UVCCM Dodoma Walaani Vikali Mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA, wautaka umma kukemea Vitendo hivyo bila kuchoka

Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa yao .naiweka kama ilivyo pasipo kuweka neno langu hata moja wala nukta.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma umelaani vikali matukio yote ya utekaji na uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini, ikiwemo kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mzee Ally Kibao.

Wakizungumza leo 09 Septemba, 2024 Jijini Dodoma Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdulhabib Mwanyemba amesema matukio hayo yanahatarisha Amani na Utulivu na kuutaka Umma kukemea vitendo hivyo bila kuchoka.

"hivi karibuni yametokea matukio ya kikatili yanayoogofya kwa jamii, tunakemea sana, ni jambo la aibu, hatufurahii na hatuwezi kutetea vitu kama hivyo"

Soma Pia: Mwenyekiti UVCCM Taifa apingana na Amos Makalla kuhusu kutoa pole kwa CHADEMA kufuatia kifo cha Ali Kibao
UVCCM wametaka kukamatwa haraka na kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na tukio hilo
Bullshit
 
UVCCM Kanda ya Ziwa waliomba wapewe kazi ya kuwapoteza wapinzani na ninaona wanaifanya vizuri sana.
Katibu Mkuu wetu wa CCM Mheshimiwa Balozi Dkt Emmanueli Nchimbi alishakemea suala hilo hadharani kabisa.
 
Nchimhi ndiye aliyeruhusu viongozi wa CHADEMA akina Mbowe na Lissu wakamatwe Mbeya na ndiye aliyeamuru waachiwe na waliachiwa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa yao .naiweka kama ilivyo pasipo kuweka neno langu hata moja wala nukta.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma umelaani vikali matukio yote ya utekaji na uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini, ikiwemo kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mzee Ally Kibao.

Wakizungumza leo 09 Septemba, 2024 Jijini Dodoma Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdulhabib Mwanyemba amesema matukio hayo yanahatarisha Amani na Utulivu na kuutaka Umma kukemea vitendo hivyo bila kuchoka.

"hivi karibuni yametokea matukio ya kikatili yanayoogofya kwa jamii, tunakemea sana, ni jambo la aibu, hatufurahii na hatuwezi kutetea vitu kama hivyo"

Soma Pia: Mwenyekiti UVCCM Taifa apingana na Amos Makalla kuhusu kutoa pole kwa CHADEMA kufuatia kifo cha Ali Kibao
UVCCM wametaka kukamatwa haraka na kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na tukio hilo
Huo ndio ubinaadam, barkiwa sn kaka.
 
Acha uongo wako hapa wewe
Kwa bahati mbaya sana Polisi Tanzania wanafanya kazi kwa maagizo ya ma-kada wa CCM inahuzunisha mno demokrasia hii iliyopokwa na CCM, ila mwisho wa siku CCM na wote wanaoishabikia wataishia kwenye laana kwa kujenga mfumo kandamizi wa ajili ya kujineemesha ki-binafsi na wewe upo.
 
Kwa hiyo hamtaki kufanyika kwa uchunguzi?
Hata uchunguzi ukifanyika unadhani ikionekana ni serikali au wanacm ndo wahusika kuna la maana litafanyika?

Kwa nini matukio yote hilo tu ajitokeze kukemea na uvcccm? Au mengine sio matukio ya kukemea?

Kwa nini ni wapinzani tu ndo yanawakuta?
 
Najua inaumiza sana .lakini tuache uchunguzi ufanyike na kupewa ripoti kamili kama ilivyoagizwa na Mheshimiwa Rais wetu
Uchunguzi gani unataka ma muuaji ni yuleyule Bashite aliyekuwa anaua akina Ben Saanane wakati wa awamu ya 5
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hii ndio taarifa yao .naiweka kama ilivyo pasipo kuweka neno langu hata moja wala nukta.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Dodoma umelaani vikali matukio yote ya utekaji na uhalifu yanayoendelea kujitokeza nchini, ikiwemo kuuawa kwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mzee Ally Kibao.

Wakizungumza leo 09 Septemba, 2024 Jijini Dodoma Umoja huo kupitia kwa Mwenyekiti wake Abdulhabib Mwanyemba amesema matukio hayo yanahatarisha Amani na Utulivu na kuutaka Umma kukemea vitendo hivyo bila kuchoka.

"hivi karibuni yametokea matukio ya kikatili yanayoogofya kwa jamii, tunakemea sana, ni jambo la aibu, hatufurahii na hatuwezi kutetea vitu kama hivyo"

Soma Pia: Mwenyekiti UVCCM Taifa apingana na Amos Makalla kuhusu kutoa pole kwa CHADEMA kufuatia kifo cha Ali Kibao
UVCCM wametaka kukamatwa haraka na kuchukuliwa hatua kwa wote waliohusika na tukio hilo
Hivi hawa si ndo walise mtu akipitea wao ndio wame fanya na wasiulizwe? Leo wana kuja hapa na lugha tata?
 
Back
Top Bottom