SoC03 Uwajibikaji katika nyanja mbalimbali

SoC03 Uwajibikaji katika nyanja mbalimbali

Stories of Change - 2023 Competition

Nyanda Banka

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2023
Posts
304
Reaction score
1,054
Utangulizi

Uwajibikaji ni ile hali ama kitendo cha mtu kutimiza majukumu yake yanayompasa kufanya bila kuwepo na shuruti ya aina yoyote. Katika huu ulimwengu wa sasa inamfaa kila mtu awe muwajibikaji katika kila nafasi yake aliyokuwepo kwani bila kuwepo kwa uwajibikaji inaweza ikaleta athari hasi katika jamii na ulimwengu mzima.

Uwajibikaji katika nyanja mbalimbali;

1. AFYA,
katika nyanja ya afya ni muhimu sana suala la kuwepo kwa uwajibikaji tena wa kiwango kikubwa hii ni kutokana na sekta hii ni muhimu katika kufanya maisha ya binadamu kuwa salama na kuzidi kuwepo, hivyo katika nyanja uwajibikaji kwanza huanza kwa kila mmoja hapa namaanisha kwa mgonjwa na kwa watoa huduma. Mtu (mgonjwa) anapaswa kutambua wajibu wake kuwa pindi anapojisikia hali ama viashiria vyovyote vya maradhi anapaswa kufika katika kituo cha huduma ya afya kwaaajili ya vvipimo na matibabu ya kina vilevile watoa huduma wanapaswa kuwajibika kwa nafasi zao kwa kuwahudumia wagonjwa tena kwa haraka zaidi.

2. ELIMU, katika nyanja ya elimu kila raia ni haki yake kupata elimu tena bora, wazazi wanalojukumu ama wajibu wakupeleka watoto wao shule tena wakiwa na mahitaji yote muhimu na pia watoto (wanafunzi) wanaowajibu wa kwenda shule kusoma na kuzingatia masomo yao na pia waalimu wanaowajibu mkubwa wa kuhakikisha wanatoa maarifa yao kwa wanafunzi kwaajili ya kuwaanda kuja kulitumikia taifa, na pia viongozi kuanzia Rais na wote waliopo kwenye sekta ya elimu wanaowajibu kupanga na kusimamia mipango yote yenye jukumu la kufanya elimu bora inapatikana tena katika mazingira mazuri kuanzia majengo mpaka vitendea kazi.

3. KILIMO, katika nyanja ya kilimo wakulima wanaowajibu wa kuandaa mashamba yao kwaajili ya kuweka mazao pia serikali kupitia wizara yake ya kilimo na wataalamu wake wanaowajibu wa kuhakikisha wanatoa elimu ya kilimo kwa wakulima ili kuchochea mavuno mengi kwa mfano matumizi ya mbolea na hata kutoa mbegu ambazo hazichukui muda mrefu shambani ili kukwamua hali za wakulima na kuishinda njaa.

4. SHERIA, katika nyanja ya sheria ni kwamba ni wajibu wa kila raia anatambua sheria na kanuni ili kumuwezesha kuishi bila kuwepo na migongano na pia wasimamizi wa sheria na watoa hukumu wanaowajibu wa kusimamia haki na usawa kwa mujibu wa sheria zilizowekwa pia wanawajibu wa kuelimimisha na kuwafafanulia zaidi raia kutokana na vipengele mbalimbali vya sheria ili kupunguza migogoro katika jamii.

5. TEKNOLOJIA, katika nyanja hii ni ukweli katika dunia ya sasa hatuwezi kuepuka matumizi ya teknolojia hii ni kutoka mapinduzi ya sayansi yanayoshika kasi hivyo ni wajibu kila mtu kutambua matumizi sahihi ya teknolojia na pia viongozi wenye dhamana wanapaswa pia kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya teknolojia.

6. UONGOZI, katika nyanja hii ni kuwa kilankiongozi ana wajibu wakusimamia ile dhamana aliyopewa bila kuonyesha ubaguzi na upendeleo wa aina yoyote na pia raia wanawajibu wakuwaheshimu na kuwatii viongozi wao katika jamii.

7. MALEZI, katika nyanja hii ni ukweli kuwa kila mtu anastahili kupata malezi bora, wazazi wanaowajibu wa kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa watoto wao kwaajili ya kuwaandaa kwa maisha ya baadae na ni wajibu kwa watoto kupata malezi hayo pia serikali na jamii yote kwa ujumla inawajibu mkubwa wa malezi katika jamii kwa kutoa elimu na mbinu mbalimbali kuhusiana na malezi bora.

8. SANAA, katika nyanja hii inaaminika kuwa sanaa ni ule ujuzi ama.ufundi aliyekuwepo na mtu, hivyo ni wajibu wa kila mtu kutumia ama kuonyesha sanaa yake kwaajili ya manufaa ya jamii nzima pia serikali inayowajibu wa kuhakikisha wanaandaa mazingira maalumu ya kuwapata wanasanaa kwa kuwekea miundombinu sahihi pia wanawajibu wa kutoa elimu na ushauri na sahaa kwa kila mtu kuonyesha kipaji chake bila kuogopa.

Hitimisho

Suala la uwajibikaji ni jambo kubwa na la msingi katika kila jamii kwani ktokana na kuwepo kwa uwajibikaji unaofanya kila mmoja akatimiza majukumu yake tena kwa wakati jambo hili litaleta ama kupelekea mabadiliko chanya makubwa katika jamii na kila sekta itajivunia kwa kila jambo ama mikakati watakayojiwekea kwani itatimia kwa wakati sahihi, hivyo ibaki kusema kuwa uwajibikaji ndio chanzo kikubwa cha mabadililo chanya (maendeleo).
 
Upvote 4
Back
Top Bottom