Uwajibikaji ajali ya ndege ndiyo imeisha hiyo

Uwajibikaji ajali ya ndege ndiyo imeisha hiyo

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Tayari serikali imeshatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege iliyopata ajali wakati inatua uwanja wa Bukoba.

Taarifa hiyo ya uchunguzi inakiri wazi uzembe wa kitengo cha dharura na uokozi uwanjani hapo. Pia hata kuleta mkanganyiko unaoiumbua serikali hususani ofisi ya Waziri Mkuu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuhusu shujaa waliyemtengeneza aitwaye Majaliwa ambaye alipata sifa lukuki na hata akapata ajira jeshi la zimamoto na uokoaji.

Picha na video mbali mbali zilizorushwa kwenye mitandao ya jamii vimeonesha namna ambavyo wananchi wakitumia vyombo vyao duni kufanya uokozi hata kuiopoa ndege kutoka ziwani

Watanzania tumepoteza ndugu zetu katika ajali ile. Watanzania tumeshuhudia uzembe mkubwa unaojirudia rudia kila maafa na ajali zinapotokea. Watanzania tumeshuhudia uwezo mdogo wa serikali katika kutoa msaada kwenye matukio ya dharura. Lakini serikali hiyo hiyo inazo silaha na zana za kutosha za kuzuia michakato ya kikatiba hususani mikusanyiko ya vyama vya upinzani kila kona ya nchi.

Serikali inayopaswa kutoa ulinzi kwenye mikutano ya wapinzani inasema haina ulinzi wa kutosha ilihali inao askari wauaji wa kutosha kudhibiti mikutano hiyo pale inapojiri.

Katika hili la ajali ya ndege; Tumeshasahaulishwa na kama ilivyo ada tumepigwa matukio ya kutusahaulisha hata kufikikia watu wazima kutukanana na marehemu kama wanajibizana vile.

Serikali chini ya Rais imegoma kuwajibika kuhusu ajali hii. Serikali yetu inatupuuza kiwango cha kutisha ndo maana wanasheherekea kugawana vyeo na kujisimikia mikakati ya madaraka kwa chaguzi zijazo.

Je, ni wakati sasa wa kumuwajibisha Rais kwa kushindwa kutimiza wajibu wake? Kwa nini hapana?
 
🤣🤣🤣🤣🤣 hii nchi tamu sana, hv ripot ya awali ilikuwa itolewe tena baada ya muda Gani. Mbona hiyo ripot ni kama imepita kimyakimya. Kunamoja ilisambaa sambaa msemaji wa serekali akakanusha kwamba sio yenyewe.
 
Hakuna uwajibikaji, sana sana watakuja kukushambulia humu kwa kuanzisha mada kama hizi kwamba zina mlengo wa kuharibu ushujaa wa dogo majaliwa.
 
Bashiru kapoteza issue ya ajali ya ndege
Tayari serikali imeshatoa taarifa ya uchunguzi wa ajali ya ndege iliyopata ajali wakati inatua uwanja wa Bukoba
Screenshot_20221210-075017_Twitter.jpg
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] hii nchi tamu sana, hv ripot ya awali ilikuwa itolewe tena baada ya muda Gani. Mbona hiyo ripot ni kama imepita kimyakimya. Kunamoja ilisambaa sambaa msemaji wa serekali akakanusha kwamba sio yenyewe.
Ndo ileile tu
 
Back
Top Bottom