Uvumi kuhusu hali ya afya kwa rais wa cameroon, Paul Biya, waendelea kushika kasi

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Siku 44 zimepita tangu Rais wa Cameroon, Paul Biya, aondoke nchini humo kuelekea barani Ulaya kwa kile kinachoelezwa na mamlaka kuwa ni safari ya matibabu. Kutorejea kwake hadi sasa kumeibua maswali, mijadala na uvumi kuhusu hatima ya kiongozi huyo

Rais Biya, mwenye umri wa miaka 93, aliondoka Cameroon tarehe 7 Juni kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matibabu ya muda mfupi. Hata hivyo, hadi sasa hajarejea nchini, hali iliyozua maswali na hisia tofauti miongoni mwa wananchi, wanasiasa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu hali ya uongozi wa taifa hilo.

Chama cha upinzani cha Union Démocratique du Cameroun (UDC) kimeeleza kuwa kutokuwepo kwa Rais kwa kipindi kirefu kunazua mashaka kuhusu ufanisi wa uongozi na utekelezaji wa shughuli za serikali. Aidha, baadhi ya wabunge wa upinzani wamezitaka mamlaka kuweka wazi hali ya urais na kutoa taarifa rasmi kuhusu mwenendo wa uongozi wa nchi.

Kwa upande wake, chama tawala cha Rassemblement Démocratique du Peuple Camerounais (RDPC) kimeendelea kusisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida licha ya kutokuwepo kwa Rais Biya nchini.

Wakati huo huo, baadhi ya wachambuzi wa diplomasia na masuala ya utawala wamezitaka mamlaka za Cameroon kutoa tamko rasmi kuhusu hali ya Rais mara tu kipindi cha kutokuwepo kwake kitakapofikia siku 45, wakisema hatua hiyo inaweza kusaidia kuondoa sintofahamu iliyopo miongoni mwa wananchi.

Licha ya mjadala huo, Katiba ya Cameroon haijaweka bayana utaratibu unaopaswa kufuatwa endapo Rais atakaa nje ya nchi kwa kipindi kirefu kinachozidi siku 45 bila kutangaza rasmi hali ya kutoweza kutekeleza majukumu yake.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu. Mwaka 2025, alitumia takribani siku 42 nje ya Cameroon kwa sababu zilizotajwa pia kuwa ni matibabu, jambo lililozua mijadala kama inavyoendelea kushuhudiwa sasa.

Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982. Mwaka 2008, alifanya marekebisho ya Katiba yaliyofuta ukomo wa mihula ya urais, hatua iliyomruhusu kuendelea kugombea na kushika madaraka. Kufikia sasa, ameiongoza Cameroon kwa zaidi ya miaka 44, na hivyo kuwa mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Chanzo: na Africa News
 
Uvumi umeendelea kushika kasi nchini Cameroon kuhusu hatima ya Rais wa taifa hilo, Paul Biya, ambaye ametimiza siku 44 tangu alipoondoka nchini humo kwa kile kilichoelezwa na mamlaka kuwa ni safari ya matibabu ya afya barani Ulaya.

Rais Biya, mwenye umri wa miaka 93, aliondoka Cameroon tarehe 7 Juni kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matibabu ya muda mfupi. Hata hivyo, hadi sasa hajarejea nchini, hali iliyozua maswali na hisia tofauti miongoni mwa wananchi, wanasiasa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu hali ya uongozi wa taifa hilo.

Chama cha upinzani cha Union Démocratique du Cameroun (UDC) kimeeleza kuwa kutokuwepo kwa Rais kwa kipindi kirefu kunazua mashaka kuhusu ufanisi wa uongozi na utekelezaji wa shughuli za serikali. Aidha, baadhi ya wabunge wa upinzani wamezitaka mamlaka kuweka wazi hali ya urais na kutoa taarifa rasmi kuhusu mwenendo wa uongozi wa nchi.

Kwa upande wake, chama tawala cha Rassemblement Démocratique du Peuple Camerounais (RDPC) kimeendelea kusisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida licha ya kutokuwepo kwa Rais Biya nchini.
chanzo: na Africa News

Wakati huo huo, baadhi ya wachambuzi wa diplomasia na masuala ya utawala wamezitaka mamlaka za Cameroon kutoa tamko rasmi kuhusu hali ya Rais mara tu kipindi cha kutokuwepo kwake kitakapofikia siku 45, wakisema hatua hiyo inaweza kusaidia kuondoa sintofahamu iliyopo miongoni mwa wananchi.

Licha ya mjadala huo, Katiba ya Cameroon haijaweka bayana utaratibu unaopaswa kufuatwa endapo Rais atakaa nje ya nchi kwa kipindi kirefu kinachozidi siku 45 bila kutangaza rasmi hali ya kutoweza kutekeleza majukumu yake.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu. Mwaka 2025, alitumia takribani siku 42 nje ya Cameroon kwa sababu zilizotajwa pia kuwa ni matibabu, jambo lililozua mijadala kama inavyoendelea kushuhudiwa sasa.

Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982. Mwaka 2008, alifanya marekebisho ya Katiba yaliyofuta ukomo wa mihula ya urais, hatua iliyomruhusu kuendelea kugombea na kushika madaraka. Kufikia sasa, ameiongoza Cameroon kwa zaidi ya miaka 44, na hivyo kuwa mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.
takataka dictator wacha life kama linakufa
 
Huyo mzee nakumbuka mwaka 1982 wakati aliyekuwa rais wa Cameroon wakati huo marehemu Ahmadou Ahidjo alipomkaimisha urais kwa muda ili aende kwenye matibabu nchini Ufaransa.

Lakini kimaajabu Ahidjo aliporejea nyumbani ili achukue urais wake ndipo Biya alipotaka kumuweka ndani na kumfanya Ahidjo arudi Ufaransa na kuwa mkimbizi kabla ya kufariki kwa presha.

Hivyo ndivyo waafrika tulivyo mbele ya madaraka. Heri punda afe lakini mzigo ufike.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Dah! Hiyo nchi ameigeuza sasa kuwa mali yake binafsi, miaka 44 yote anaongoza kwa mkono wa chuma, hata hivyo kwa umri huo wa 93 probability ya kuaga dunia ni kubwa sana, soon Cameroon itapata Rais mpya
 
Siku 44 zimepita tangu Rais wa Cameroon, Paul Biya, aondoke nchini humo kuelekea barani Ulaya kwa kile kinachoelezwa na mamlaka kuwa ni safari ya matibabu. Kutorejea kwake hadi sasa kumeibua maswali, mijadala na uvumi kuhusu hatima ya kiongozi huyo

Rais Biya, mwenye umri wa miaka 93, aliondoka Cameroon tarehe 7 Juni kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matibabu ya muda mfupi. Hata hivyo, hadi sasa hajarejea nchini, hali iliyozua maswali na hisia tofauti miongoni mwa wananchi, wanasiasa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu hali ya uongozi wa taifa hilo.

Chama cha upinzani cha Union Démocratique du Cameroun (UDC) kimeeleza kuwa kutokuwepo kwa Rais kwa kipindi kirefu kunazua mashaka kuhusu ufanisi wa uongozi na utekelezaji wa shughuli za serikali. Aidha, baadhi ya wabunge wa upinzani wamezitaka mamlaka kuweka wazi hali ya urais na kutoa taarifa rasmi kuhusu mwenendo wa uongozi wa nchi.

Kwa upande wake, chama tawala cha Rassemblement Démocratique du Peuple Camerounais (RDPC) kimeendelea kusisitiza kuwa serikali inaendelea kutekeleza majukumu yake kama kawaida licha ya kutokuwepo kwa Rais Biya nchini.

Wakati huo huo, baadhi ya wachambuzi wa diplomasia na masuala ya utawala wamezitaka mamlaka za Cameroon kutoa tamko rasmi kuhusu hali ya Rais mara tu kipindi cha kutokuwepo kwake kitakapofikia siku 45, wakisema hatua hiyo inaweza kusaidia kuondoa sintofahamu iliyopo miongoni mwa wananchi.

Licha ya mjadala huo, Katiba ya Cameroon haijaweka bayana utaratibu unaopaswa kufuatwa endapo Rais atakaa nje ya nchi kwa kipindi kirefu kinachozidi siku 45 bila kutangaza rasmi hali ya kutoweza kutekeleza majukumu yake.

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Biya kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu. Mwaka 2025, alitumia takribani siku 42 nje ya Cameroon kwa sababu zilizotajwa pia kuwa ni matibabu, jambo lililozua mijadala kama inavyoendelea kushuhudiwa sasa.

Paul Biya amekuwa Rais wa Cameroon tangu mwaka 1982. Mwaka 2008, alifanya marekebisho ya Katiba yaliyofuta ukomo wa mihula ya urais, hatua iliyomruhusu kuendelea kugombea na kushika madaraka. Kufikia sasa, ameiongoza Cameroon kwa zaidi ya miaka 44, na hivyo kuwa mmoja wa viongozi waliokaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

Chanzo: na Africa News
Miaka 93 🙆
 
Huyo ndio rais mzee sana duniani kwa sasa na nchini Cameroon ni marufuku kuongelea kuhusu afya yake.
 
Back
Top Bottom