Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Hivi uvcmm bado ni umoja wa vijakazi vya ccm au siku hizi wamebadilishiwa kitengo...??

Tumeona matunda yao kama akina Makonda, Nape, et al... vijakazi waliotayari hata kulamba viatu vya akina kikwete na familia zao...!
Wataalamu wa kupaza sauti na kujipendekeza...!!
 
Lowasa hakuwa na uwezo wa kuchambua ametoa vitu jumlajumla. unapozungumza utendaji wa serikali popote duniani unazungumzia elimu, afya, ulinzi ,mawasiliano na vitu vya namna hiyo. kwa case ya matatizo ya Tanzania Magufuri amegusa maeneo maalum yatakayoshughulikiwa na serikali yake.

Usitake kufukia udhaifu wa lowasa jana aliposhindwa kabisa kutueleza tutarajie nini katika miaka mitano yake. Acha mahaba ya hivyo. Kiongozi mzuri ni yule aaeweza pia kueleza mawazo yake kwa ufasaha kwa wananchi wake. Hiyo itakufanya hata ukiwa mtendaji mzuri ukishindwa kufafanua unachokifanya utazua usumbufu usio wa lazima.

Ntachagua mabadiliko, no matter what Mkuu
 
Nilidhani ni taarifa ya maana kumbe mihemko tu ya vijana.Mlitaka aeleze kuwa atandeleza vipi miradi yenu,kwani hiyo miradi ya wapinzani? Kama ni ufisadi si ccm ndiyo imejaa mafisadi? Lowasa alikatisha hotuba kutokana na mda,hivi angeendelea si mngeita polisi kupiga mabomu? Kama uvccm imejaa watu wasiojielewa kama shaka ninamashaka na uwezo wenu.Lowasa amesema atazungumza zaidi kwenye mikutano mingine,nyinyi mnataka kuwapangia UKAWA cha kuzungumza? Mbona Magufuli anaiponda serikali as if yeye ni mpinzani?Taarifa kama hizi pelekeni kwa watoto wenzenu huko.

Mkuu hotuba aliimalizia usiku kuanzia saa tatu kupitia television . ITV
 
Hawakubaka wale ni mzee wa kaya alipigiea mashine yake akajenga bifu
 
kumbe yanawaingia ccm,mnalalamika nin ninyi?kwan ninyi wapinzan au?mi mtanzania najua haki yangu ya kupiga kura na najua nani nitampa.
 
Kweli uvccm mnakurupushwa na kupelekeshwa kama taka wakati wa mafuriko. Mnasikitisha na kushangaza zana kwa tathmini mliyofanya kuhusu gharika ya jana. Niwaulize swali dogo tu, ni mwalimu gani aliyekufundisheni ku-evaluate jambo zito kama la jana na kulitolea majibu dhaifu kiasi hiki? Au lengo la kikao chenu kilikuwa kupiga sitting allowance kama ilivyo ada?
Na kwanini mnatisha raia kuwa wakifanya mabadiliko yatakuwa kama yale ya Libya ilihali kuna nchi kama Kenya, Malawi, Tunisia na Zambia zimebadili mifumo yao kwa amani tu?
Nina shaka kubwa kama ccm imejiandaa kukabidhi nchi kwa amani bila vurugu kwani mmeanza kujitangaza mapema kwa kuiona Libya tu na nchi nyinginezo kama Nigeria ya juzi.
Lowasa yupo vizuri kwani hahitaji kuwaimbia wananchi ngonjera za kujenga barabara zisizokwisha kila mwaka na kupasha viporo vya mwaka 2005 na 2010 ambavyo mnaviamsha kana kwamba hakuna vipaumbele vingine.
Hivi wewe mwenyekiti wa uvccm na Lowasa ni nani mwenye kuijua hii nchi ndani- nje na mwenye siri nyingi na nzito kati yenu? Alivyovisema jana anavimaanisha na si porojo na vitisho vyenu vya Libya. Jiandaeni kuwa wapinzani safari hii kwani mnachosha kama andiko lako linavyochusha.:blah: :blabla:
 
Mwaka huu ukawa kazi wanayo, Eti wanadhani kuweka mamluki ndo watatushinda Hahahahaha ccm sio chama cha mchezo
 
Uvccm ni wanafunzi wa darasa la ngapi.. mbona wanauongo wa watoto wa chekechea? Hivi hawajui kuwa watu wanaangalia tv na clips zinaweza kurushwa watu waone mgombea kaongea nini.. duh siasa za enzi zile za simu za mezani zimepitwa na wakati..tuliona na tumesikia..la babu seya wananchi ndo waliopaza sauti zao na yeye akasema ataliangalia katika utawala bora..kama watu wengi wanaamini Babu seya yuko jela kwa ajili ya manufaa binafsi ya baba rithiwani hamuoni ni haki ya wananchi kutaka kuujua ukweli..mlitaka awaambie wananchi sitolishughulikia mpate cha kusema...ikiwa itagundulika kwa jicho la tatu kuwa kweli alibaka hamuoni itasaidia kumsafisha baba rithiwani kwa tuhuma hiyo nzito na ya kisasi inayomhusu?kumleta balali kuna tatizo gani watanzania wanataka mtuhumiwa wao awe yuko hai au amekufa ..kama amekufa tutahitaji mabaki yake na juu ya kaburi tufunge pingu..tuache kujitoa ufahamu kwa siasa za 1920
 
shaka.jpg

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA

Tulieni dawa iingie magamba mbona mnaweweseka sn?! tulieni tulieni biziness ndo inaanza...
 
Lowassa ndie aliye muweka mwenyekiti wenu madarakani,na sumaye jana alifunguka,sasa nyie endeleeni kumchafua
 
UVCCM ni genge la kihuni kabisa, kuwahi kutokea Nchini. Hawa ni vijana wanaotumika kama silaha ya Muovu shetani.

Ni mangapi mabaya yanayowatokea wananchi, wao wanakaa kimya? Iweje hili la BABU SEYA liwaume hivi?

LOWASSA akiwa Rais hii kesi ya akina BABU SEYA itapitiwa upya! Kama haki haikutendeka wataachiwa huru!! Kwa hili jiandaeni kisaikolojia!

Mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko, na bahati mbaya sana mabadiliko ya mwaka huu hayazuliki hata mkiiba kura!

CCM lazima iondoke!!!!!
 
Jina UKAWA likitajwa popote hata malaika huko mbinguni wanaimba na kucheza!!
 
CCM tutashinda asubuh

Asubuhi ya OCTOBER 25, ni moja ya asubuhi mbaya zaidi kuwahi kutokea kwa CCM. Ndiyo siku ambayo CCM inaondoka!

Siku hiyo ndiyo siku ambayo watanzania wanaifananisha na Desemba, 9, 1961 siku tuliyopata UHURU kutoka kwa

mkoloni mweupe, sasa mwaka huu tunapata UHURU wa kiuchumi, kisiasa, na kijamii kutoka kwa mkoloni mweusi CCM.

Hakuna namna tena, tumenyanyaswa vya kutosha, tumeonewa vya kutosha, na tumedhalilishwa vya kutosha na hawa wakoloni weusi!

Sote kwa kauli moja tunasema BAAAAAAAAAAAAAAAASI!!!!!!

CCM should step down...!!!
 
Mimi na marafiki zangu wa karibu sana tutapigia kura upinzani na Lowasa sio kwa sababu wana uwezo wa kumaliza kero za Watanzania bali tunataka CCM itambue kuwa TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.
 
Billions of bilious blue blistering barnacles!
 
shaka.jpg

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA
Mjingaa aliandika mada ndefuuuu Maninnner salsa sema tena boya
 
Back
Top Bottom