Jaquelines
New Member
- Jul 28, 2022
- 4
- 3
Utangulizi
Uwajibikaji ni neno la Kiswahili linalotokana na neno 'wajibu' likiwa na maana ya jambo la lazima ambalo mtu au watu fulani kulifanya. Uwajibikaji wa malezi ya watoto katika familia, jamii na hata taifa zimandio hulea mabadiliko (manufaa au yasiyo na manufaa) katika jamii au taifa hilo. Kwa mfano tunaposikia majina kama watoto wa siku hizi, vijana wa siku hizi mara nyingine wamama wa siku hizi ni matokeo ya jinsi na namna wazazi, walezi na jamii nzima ilivyowajibika katika malezi ya makundi haya. Suala la malezi bado ni la kusuasua na kuonekana kubwa kwa kila mtu. Hii imetokana na wahusika kushindwa kutambua nafasi zao katika malezi au kutambua na kupuuza.
Suala la malezi limekuwa ni la mzazi peke yake na mara nyingine mzazi mmoja na siyo kwamba wengine hawaoni. Lah! Wanaona lakini wanakosa sababu au msukumo wa kurekebisha kile wanachoona hakijakaa sawa au pengine wewe mzazi hutaki kuambiwa wala mtu kusema jambo linalokuhusu. Ukali na ukorofi wa wazazi wengi umekuwa kikwazo kwa jamii kukemea uovu na tabia changa zisizofaa. Ili kuepuka migogoro na vikwazo ni bora jirani au hata mzazi mwenza kukaa kimya jambo ambalo siyo sawa. Wakati mwingine kuna mtu amechukua hatua ya kukemea uovu ambao ameuona lakini kwao yule mtoto ni jambo la kawaida au hajawahi kukemewa kwa kufanya hivyo.
Mfano matumizi ya maneno makali yenye kudhalilisha, pengine kwao yanatumika bila kificho jirani ukionya ni sawa na bure tu. Kama mzazi, mlezi, na jamii kwa ajumla, kila mmoja akisimama kwenye nafasi yake, likitambuliwa jema na baya kwa wote na yakasimamiwa kidete watoto wa siku hizi, vijana wala wamama wa siku hizi hawatakuwepo kwenye jamii. Kila mtu katika jamii anayo haki na wajibu wa kukemea uovu katika jamii anamoishi. Usiache mtoto kufunzwa na ulimwengu kabla yako.
Wajibu wa mzazi katika malezi.
1. Mzazi anatakiwa kusikiliza mahitaji na maoni ya mtoto pia kuyafanyia kazi pale inapowezekana ili kuepuka nafasi hiyo kuchukuliwa na mtu wa mbali.
2. Kukaa karibu na mtoto na kutengeneza urafiki ili kujua mambo anayopitia katika nyanja zote za maisha. Ni rahisi pia kutatua changamoto zake anazopitia kwa kuwa muwazi kwako.
3. Kuchunguza tabia na mwenendo wa mtoto ili kuupa nguvu au kuukemea. Hapa yafaa uchunguze hata yale unayoambiwa na fulani kumuhusu.
4. Kushirikishana taarifa na mzazi mwenzio zinazowahusu watoto wenu ili kujua njia sahihi na yenye mafanikio. Hutaweza peke yako maana kidole kimoja hakivunji chawa.
5. Kutambua sehemu ya adhabu na ushauri unapoona kosa, shirikiana na chanzo cha taarifa kujua maendeleo ya tabia ambayo umeambiwa na usijaribu kukaa upande wa mwanao kila unapopewa taarifa yake mbaya.
Malezi yasiegemee upande mmoja tu bali pande zote mbili za wazazi. Baba au mama usione kuwa wewe ndiye unatoa kila hitaji basi mwenzio ahusike na tabia; hapana. Mahitaji kutimizwa hakumfanyi mtu kuwa bora kama hana msingi mzuri wa tabia. Mama unaanza kuona viashiria vingi vya tabia kuliko mtu mwingine yeyote, usipochukua hatua hatua mapema atakuwa mzigo wako.
Ili wazazi mtimize wajibu wenu ni lazima muwe na kusikilizana, kushirikishana na kuchunguza mlichosikia.
Mapungufu
-Mzazi kutokukubali ya kwamba mtoto wake ameweza kufanya jambo fulani, kuona kwamba hajafikia kiwango cha kufanya kosa kubwa namna hiyo. Kwa kuwa ameambiwa na hajaona hawezi kuamini wala kukubali. Swali ni kwamba, je, unajua anao uwezo wa kufanya mangapi?
-Mara nyingine wazazi kukataa ukweli wa mtoto kuwau wa jamii nzima na kwamba yeyote katika jamii anaweza kumkosoa na kumkemea anapokosea.
-Vilevile mzazi mwenyewe anapuuzia nafasi aliyo nayo yeye katika mabadiliko ya tabia ya mtoto. Jinsi unavyoishi naye nyumbani ndivyo ataishi na watoto wengine na hata jamii. Kila mzazi awe na sauti ya kukemea uovu nyumbani na kusikilizana.
-Hata hivyo kujikubali kupita kiasi kunawapoteza watoto. Mzazi anaona kuwa yeye anatoa malezi bora sana hivyo siyo rahisi mwanaye kukosea au kufanya jambo lisilokubalika. Kumbe mzazi ndiye yupo gizani, jamii na walezi wanaona lakini haambiliki.
Wajibu wa Mlezi
●mlezi asimame pale ambapo ameina mzazi amepaacha wazi, ama pengine amepagusa lakini hakumaliza. Huenda ikawa hana muda wa kumsikiliza mtoto au kusema naye, simama mahali hapo au mwambie mzazi wake.
●Wakati kuna vitabia vinaonekana
kwenye mgongo wa mzazi na wewe mlezi unaviona, usisubiri mzazi aone madhara ya kinachofanyika nyuma yake. Toa sauti, onya, kosoa na ikibidi washirikishe wazazi kuhusu tabia za mtoto wao. Ushirikishwaji utaleta mabadiliko ya mwenendo ulioanza kuota na kuupoteza.
Kuna uwezekano wa majukumu haya kushindikana kama hakuna maelewano kati ya mlezi anayeona mabadiliko na wewe mzazi uliye gizani. Pengine wewe mzazi unasimama sana upande wa mwanao akifanya kosa. Kwa yote haya mawili, mlezi hataweza kutoa sauti yake kwa mwanao ili kuubadili mwenendo wake.
Mapungufu
-Mlezi kupuuzia ule wajibu alionao kwa mtoto kwa kuona kuwa hata mzazi wa yule mtoto anaweza kufanya wajibu huo. Ni ngumu kwa sababu kuna mambo ambayo mzazi hawezi kuyaona na mlezi unayaona. Ina maana kwamba mlezi usipofanya kitu kwa ajili ya tabia unayoona, hskuna atakayefanya jambo kwa kitu asichoona.
-Mlezi kuona kuwa mabadiliko ya tabia mbovu ya mtoto wa fulani ni ya wazazi wake pekee. Yaani anaona akisema na kukemea jambo lisilofaa anatumia nguvu ambayo hatapata chochote kwa kuitumia. Lakini usiposema leo kesho utajutia kwani matokeo ya uovu uliouacha ukastawi siyo kwa wazazi wake pekee.
-Jambo lingine ni usasa kwa maana kwamba mtu wa pembeni anaona kuonya ama kushauri mtoto asiye wa kwake ni kuingilia maisha ya watu wengine; hivyo kuacha jambo kama lilivyo. Hii siyo sawa kabisa, kukemea uovu unaoanza ni kujikinga na kuwakinga wengine. Weka usasa pembeni, kuwa chachu ya mabadiliko pengine mzazi alishawaza pa kuanzia, ukisema utakuwa umempa nguvu ya kuendelea.
Wajibu wa Jamii
●Jamii inao wajibu wa kusimama na kutoa sauti pale mzazi na mlezi aliposhindwa au alipokwama kufanya jambo. Pale mzazi na mlezi walipochukua hatua na kila jitihada aliyoweza kumrekebisha mtoto lakini hakufanikiwa. Jamii haitakiwi kukaa na kutazama jinsi mzazi au mlezi anavyochukua hatua zisizo na matokeo chanya, bali isimame naye ili kuhakikisha kuwa lile jambo linafanikiwa. Ni wajibu wa jamii kusaidia ili wasioze samaki wote.
●Lakini pia kuna tabia zisizoonekana kwa mzazi na mlezi au kwa watu wa karibu na tabia hizi huonekana kwa watu wa mbali ambao hawana uhusiani wowote na watoto. Kama watu hawa wakiweza kutoa sauti zao kuhusu mwenendo wa yule mtoto, mzazi na mlezi nao watasimama kuchangia mabadiliko chanya kwa familia zao na jamii nzima.
Madhara ya Kutofanya Wajibu
1. Kuporomoka kwa maadili ambapo ni janga la jamii nzima.
2. Kuongezeka kwa vitendo vya kikatili .
3. Kuwa na jamii isiyo na maendeleo na mipango endelevu.

Upvote
1