Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Elections 2015 UVCCM yamvaa LOWASSA, yakerwa na kauli zake za kutetea wabakaji, wamshangaa SUMAYE

Kama alichemsha hotuba si ndio raha kwenu?

Mbona sijui ilani ya ccm wala siihitaji kuijua
 
Kufeli kwa CHADEMA kunawahusu nini UVCCM? Eti wanasema walitarajia Lowassa akonge nyoyo zao......mmmmh hapa nina mashaka na uimara wa UVCCM. Awakonge nyoyo ili iweje? Adui yako mwombee njaa. Jamani tupeni sisi hiyo CCM tuiendeshe mwone tutakavyoifanya chama imara.....
 
Sie ukawa hatutaki maneno mengi yasiyo na faida, we ulitaka naye aanze kukariri lugha za makabila mbalimbali masuala ya ngojera pereka huko. Mtu unachagua vitu viwili au vitatu kama alivyosema vingine vyote vitakuja tu cha msingi ni usimamiz mzur wa uchumi
 




“CCM wanawajaza Watanzania kitu kinaitwa woga wa usilolifahamu au woga wa usilolijua kwa hiyo kila siku wanawaambia Watanzania mkiwapa wapinzani nchi itaingia kwenye vita,” alisema Sumaye.

Jana mgombea wao ameanza kutishia watu , eti msikimbilie mabadiliko angalieni Libya. Atakuwa raisi wa namna gani kama hawezi kutofautisha AK 47 na KICHINJIO. Mh lakini kuchinjwa noma! Kwao, tuwachinje tuuu.
 
Kashindwa. Kashindwa. Kashindwa.

Nyie mmeweza nini cha msingi miaka 50 na ushee?

Zungumzieni yenu. Lowassa sio mwanasiasa wa majukwaani. Yeye ni mtendaji.

Acheni porojo. Kama ni ilani, hotuba ilitangazwa na nakala zimesambazwa.

Ajabu kweli kweli. Miraji kapewa tenda ya T-shirt na vinginevyo, bado mwaishabikia CCM?

Sisi twasema CCM ni Biashara. Ingekuwa chama Lowassa asingehama.

Tunaleta #Mabadiliko2015. Kama mna nguvu ya kuyazuia, yazuieni!
 
Sindano zimegusa mifupa na dawa imefika katika jeraha.
Kumbe mlikua mnafuatilia live hatua kwa hatua? Neno kwa neno?
Ni furaha kuona mpinzani wako anakufuatilia namna hii.

Tena kwa maneno yao wenyewe wanakiri "hadhira ilikuwa kubwa...." Na bado,kutwa kumsema Lowassa wakati Mgombea wao jana alikuwa ananong'ona na MIC Mbeya.Mimi nilishaamua hivyo,hata ingekuwa picha ya Lowassa tu hapo Jukwaani,kura yangu nitampigia.CCM iondoke kwanza,mengine baadae.
 
kiherehere chenu nyie mauvccm mlikuja kumuangalia na kumsiliza mh.lowasa mlizani atawasifia nyie maboya mimi ukawa sinaga ata mda wa kusikiliza uyo raisi wenu anayetegemewa kumkabizi lowasa madaraka wala siwezi msikiliza kiongozi yeyote wa ccm mahana naweza kutapika aise chalii yangu
 
Linganisha vipaumbele vya hawa Wagombea wetu,

LOWASSA,
1.Elimu
2.Kilimo
3.Afya
4.Mawasiliano
5.Nidhamu pamoja na Utawala bora.

Kwenye kona ya kitalaaam Lowassa yuko vizuri sana amegusa mahitaji ya jamii kwa kutumia lugha ambayo inaeleweka kwa kila mtu, intellectual pamoja na layman

VS
Ahadi za JP Magufuli;
1. Umoja wa Taifa
2. Kulinda Muungano wa Tanzania.
3. Ulinzi na usalama
4. Kuheshimu mihimili ya Dola.
5. Mahakama maalum ya mafisadi na majizi
5. Utawala bora
7. Ataheshimu mawazo yote ya kuleta maendeleo hata yakitoka upinzani
8. Ataimarisha vyombo vya usalama
9. Vita dhidi ya ubadhirifu
10. Kodi ilipwe na wote
11. Ataongeza ajira kwa kuimarisha viwanda
12. Sekta ya kilimo itaimarishwa
13. Sekta ya mifugo itaimarishwa ili iwe na tija kwa kujenga viwanda
14. Madini yatadhibitiwa ili yalete maendeleo
15. Maji yatapelekwa Vijijini na mijini
16. Zahanati kila kijiji, Hospitali ya rufaa kila mkoa, kuboresha maslahi ya wauguzi
17. Elimu bure hadi kidato cha nne, nyumba za walimu zitajengwa.
18. Wanafunzi wa vyuo vikuu, atahakikisha mikopo inakwenda mapema ili wasome
19. Kujenga hostel za wana vyuo
20. Maslahi ya watumishi, kila mtu anayefanya kazi atapata haki yake.
21. Gesi itasimamiwa vyema ili isaidie nchi
22. Barabara zitaboreshwa, flyovers kujenga ya kwanza salander, tazara
23. Msongamano Dsm utashughulikiwa
24. Reli itajengwa upya
25. Bandari, anga zitaboreshwa
26. Maslahi ya maliasili yataboreshwa ili watalii wengi waje ili tupate pesa
27. Serikali itakuwa rafiki kwa wawekezaji wenye nia njema
28. Maslahi ya wafanyakazi yatalindwa
29. Walemavu watalindwa na haki zao zitalindwa
30. Uhuru wa Habari utalindwa na atakuwa na waandishi karibu
31. Wasanii na wanamichezo haki zao zitalindwa, kutakuwa na Mfuko maalum kwa ajili hiyo
32. Reli ya Dar itajengwa

Hakuna Tafiti yoyote duniani ambayo unaweza kutekeleza kwa kuwa na Malengo (objectives 32)kwa Kipindi Cha miaka mitano utaalamu hapo umewekwa pembeni ila utamu wa lugha ndo umewekwa mbele Hakuna uhalisia (insight and realistic)

Hahaahaaa!...ukweli utawauma sana hawa MAFISIEMU SIO SIRI,Alafu mkuu umesahau ile point kwenye ilani ya MAGUFULI anayosema "ATATENGA MILLION.50 KILA KIJIJI KWA AJILI YA WANAWAKE WAJASIRIAMALI" NA ILE ALOSEMA ATAJENGA "BARABARA YA NJIA SITA YENYE FLYOVER SABA"...AMBAVYO VYOTE HIVYO NI UONGO ULIOTUKUKA KABISA maana tukianza na hilo la million.50 kwa kila kijiji...kwa hapa TANZANIA TUNA VIJIJI ZAIDI YA ELFU TATU HIVYO KWA AHADI HIYO INATAKIWA ITENGWE ZAIDI YA TILLION 1.5 KWA KAZI HIYO JEE HII INAWEZEKANA? IKIWA SERIKALI INA MALIMBIKIZO NA MADENI YA WALIMU NA MAKANDARASI KIBAO NA HAIJAWALIPA HADI DAKIKA HII,TUJE NA HILO LA BARABARA YA NJIA SITA YENYE FLYOVER SABA KITU AMBACHO NI UONGO ULIO WAZI IKIWA MWENZIE JK ALIFELI KUTEKELEZA AHADI YAKE YA BARABARA YA "JUU NA CHINI" PALE UBUNGO MATAA ALIYOHAIDI MWAKA 2005 KWENYE KAMPENI ZAKE ZA KUGOMBEA URAIS HADI LEO HII HAJAFANYA HILO,NDO ATAFANYA YEYE??...TENA IKIWA HILO LAKE NI KUBWA ZAIDI YA ILO LA JK SASA.
 
Liuzi lirefu hivi kumpamba mpinzani. Pole sana makitoro
 
Last edited by a moderator:
Sie ukawa hatutaki maneno mengi yasiyo na faida, we ulitaka naye aanze kukariri lugha za makabila mbalimbali masuala ya ngojera pereka huko. Mtu unachagua vitu viwili au vitatu kama alivyosema vingine vyote vitakuja tu cha msingi ni usimamiz mzur wa uchumi

Wanataka tuletewe porojo kama zile ahadi 68 za JK za 2010,hakuna hata tano tu zilizotekelezwa,matokeo yake Mgombea wa sasa anajikuta anaahidi kitu kile kile kilichoahidiwa na Kikwete 2010.Maneno meengi utendaji sifuri.Bora bubu lakini mtendaji.CCM itoke kwanza,mengine baadae!
 
Sindano zimegusa mifupa na dawa imefika katika jeraha.
Kumbe mlikua mnafuatilia live hatua kwa hatua? Neno kwa neno?
Ni furaha kuona mpinzani wako anakufuatilia namna hii.

Hahahaaaa kwa kweli umenikosha na comment yako
 
UVCCM ni moja ya taasisi zilozopoteza mvuto kwa vijana! sababu moja kuu ni kua imekua ikitumika kuandaa watoto wa vigogo kuwa wanyang'anyi badala ya kuandaa viongozi wa baadae. uvccm imebakia kama kijiwe cha wapika majungu na walevi na waganga njaa haina mvuto na ushawishi kwa vijana tangu nchimbi amalize muda wake na pia uvccm ni tofauti na youth tanu iliokua ikiandaa viongozi wa baadae!
 
shaka.jpg


TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM ( UVCCM) MAKAO MAKUU DAR ES SAALAM KWA VYOMBO VYA HABARI JUMAPILI 30 AUGUST 2015.


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho wakiwemo na waliokuwa Mawaziri waandamizi katika Setikali ya CCM, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha wakihutubia mkutano huo.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kusudiwa kama muongozo wa uendeshaji Serikali ukikosa kuainishwa kwenye kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Kwa msingi huo, CHADEMA/UKAWA wameonesha jinsi gani wasivyo na maandalizi ya mkakati wa kitaalam na mipango endelevu kwa maendeleo ya kisekta katika dhamira ya kujenga uchumi imara utakaoimarisha huduma za jamii, kuheshimu misingi ya utawala bora wa sheria huku akionesha kukosa dira makini ikiwemo mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya Serikali yao ikiwa itatokea muujizq wa wa kushinda na kujikuta wakitaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi zinazoendelea.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku na hatimaye atoe majawabu mbadala ya utatuzi wa msingi unaoweza kuaminiwa na wananchi wanaoishi aidha mijini au vijijini.

Lowassa ameshindwa kabisa kukonga nyoyo na kugusa hisia za Watanzania katika mambo ya msingi kwa sababu ya kuandamwa kwake na pupa, kiherehere na kukurupuka toka Chama kimoja hadi kingine huku akiwa hana maandalizi yanayoweza kutoa majibu halisi yanayowakabili wafanyakazi, wakulima, wavuvi, wafugaji, walimu, madaktari, wauguzi pia wasanii na wanamichezo.

Lowassa na CHADEMA, wameshindwa kubainisha dhamira na maandalizi ya kuleta chachu ya maendeleo mbadala kwa sababu sehemu kubwa ya changamoto zilizokuwepo zimetatuliwa hatua kwa hatua kwa kipindi cha miaka kumi iliopita chini uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo sasa mashirika ya Kimataifa ya kusimamia uchumi na fedha ikiitaja Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kuelekea uchumi wa kati.

Sisi UVCCM, tulitegemea sana kuona labda ile shauku , mikiki , hamu na kiu alionayo Lowassa ya kutamani Urais kwa gharama yoyote huenda angekuwaa na mikakati. , sera au mipango mipya ya kushughulikia matatizo yaliyobaki ambayo aidha yamekawia kiutekekezaji kwa ukosefu wa fedha au utatuzi wa matatizo hayo miradi husika imeanzishwa na kutofikiwa suluhisho kwa wakati au baadhi ya viongozi waliopewa dhamana hizo kushindwa kutekeleza kwa muda na wakati muafaka.

Hotuba ya Lowassa kuhusu azma na dhamira yake katika kukuza uchumi, UVCCM tunaifananisha na orodha ya manunuzi (shop list) maana haioneshi viashiria , njia au vyanzo vya mapato ya kukuza uchumi kwa mwendo haraka wa kisera na kujikuta akipiga porojo akifanana na kasuku aliyekariri maneno aliyofundishwa akiyatumia bila kujuwa tija , faida, hasara na maana ya jambo analolikusudia.

Tumeshangaa kumuona akishindwa kuzungumzia masuala ya ufisadi na kutowataja wezi waliopora rasilimali za umma na maliasili za nchi, waliofuja uchumi, wala rushwa watu waliokosa kuwajibika na kutochukuliwa hatua za kisheria kwa masuala mazima ya kukiuka maadili ya uongozi ikiwemo sakata zito za mradi wa kufua umeme wa dharura kupitia kampuni hewa ya RICHMOND ambayo ilimsababishia Lowassa kulazimishwa na Bunge ajiuzulu Uwaziri Mkuu akiwa ni Waziri Mkuu aliyekaa muda mfupi zaidi kuliko yeyote katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

UVCCM tunachukua nafasi hii kuwaasa na kuwaomba sana Watanzania wenzetu kwamba mabadiliko au mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hayahitaji pupa na papara kama iliyotokea kwa wananchi wa Taifa la Libya ambao sasa wako katika dimbwi la majuto.

Viongozi wa Upinzani akiwemo Lowassa na kundi la UKAWA hawana dhamira njema kwa nchi yetu na UVCCM tunawafanisha sawa na manahodha ambao muda mfupi ujao toka sasa watagombea sukani wakiwa katika kina kirefu cha bahari jambo ambalo ni hatarishi kwa maisha na mustakabali wa wasafri waliomo kwenye chombo chenye amani, utulivu, umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa kinachoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Lowassa ameonyesha dalili za kuwa kiongozi dikteta asiyeheshimu hata misingi ya utawala bora hasa pale aliporejea kwa mara ya pili akisisitiza msimamo wake wa kuwaachia huru Masheikh wanaokabiliwa na tuhuma za makosa ya ugaidi ambapo suala hilo sasa lipo mbele ya mahakama na hatutakiwi kuingilia mwenendo wa kesi kulingana na matakwa ya mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili ya dola.

Mbali na suala hilo, pia ameonekana kulizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya juu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekwisha litolea hukumu kesi ya Mwanamuziki Nguza Viking na mwanawe Papii Kocha waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji kana kwamba Lowassa anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza.Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha.Aidha, Lowassa na UKAWA wameonekana kuzungumzia sana dhana ya uzalendo wakati mfumo utokanao na itikadi ya Chama chao imejiegemea katika uliberali usiojali wala uzalendo zaidi ya kuthamini utajiri binafsi, kujilimbikizia mali zisizo na vyanzo na uvukaji wa mipaka isiyozingatia mila, desturi na utamaduni.


UVCCM tumeshangazwa sana na ujasiri uchwara ulionyeshwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye anapothubutu kuzungumzia ufisadi wakati yeye mwenyewe ni miongoni mwa viongozi wanaotuhumiwa kwa kashfa ya uanzishaji wa Televesheni ya Taifa {TVT} na ufufuaji wa fedha za umma , soko la Kibaigwa, tuhuma ya uporaji ardhi huko Tondoloni akitumia madaraka yake vibaya pia chini ya usimamizi wake akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, halmamshauri nyingi za wilaya nchini ziliongoza kupata hati chafu kutokana na matumizi holela ya ruzuku toka serikali kuu kama ilivyofichuliwa na ofisi ya CAG kufuatia upotevu wa fedha za miradi ya maendeleo ya jamii.

Sumaye kinywa chake wakati mmoja kikitoa moto na baridi ndiye aliyekitaka Chama cha Mapinduzi kutompitisha Lowassa kuwa mgombea urais kwa madai ya kuhusika kwake na tuhuma za ufisadi huku akitishia kuhama CCM. Matamshi ya Sumaye yameushangaza ulimwengu na sasa anapopania kumsafisha Lowasa kwa kutumia maji taka akifikiri atasafika ili aaminiwe na watanzania werevu na wazalendo ajijue fika anatwanga maji kwenye kinu.
SHAKA HAMDU SHAKA (MNEC)KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TANZANIA
Zipo taarifa humu kuwa Bashe mgombea Ubunge Nzega kwa tiketi ya CCM amesema Lowassa anatosha, UVCCM zungumzieni hilo, kumjibu Lowassa hakutasaidia kuongeza kura za Magufuri.
 
Inaonesha jinsi mnavyoweweseka, tulieni tu. sindano iwaingie vizuri
 
Back
Top Bottom