukemea vitendo hivyo bila kuchoka.
"hivi karibuni yametokea matukio ya kikatili yanayoogofya kwa jamii, tunakemea sana, ni jambo la aibu, hatufurahii na hatuwezi kutetea vitu kama hivyo"
Soma Pia: Mwenyekiti UVCCM Taifa apingana na Amos Makalla kuhusu kutoa pole kwa CHADEMA kufuatia kifo cha Ali Kibao
UVCCM wametaka kukamatwa haraka na kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na tukio hilo