UVCCM Dodoma Walaani Vikali Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA, wautaka umma kukemea Vitendo hivyo bila kuchoka

UVCCM Dodoma Walaani Vikali Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA, wautaka umma kukemea Vitendo hivyo bila kuchoka

hamna hata haya hayawani wakubwa nyie mnalia machozi ya mamba kama kawaida yenu msibani mmekaa siti za mbele mkijiliza kwa uchungu wa uongo anyway nanyi pia mtakufa vilevile na kwa kuwa mtakuwa hamjatubu basi kuzimu mtaingia vizuri sana
Mkuu mbona "unageneralize" ?!!

Yaani ikitokea kaka yangu mchawi ,kamweka mtu msukure basi mimi ndugu yake nami ni mchawi na nihukumiwe?!! 😲😲

Mkuu "I feel sad" to what happened.....

#Nchi Kwanza😍
 
Tutawachoma Sindano za sumu~Heri James

Tukiwapoteza Polisi msiwatafute-Kiongozi UVCCM kagera

Tungetuma wataalamu wetu wasingechezea risasi zote zile ~ Samia

Kawaida yeye anapata ukakasi na watoa taarifa.

UVCCM!
 
Lucas Mwashambwa shetani hana rafiki. Hata wewe anaweza kukugeuka.

Kama wewe ni mkubwa nadhani unakumbuka kauli ya mwalimu, maendeleo huletwa na siasa safi na uongozi bora.

Nikisema maendeleo namaanisha maendeleo ya watu. Siyo vitu.
Hatuungi mkono Vitendo vya mauaji.ndio maana Rais wetu mpendwa amelaani na kukemea tukio hilo na kuagiza kufanyika kwa uchunguzi wa kina.
 
Mwenyekiti UVCCM Taifa si amekataaa ..... Au mmeshaona mama yenu amekemea ndio mnakurupuka Sasa ... Kama kawaida yenu.
Chama cha Mapinduzi kupitia Mwenezi wetu Taifa Mheshimiwa CPA Amos Makala ameshatoa salamu za pole na kulaani sana tukio hilo.lakini pia kwa upande wa serikali nako pia Rais wetu mpendwa amelaani sana tukio hilo.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa yao .naiweka kama ilivyo pasipo kuweka neno langu hata moja wala nukta.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma umelaani vikali matukio yote ya utekaji na uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini, ikiwemo kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mzee Ally Kibao.

Wakizungumza leo 09 Septemba, 2024 Jijini Dodoma Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdulhabib Mwanyemba amesema matukio hayo yanahatarisha Amani na Utulivu na kuutaka Umma kukemea vitendo hivyo bila kuchoka.

"hivi karibuni yametokea matukio ya kikatili yanayoogofya kwa jamii, tunakemea sana, ni jambo la aibu, hatufurahii na hatuwezi kutetea vitu kama hivyo"

Soma Pia: Mwenyekiti UVCCM Taifa apingana na Amos Makalla kuhusu kutoa pole kwa CHADEMA kufuatia kifo cha Ali Kibao
UVCCM wametaka kukamatwa haraka na kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na tukio hilo
UVCCM waache utekaji wa viongozi wa upinzani hususan CHADEMA. Inasikitisha sana.
 
Back
Top Bottom