UVCCM yachangia wheel chairs tano kuunga mkono taasisi ya Mama Ongea na Mwanao

UVCCM yachangia wheel chairs tano kuunga mkono taasisi ya Mama Ongea na Mwanao

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

✳️ UVCCM YACHANGIA WHEEL CHAIR TANO (5) KUWAUNGA MKONO TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO


🗓️07 Aprili, 2024
📌Karimjee, Dar es Salaam.

Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi imechangia Wheel Chair tano kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi ya Mama ongea na Mwanao ya kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Komredi Jokate Urban Mwegelo amewasilsiha Mchango huo kwa niaba ya Jumuiya.

"Ndugu yangu Steve nimetumwa hapa na Mwenyekiti wetu Komredi Mohammed Ali Kawaida na sisi UVCCM tunatambua kazi kubwa mnayyoifanya ya kuyafikia Makundi maalum katika Jamii na kuzitangaza kazi nzuri zinazofanywa na Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan".

"Tumeona kazi nzuri Mama ongea na Mwanao mkiwavisha Viatu wanafunzi kwenye Maeneo Mbalimbali nchini tunawapongeza sana".

"Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka miondombinu mizuri kuhakikisha wanafunzi hawa mnaowavisha viatu wanajiendeleza kielimu".

Mwisho Komredi Jokate ameihakikishia Taasisi ya Mama Ongea na Mwano kuwa UVCCM itaendelea kushirikiana nao na kuwaunga mkono kwenye jitahada zao mbalimbali za kijamii.

"Nikuhakikishie Ndugu yangu Steve Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Chini ya Mwenyekiti wetu Komredi Mohammed Ali Kawaida tutaendelea kuwaunga Mkono kwenye shughuli zenu zote za kijamii kwani ni utamaduni wetu kuunga mkono Mtu au taasisi yoyote inayofanya mambo yanayoigusa Jamii" alisema Jokate".

#KulindaNaKujengaUjamaa
#SisiNaMamaMleziWaWana
#Kaziiendelee

Imetolewa na;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa.

WhatsApp Image 2024-04-08 at 00.07.31.jpeg
 
Wheel chair moja inauzwaje?

Mnatumia mamilion hapo alafu mnatoa kamsaada cha pesa ndg
Wazushi kwelj nyie

Ova
 
Back
Top Bottom