DOKEZO Uvunjifu mkubwa wa Sheria za Mazingira na Makazi Misugusugu, Kibaha - Pwani

DOKEZO Uvunjifu mkubwa wa Sheria za Mazingira na Makazi Misugusugu, Kibaha - Pwani

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa mtaa unaitwa Vitendo, Kata ya Misugusugu, Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.

Hapa jirani yangu kimejengwa kiwanda kikubwa cha kuten geza Ethanol na vingine vinavyotokana na molasses ya miwa.

Tatizo linakuja, kiwanda kimejengwa ubavu kwa ubavu na makazi, kuna shule mpya ya sekondari, kuna madrasa kunamakazi yetu kwa miaka. Cha kushangaza, kimejengwa kiwanda hiki ambacho hata tafiti ndobdoigo tu za kwenye mitandao zinaonesha kina madhara makubwa kikiwa karibu na makazi ya watu kama hakikufata sheria za usalama wa mazingira na afya za wakazi na wafanyakazi. Tunaoishi hapa tunadiriki kusema hiki kiwanda hakikufata sheriaz zote za NEMC, OSHA z Ardhi lakini tunasangaa kimeweza kujengwa na kuanza uzalishaji ilhaji maafa yanjinesha waazi kabisa.

Maafa yaliokwisha jitokeza mapema kabia ni...

1) Kiwanda kinatoa mvuke wa unyevunyevu unaotoa harufu kali zinazopelekea watu kuumwa na kichwa, watu kuwashwa mwili, watu wenye pumu kuwajia mara kwa mara na kearoi ya harufu kali ya kemikali kwa masaa 24.

2) Kuna moshi wa kuni au kitu kibachofanana na kuni saa zote, moshi mweusi ambao unazagaa na kutoa harufu ya moshi wakati wote, sema kuna muda ndio unakua mwingi na kwa muda mrafu unakua unasikia harufu tu ya kuungua kuni.

3) Kelele za kama mvuke kutoka kwenye mabomba kwa wakati eotw na kuna wakati zinakuja kelele kwa dakika mbili au tau, ambazo naamini hazikidhi vigezo vya uchagfuzi wa mazingira ya kelele. Ni kelele kubwa za ajabu zinazikuja kila lisaa limoja au mawili.

Cha ajabu, binafsi nilituma malalamiko kwenye group letu la kata la whatsapp, Diwani wetu, akajibu kua, "si mmeuz viwanja wenyewe, sasa mwekezaji kishaweka zaidi ya milioni 30 ndio mnasema". Diwani akanipigia simu lakini hakuna chochote alichonambia kua kimechukulikwa hatu na mamlaka yake au ya halmashauri au mkoa au taifa, kunusuru hali za wakazi wa hapa.

Sikuishia hapo, nikajaribu sana, ku[piga simu Wilata ya kibaha, lakini simu zinaonesha zimewekwa tu kwenye tovuti hazijibiwi, Nikapiga simu NEMC hazijibiwi, nika[piga simu OSHA hazijibiwi, nikapiga simu TLS ili tupate msaada wa kishria nako hazijibiwi.

Hali inasikitisha sana. Nakaribiusha wsnaharakati, wanasheria, waziri wa mazingira, NEMC, Halmashauri an yeyote anaeweza kuwa msaaea kutuokoa na hii hali atupigie. Hivi sasa naanza kujitahidi kuwapata vingozi wa kata yangu wa CCM walipeleke mbele hili suala.

Tunahfia sana afya zetu wakazi wanaozunguka hiki kiwanda. Meengine alionijibu diwani wetu kwenye simu hayaelezeki hapa. Lakini kama kuna kingozi yeyote atakua na hamu ya kuyaelewa anipigie namba hizo chini.

Naapa nitasema kweli daima, uongo kwangu mwiko.
 
Mipango miji Nchi hii ni sifuri kabisa.kunakiwanda kingine Cha wachina Cha plastic kipo makazi ya watu tena viongozi(mawaziri) hapo mikocheni.hiki kiwanda wakati wa uchakataji wa hizi plastic,vipande vingi vidogovidogo husambaa Kwa wingi kwenye mitaro ya maji na kusafirishwa Hadi baharini na kuhatarisha maisha ya viumbe baharini.NEMC wamelala usingizi.
 
 
Back
Top Bottom