Uvumi unaendelea kuhusu unga kutiwa vitu vya kupunguza nguvu za kiume na kuchochea ushoga

Nenda kanisani mkuu mengine uachie ulimwengu.....


Lakini wewe umejuaje unga una madhara?? Umeadhirika??
 
Na hizo hormone za ushoga ndio kitu gani....?
 
Serikali kwa maana ya TBS imeishatoa ufafanuzi kuwa unga uko sawa,msipende kuchafua biashara za wezenu
 
Mkuu Hii ni mbinu za kuchafua biashara za watu,hivi unajua kazi za TBS au umeamua kuandika tu,harafu ujue nakuona mtu mzima wewe ila kuna wakati huwa unafikia hitimisho kitoto sana.
 
Kama ni kweli basi TBS na TFDA zifutwe zimewaumiza watanzania wengi sana kupitia kutowajibika na rushwa
 
Mtasingizia mno ushoga unaenezwa na wajomba na majirani kuwalawiti watoto wa kiume
 
Ujinga ni 98% kasoro Mimi, wewe na baadhi ya Watu...
 
Kuna nini nyuma ya hivi virutubishi?

Mbona wazee wetu wame survive miongo Kwa miongo pasipo hayo mavirutubisho?
Lakini ndio wazee wajinga kuliko wa ulaya japani na kwineko.
 
ujue humu ndani kuna watu wanafanya wanajielewa,wamesoma na wanaelimu kumbe unga tu,,kufanya assumptions si vibaya kwa mwananchi na huwezi jua l;abda kuna thirdy party au whistler blower wa kwenye kampuni amefanya hayo kwa lengo la kuokoa umma.

inakuwaje wewe ambayo hujui lolote unaropoka watu kuwa hawana elimu wkt ni muhimu mtu kudadisi,kwani agenda za washirika wetu hatuzijui?

zipo stori za viongozi za dini kuchukuliwa kule mkuranga sijaona serikali ikikanushapia kuna ile ripoet ya mwakyembe sijaona kukanushwa na kuna mchakato wa paul makonda sijaona kukanushwa kwahiyo tusiangalie upande wa kupata uthibitisho tu,watu wanafanya siri ili kutimiza malengo yao.
 
Kuna nini nyuma ya hivi virutubishi?

Mbona wazee wetu wame survive miongo Kwa miongo pasipo hayo mavirutubisho?
Aina ya nafaka walizokuwa wakila hivi sasa hazipo, yale maharage tuliyokuwa tukichanganya na vipande vya maandazi kutengeneza zege hayapo. Ladha ya mahindi ya kuchoma au kupika si ile ya zamani, hivi sasa ni kama unakula pumba tu, mbolea za chumvi na mbegu za kutengenezwa maabara zimeharibu ubora wa nafaka, hivi sasa tunakula ili tuishi tu.
 
Hakuna kitu kama hicho, hizo ni propaganda za wajinga huku Afrika. Ushoga hauji kwa kulishwa vyakula, bali kwa kulishwa taarifa, na taarifa hizo zimejaa Facebook, Twitter, Instagram, Google, Youtube, Whatsapp nk. Kataa kutumia hizo platform (kama utaweza!) ili uepuke kuwa shoga kama unaogopa sana ushoga kwa style hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…