SoC02 Uwajibikaji katika maadili

SoC02 Uwajibikaji katika maadili

Stories of Change - 2022 Competition

KHALFAN CHETU

Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
10
Reaction score
10
Kama ambavyo Jasusi anahakikisha anaifanya kazi yake kwa uweledi ndani au hata Nje ya mipaka ya Taifa lake ili kuifanya NCHI yake iwe mahala salama na penye maendeleo ya uhakika dhidi ya wazandiki wa kiuchumi na kisiasa wanaotaka kufanya hujuma,ndivyo hata mimi na wewe tunavyopaswa kuwajibika kuhakikisha MAADILI ya Jamii zetu yanabaki kwenye viwango vinavyokubalika kupitia kipimo cha dhana ya kuwa Waafrika.

Tuwe tayari kuendelea kuupokea Utandawazi pasina kuyapokea MAADILI MABOVU kwa kuamini kuwa Maadili hayo ni sehemu pia ya UTANDAWAZI, Kwasababu JAMII inayohusudu Mapinduzi ya Kiteknolojia na Uvumbuzi itakua sawa na Mtema Kuni anaejaribu kumnusuru Suala dhidi ya mawindo ya Simba mwenye njaa kali kwa kutumia kipande cha Mti kama Silaha,ikiwa tu suala la Maadili tutaliacha nyuma.

Mungu alimuumba Mwanadamu, kisha akampa KANUNI za kuzishikilia na kuziishi,kisha akampa NAFSI iliyobeba Akili,Hisia na Utashi.. Kama watanzania, tumekua tukizitumia Akili zetu kuwajibika,lakini Utashi wetu ndio utakaotufanya tutofautiane katika maeneo ya kuwajibika nayo zaidi kwasababu wengi wetu tunawajibika kwa kuzifuatisha Hisia ndio maana Zama hizi wapo Vijana wanaotumia nguvu kushiriki katika Matukio ya Unyang'anyi, lakini pia wapo wengi wanaotumia nguvu kushiriki katika shughuli tofautitofauti za halali ili kujipatia Vipato.

Jamii kwa ujumla inapaswa kuwajibika kwa pamoja ikiwemo Serikali kuhakikisha Taifa linakaa katika Muundo mzuri wa Kimaadili kwasababu Viongozi wa baadae,Raia wa baadae, Wazazi na Watumishi wote wa baadae hawatolifaa Taifa ikiwa Suala la Maadili litakua Gumu kulikazania kwenye kizazi hiki.

Licha ya kila Taifa kuhitaji Uchumi mzuri,Na Teknolojia nzuri,ni Jukumu la Serikali sasa na Raia kuhakikisha hatuziparamii Dhana za Maisha Mazuri na Kamilifu kwa kuipa kisogo Dhana ya Maisha Muhimu ambayo Mungu ametutunuku kupitia Asili.

Unyeti wa suala la Maadili yetu ulivyo ni Sisi tu ndio tunaopaswa kuwajibika nao kwasababu,Mashirika binafsi ya Kijamii,Asasi binafsi za Kisiasa na Kimaendeleo zipo tayari kuonyesha Miitiko ya haraka katika kuisaidia Jamii kwenye masuala ya Kimaendeleo,Haki za Binadamu, na Mienendo ya Kiuongozi ama hata kutusaidia kuishutumu Serikali kwa mambo mbalimbali lakini si kwenye kusafiri na Sisi katika SAFARI yetu ya kuyalinda Maadili.

Kuna sababu nyingi sana zinazopelekea mmomonyoko wa Maadili ambazo kama Serikali na Jamii kwa pamoja tungeshirikiana basi kwa kiwango kikubwa Maadili yangebaki Salama vizazi kwa vizazi licha ya Utandawazi kuendelea kushamiri. Matukio mengi ya Kihalifu huwa Serikali inapambana kuyakabili Matokeo yake na Si vyanzo vyake ndio maana tumejisahaulisha ya kwamba Matumizi ya Pombe na Sigara ndiyo yanayochochea Vijana wengi kutumbukia katika Matumizi ya Bangi na Madawa ya Kulevya,Lakini pia sababu ya Watu wengi kuwa Mashoga au kubakwa inatokana na Mlawiti/Mbakaji alilewa au Mlawitiwa/Aliebakwa alifanyiwa hivyo baada ya kulewa kupitiliza.

Kwahiyo, suala la kuwajibika katika kulinda Maadili,haliwezi kufanikiwa kwa kuendekeza Propaganda Hasi kama ambavyo Kampeni za Uzazi wa Mpango na Matumizi ya Kondomu zinavyotupotosha Vijana badala ya kutuhamasisha Vijana kuepukana na Ngono kabla ya Ndoa. Mwishowe pasina kutumia Akili za Kuzaliwa tumekua tukiamini zaidi Jela,Polisi na Mugambo kama Nyezo za kudhibiti Uhalifu wa Vijana kama Panyarodi kwasababu ya Uroho wa Kodi za Wazalisha Pombe na Sigara huku tukisahau kuwa tunazalisha Mashoga,Watoto wa Mitaani,Wezi,Majambazi na Malaya.

Ukifanya Tafiti utagundua kuwa Vijana waliopo kwenye Makundi ya Kihalifu,Wengi wao walitokea kwenye Familia ambazo Wazazi/Mzazi alishindwa kuwahudumia kwasababu ya Ulevi na si kwasababu hakuwa na Kazi. Tutagundua pia kuwa Ndoa nyingi zinavunjika kwasababu ya Mwanaume kushindwa kulimudu Tendo la Ndoa kutokana na Madhara ya Utumiaji wa Pombe, Na mbaya zaidi Mwanaume kwa kuzikwepa Fedheha atakua akijihusisha na Vitendo vya kuwaingilia Watoto wadogo na Kuwalaiti anaposhikwa na Hisia ili kuepukana na zile Fedheha anaposhiriki na Wakubwa wenzie.

Tutakapoacha kuyatazama Maadili kwa Upeo wa chini ndipo tutakapoelewa kuwa haifai Kitu kuongeza Magereza,haifai Kitu kupoteza Fedha nyingi kwenye Bajeti ya Wizara ya Ulinzi,haifai Kitu pia kuipinga Rushwa ya Fedha na Ngono ikiwa Pombe na Sigara zitaendelea kuzalishwa ili kuzitumia Nguvu-Kazi kwenye Viwanda kukuza Uchumi zitakazoua Nguvu-Afya kwenye Jamii zetu.

Nilipokua Shuleni kati ya Mwaka 2014 mpaka 2017 nikiwa kama Mwanafunzi wa Sekondari,haikuniitaji kuzisubiri Tafiti wala Makala kutoka kwenye Mashirika Makubwa Ulimwenguni ili kuijua Hali Halisi na hata kupata Makisio ya Hali ya Kiafya, Kiusalama na Kimaadili ya Miongo kadhaa mbele, bali ni kupitia Mambo niliyokua nikiyashuhudia kwa Wanafunzi wenzangu tu, yalinipa Picha halisi. Wapo wiliotambulika kwa kumbukumbuku za kubakwa Udogoni,wapo walioshinikiwa kufanya Ngono na Baba zao wa Kambo,wapo vijana ambao tayari walikua Wakijihusisha na Uuzaji wa Bangi, Wapo pia wanafunzi ambao waliishi kama Wapenzi na kama haitoshi wapo Walimu waliokua wakiwasumbua Wanafunzi wa Kike ili washiriki nao Tendo kama Wapenzi. Wapo marafiki zangu ambao iliwalazimu kufanya Kazi wakiwa bado Wanafunzi kwasababu Familia zao zimeharibiwa kwa Ulevi wa Baba zao.

Yote hayo hayamaliziki kwa Propaganda za Makaratasi na Peni chini ya Mwamvuli wa Usomi,bali ni kwa kuijua Mizizi ya Matatizo na Kuichimbua ili isiote tena.

Serikali na Jamii inapaswa kuhakikisha Mafundisho ya Kiimani kwa Watoto na Vijana ni lazima,Kuwajengea Vijana Mazingira Rafiki ya kujitafutia Vipato,Kuviua au kuvipandishia Kodi kubwa Viwanda vizalishavyo VILEO ili kupunguza uzalishwaji.

Pia wajikite zaidi katika kukataza na kulaani Mahusiano ya Kingono kabla ya Ndoa badala ya kuhamasisha Matumizi ya Kondomu na vidhibiti Mimba. Athari za mmomonyoko wa Maadili haziwezi kupatiwa Tiba kwa kuamini Viongozi wana Maamuzi Sahihi nyakati zote.

Inatupasa sasa tuache kuuandamanisha Ukweli na Uongozi kwasababu sio kila Kiongozi ni Mkweli ila kila Mkweli Asili humzawadia Cheo mara zote. Anaweza asiwe Raisi, Mwenyekiti wala Mkurugenzi ila akawa Mwalimu, Kiongozi wa Kiimani au hata akawa Raia mwema.

Haiingii Akilini Viongozi wapo, kisha badala ya kupinga Mahusiano ya Kimapenzi kwa Vijana kabla ya ndoa, Eti wamekubali Maadili yavunjike ila kwa kutumia Kondomu, Je Kijana mwenye Ulevi wa Ngono unawezaje kumfuatilia kwenye kila Tendo kuhakikisha anavaa Kondomu?,

Na Je, Mtu ambae Ulevi ndilo jambo analolipenda, Anawezaje kukumbuka kuwa UNYWAJI WA POMBE KUPITA KIASI NI HATARI KWA AFYA YAKE, ikiwa Chupa kadhaa tu alizokunywa zinamharibu Akili?

Kama ambavyo Viganja vya Mvuvi havikosi Shombo anapokua akiziandaa Nyavu Ufukweni,Ndivyo hata Serikali na Viongozi wasio na Upeo hawakosi Dosari katika Maamuzi, Uwajibikaji na Mifumo yao ya kudhibiti Matukio ya Uhalifu.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom