Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Kwa niliyoyasikia jana Jangwani....
Nawashauri SISIEM mkae kimya mana ni mtahaibika
 
Swadaktamaneno yako mkuu
Full hofu na mashaka,poleni UVCCM maana naona mmetingwa kwelikweli.Mnashindwa kutoa matamko dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu,uchafu wa jiji la dar,na matatizo kibao ya chama chenu na serikali mnawashwa na mabadiliko ya ukweli!
 
Hivi kati ya Rwanda na Tanzania nani wakumsaidia mwezake mipango ya kiuchumi ? najuta kuwa mtanzania.
 
Hivi UVCCM wanataka EL akoge nyoyo alikuwa anaimba taarabu; mtiririko na details za hotuba za nini kwani alikuwa anafanya mtihani? Wenye akili walielewa ila siyo rahisi CCM kuelewa kutokana na ukilaza wao
 
Nilidhani ni taarifa ya maana kumbe mihemko tu ya vijana.Mlitaka aeleze kuwa atandeleza vipi miradi yenu,kwani hiyo miradi ya wapinzani? Kama ni ufisadi si ccm ndiyo imejaa mafisadi? Lowasa alikatisha hotuba kutokana na mda,hivi angeendelea si mngeita polisi kupiga mabomu? Kama uvccm imejaa watu wasiojielewa kama shaka ninamashaka na uwezo wenu.Lowasa amesema atazungumza zaidi kwenye mikutano mingine,nyinyi mnataka kuwapangia UKAWA cha kuzungumza? Mbona Magufuli anaiponda serikali as if yeye ni mpinzani?Taarifa kama hizi pelekeni kwa watoto wenzenu huko.
 
UVCCM, hongereni sana, nyie ndio mfano wa kuigwa wa vijana wazalendo mnaojua nchi yenu inatakiwa kuendelea kwa dhati na sio kimaigizo na usanii wa mafisadi wa ukawa
 
Wakakemee kauli ya magufuli kuwa wananchi wakiikataa ccm nchi itaingia vitani kama libya wamuulize kwa nini anaamini haya yatatokea?
eti Libya, kwani Libya kuliwahi kuwa na vyama vingi!?
je, hao akina Lowassa, Dovuttwa, Mchange, Anna Mgwila nk wamejipitisha wenyewe au na tume!?
Na kama wanaweza kutupeleka katika vita ni kwa nini usalama wa taifa hawajawazuia au ccm kuwawekea pingamizi!?
Mimi naona hawa jamaa wanaongezewa promo na kupewa hoja za kujibu!
Kwa vile Ghadafi alitawala nchi peke yake na kutaka kurithiwa na wanawe, sasa mnadhani hapa kuna baadhi ya waliokwisha wachomeka watoto wao na wanadhani mpango wa kuwatibulia kuendeleza ufalme ndio vita!?
Kuendelea kuzinyamazia propaganda za kizamani na woga kama hizi si kitu cha kuchekea.

Hongera sana vijana mnaojitambua.

mnawachimbia shimo vijana wa watu, kama kwawaida yenu mtawafanya kama karai.... mmewanyima tenda ya kutengeneza t-shirts lakini hamuachi kuwatumia. nawaonea huruma vijana wenzangu hawa waliokubali kuwa watumwa kwa wao kutumika
 
Hata Kama Hajasema Neno Lowasa Ni Chaguo La Watanzania. UVCCM poleni sana
 
shaka.jpg

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA

kichinjio kiko tayari mnapoteza muda na nguvu zenu tu. kura ni kwa Lowassa
 
Kwahiyo wamechukia kwakuwa hotuba yake siyo nzuri? Wanahisi Lowassa hajawabeba vizuri UKAWA? Kumbe wanapenda mabadiliko. Hotuba yake iko kwenye tovuti ya CHADEMA, waisome kisha watoe maoni ili akiona yanafaa ayafanyie kazi.

TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalisi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama ili yote Kea c kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.

Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.

Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.

UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.

SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)

KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA
 
Heee!! Hii nchi ina watu wa ajabu sana. Hata sielewi nianzie wapi kuelezea kinachonishangaza!!
 
Njaa tu hizi. Huu ndo ulofa na upumbavu aliokuwa anausema Mkapa
 
Ndio maana walisema"Tunajua walikuwa wanasema tunatengeneza picha wamejibana wanaangalia kinyemela".Kumbe mafuriko yalikuwa hadi Lumumba kwa Magambaz?Kweli sindano imepenetrate...
 
Nadhani huu sio wakati muafaka wa CCM NA UVCCM kukaa na kuanza kumuongelea LOWASA mnampa publicity bila nyie kujijua au ndo lile kundi lililohaidi kumsapot mkiwa ndani ya chama ?
 
Kijana mwenzenu Bashe yeye ana akili nyingi. Changamkeni vijana, nchi inaelekea kwenye mabadiliko makubwa
 
Back
Top Bottom