Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 165
- 181
UVCCM Mwanza" watapeli" mamilioni ya pesa, viongozi wagawana
Katika hali ya kusikitisha Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wanadaiwa kutapeli zaidi ya milioni 80.
Tuhuma za UVCCM wilaya ya Nyamagana zinawakabili watu wawili ambao ni viongozi, Mwenyekiti wa UVCCM wilaya, Bonipace Zephania na aliyekuwa Katibu wa UVCCM Nyamagana Maranyingi Matukuta ambaye kwa sasa ni Katibu wa UVCCM mkoani Dodoma.
Inaelezwa kuwa viongozi hao kwa kushirikiana na genge lingine la watu zaidi ya watano walitengeneza kikundi hewa na kisha kukiwasilisha halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuchota fedha hizo.
Kwa mjibu wa chanzo cha habari hizi, inaelezwa kuwa, kikundi kilichoundwa cha vijana awali kilikuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wao Kisali Simba lakini baada ya mchakato kukamilika, Mwenyekiti na Katibu walipeleka akaunti ya uvccm Nyamagana na kuwekewa fedha.
Kikundi hicho kilitengenezwa ili kuiaminisha Serikali (Jiji) na namna nzuri fedha hizo zitakavyotumika na kuweka mfumo mzuri wa kukopesheka kutokana na Umoja wa UVCCM kutokuwa na sifa za kupewa mkopo.
Hata hivyo, kikundi hicho kilikidhi vigezo cha kusikitisha hakikupewa fedha licha ya kunaonekana Jiji ndicho kimekopeshwa mamilioni hayo.
Hatua za kukamilika kwa mchakato na mawazo ya namna ya kutengenezwa kikundi hicho, yalifanyika ofisi za kata ya mirongo, chini ya ushauri wa Mtendaji wa kata hiyo.
Fedha zilizochotwa au kuombwa Jiji la Mwanza, lengo lilikuwa ni kwa ajili ya mradi wa kununua bajaji moja kila kata za Jiji la Mwanza.
Hata hivyo, baada ya fedha kupatikana wazo la kununua bajaji kila kata lilikufa na viongozi hao kuanza mchakato upya na kupanga mradi mwingine.
Fedha hizo baada ya kuwekwa katika akaunti ya uvccm wilaya, wapigaji hao wawili walienda kuzitoa katika benki ya NMB tawi la Mwaroni Kirumba.
Baada ya kutolewa kwa fedha hizo, Mwenyekiti na Katibu wake walienda kununua 'hiace used mbili.
Chanzo hiki, kinadai kuwa, hiace mbili zilizonunuliwa, kila moja ilinununuliwa kwa gharama ya shilingi Milioni 35.
Chanzo kinaeleza kuwa milioni 10 iliyobaki waliigawana watu wawili, mgao ambao ulifanyika eneo la mgahawa wa Malikusema mlango mmoja.
Chanzo kingine ambacho kiliomba kutotajwa jina lake kutoka ofisi ya chama cha mapinduzi, kinaeleza hiace hizo ambazo kwa sasa zinafanya kazi ya kubeba wanafunzi shule ya Nyanza English Medium, Hiace moja ilikuwa ikiuzwa kwa shilingi Milioni 16.
"Brother (kaka) sitaki kuficha kitu na ninachokueleza hapa no ukweli mtu, kama unavyofahamu hivi karibu ulisikia mkuu wa mkoa wa Mwanza anaongelea suala la upigaji wa fedha za makundi maalumu.
"Mkuu alichokuwa anakifanya ni kufunika tu upigaji wa hao vijana wa CCM ambao wao ndio walengwa wakubwa kwa sababu wamekuwa walitengeneza vikundi hewa na kuchota mamilioni ya pesa.
"Tunashangaa mkuu wa mkoa anashindwa kunyooka na kuwataja wakati tayari (Takukuru) Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa, wanaendelea kuwahoji, yeye anashindwa nini kuwa wazi," kilisema chanzo hicho.
Upigaji wa fedha hizo, umewaibua wajumbe na wanachama wa Umoja wa vijana ambao wanalalamikia Umoja wao kutuhumiwa kuchota fedha hizo kitendo ambacho sio cha kweli.
Kwa mjibu wa kikao cha dharura cha uvccm wilaya ya Nyamagana kilichoketi Desemba 24 mwaka 2021 kiliwahoji viongozi hao kuhusu tuhuma hizo.
Baada ya wajumbe hao kuhoji, inadaiwa viongozi hao walidai kuja na majibu sahihi katika vikao vingine vitakavyofatia kwa kuwa hawakuwa na majibu ya maswali waliyotwangwa.
Hata hivyo, mpaka sasa viongozi hao hawajawahi kufanya kikao chochote ili kuwaelezea kuhusu tuhuma hizo na inadaiwa Mwenyekiti amekimbia ofisi.
Kwa upande wake Mwenyekiti huyo wa UVCCM, Boniphace Zephaniah, alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alikiri fedha hizo kutolewa na Jiji la Mwanza.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa, fedha hizo ziliingia katika akaunti ya kikundi ambacho hakukitaja jina na kwamba hazikuingia kwenye akaunti ya vijana.
Zephania anadai kuwa, tuhuma hizo zimejaa chuki za kisiasa zaidi wanaodai kupiga fedha hizo ni wale washindani wake aliowashinda kwenye uchaguzi.
"Mtu anayeeneza hizo taarifa anaenda Takukuru na ofisi za Serikali ni mtu mmoja anaitwa Kisali soud Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wao zamani na sasae alishaondolewa.
"Taarifa wanazotoa hazina ukweli na ambao wanaongea hivyo vitu hawavijui na hawana uhakika, ila ni kweli hizo hiace zilinunuliwa kila moja shilingi milioni 35 na hizo gari tuliziagiza nje," alisema Zephania.
"Hizo gari zipo pale shule ya msingi nyanza, ni gari mpya na hazina shida yoyote ile na kama zingekuwa na shida Serikali ingekuwa wamezikataa... Mpaka viongozi wa CCM walishaenda wakazikaguwa zipo vizuri," alisema Zephania.
Zephania anakiri kuwa fedha zilizoombwa Jiji zilikuwa ni kwa ajili ya kununua bajaji 10, lakini uongozi wa kikundi hicho ulibadilisha mradi na kununua gari hizo baada ya kuona mradi wa awali haulipi.