maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,311
- 15,640
Kuna uzushi umeenea sana kwenye magroup ya WhatsApp kuhusu unga wa mahindi kama inavyoonekana kwenye picha.
Mwanzoni nilipuuzia ila kila group naikuta. Kimsingi wabongo elimu ya fortification (uongezaji virutubishi kwenye unga kwa ajili ya kupunguza utapiamlo na udumavu bado hawajaielewa.
Kuna kazi kubwa inahitajika kwenye elimu maana inaonekana hata mamlaka zetu hazitilii maanani.
Kiufupi unga wote wa ngano tunaokula kwenye maandazi, chapati, mikate etc umeongezwa virutubishi kisheria tangu mwaka 2011, ila sababu kwenye unga wa mahindi haikutiliwa mkazo basi sasahivi inaonekana ni kitu kipya.
Na ni virutubishi vilevile kama kwenye unga wa ngano (Iron, Zinc, Folic Acid, Vitamin B12).
Nawasilisha.
===
UFAFANUZI WA TBS
Hivi karibuni, kumekuwepo na taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoeleza kuhusu kiwanda cha "Mr and Mrs Jonsson-Johnsson Varmland Hagfors kuzalisha unga wa mahindi (sembe) ujulikanao kwa jina la "Jonsson Lishe- Sembe Mswed" unaosemekana "kuwekwa madawa ya kuua nguvu za kiume na kuongezea hormones za ushoga".
TBS inapenda kuujulisha umma kuwa mzalishaji huyo anamiliki kiwanda cha kuzalisha unga wa mahindi ulioongezewa virutubisho (fortified maize flour) kilichoko mkoa wa Tanga, wilayani Lushoto ambacho mifumo yake ya uzalishaji pamoja na ubora wa bidhaa hiyo vimethibitishwa na TBS na kupewa Leseni ya kutumia alama ya Ubora yenye namba 5657. Hata hivyo, kiwanda hiki kilisimamisha uzalishaji toka mwezi Januari 2024 kutokana na kukosa malighafi.
Aidha, baada ya uchunguzi TBS imebaini kuwa mzalishaji huyo amefungua kiwanda kingine nyumbani kwake katika mkoa wa Pwani wilayani Bagamoyo kinachozalisha unga wa mahindi ulioongezewa virutubisho (fortified maize flour), ambacho kilifanyiwa ukaguzi na kugundulika hakijathibitishwa na TBS. TBS ilichukua sampuli ya unga wa mahindi unaozalishwa na kiwanda cha Bagamoyo na kuifanyia uchunguzi wa kimaabara na kuthibitisha kuwa imeongezewa virutubisho kwa mujibu wa Kiwango cha bidhaa hiyo. Utaratibu wa kuongeza virutubisho vya vitamini na madini kwenye unga wa mahindi unakubalika kwa mujibu wa Kiwango cha Kitaifa na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.
Hata hivyo, TBS imechukua hatua za kusimamisha uzalishaji na usambazaji wa bidhaa zinazozalishwa na Kiwanda cha Bagamoyo hadi hapo mhusika atakapokamilisha taratibu za kupata leseni ya kutumia. alama ya ubora.
TBS kupitia mifumo yake ya kiudhibiti itaendelea kuhakikisha kuwa bidhaa hiyo pamoja na bidhaa nyingine za chakula zinaendelea kukidhi matakwa ya viwango ili kulinda afya ya watumiaji.