ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,753
- 9,575
HABARI WADAU
Natumai mu wazima, nimefurahia kujitokeza tena kwenye kinyang'anyiro cha shindano hili
hapa jukwaani.
Nijikite kwenye mada tajwa hapo juu isemayo: "Uwajibikaji mahali pa kazi hulete chachu ya maendeleo na kukua kwa uchumi kwa jamii inayotuzunguka na eneo uliilopo na hata kwa mtu binafsi pia".
MAANA YA UWAJIBIKAJI:
Uwajibikaji ni ile hali ya mtu, mtendaji, ama kiongozi wa kubeba dhamana ya jambo/kitu afanyacho na kutoa ripoti ama majibu pale anapofanyia jambo hilo au kitu hicho.
Maana ya pili ni ile hali ya mtendaji kuwajibika kwenye lile jambo alilopewa na kulifanya kwa umakini na weledi pasipo kukosea.
NINI MAANA YA KAZI?
Kazi ni seti ya shughuli ambazo zinafanywa kwa lengo au dhumuni la kufikia hatma au kutatua shida au kuzalisha bidhaa na huduma.
KUWAJIBIKA MAHALI PA KAZI
Eneo ambalo upo unafanyia shughuli zako au ambalo umewekwa ufanye kazi, au mahali upoajiriwa au jiajiri una budi kufanya kazi/shughuli hapo kwa nguvu na juhudi sana ili kuleta maendeleo katika jamii na wewe mwenyewe binafsi, pasi kufanya kinyume ni kudhorotesha uchumi wa hilo eneo/kampuni/kiwanda na kuleta kudumaa kwa kiwanda/kampuni ambayo imekuweka hapo.
Maendeleo hayaji kwa kukaa, kupiga story bali kwa kujituma, na kuwa na bidii na ufanyakazi kwa ufanisi mzuri ndipo utaona maendeleo na ustawi wa uchumi ukikua. kwa kasi kama hutokuwa au hatutokuwa watu wa kujituma, kuwajibika tusitarajie kuona tumepanda daraja la juu. Tatizo ambalo lipo kwa sasa Duniani hususani Afrika yetu, watu wengi hawawajibiki wengi wako wavivu, wazembe wanataka kuona kitu kinajiendesha chenyewe hawawajibiki tunabaki katika lindi zima la umaskini wakati rasilimali zipo; zinahitaji uwendeshaji wake. Sasa hapo utaona Uchumi ukikua, la hasha tutabaki kwenye lindi la umaskini na hohehahe.
Kwanini nchi zilizoendelea wako juu kimaendeleo na kiteknolojia? Wako hivyo kwa sababu wametambua kuwa kuwajibika na kujituma kwenye kazi zozote ndiko kunaleta maendeleo ya uchumi na ukuaji wa nchi zao. Endapo wangekuwa watu wa porojo je wangeendelea na kuleta mapinduzi katika nchi zao?
Tunalo la kujifunza hapo, sisi tumebaki hivi tulivyo sababu tuko na porojo hatuwajibiki, waliopo makazini kazi yao kubwa ni kusaini wakati wakiingia nakutoka ofisini na kupiga stori pasipo kutambua kilichowapeleka pale ni kuwajibika na kuleta chachu ya maendeleo ya kampuni, ama ofisi yao. Je, kama sio kujituma tutaona hayo maendeleo kama nchi zingine? Chachu ya maendeleo inakuja pale ambao mtu/watu kujituma na kuwajibika sehemu yoyote uliopo. Tunaona wenzetu wanakuja kuwekeza hapa katika rasilimali zetu, je, sisi wenyewe hatuna nguvu hizo? Ninaoposema nguvu ninamaanisha uwezo/mali/ fedha za kuwekeza kitu.
PICHA KWA HISANI YA MTANDAO
NINI KIFANYIKE SASA?
Hatuna budi kutambua na kujitoa katika zama za kujibweteka; tuchukue hatua ya kujituma mahali pa kazi yaani ppopote panapokupa tonge ndipo tutaona maendeleo katika Taifa letu, wewe binafsi na uchumi wetu ukikua hiyo itakuwa chachu ya mendeleo kwetu.
Maendeleo hayaji hivihivi bali ni kujituma na kuwajibika kwa ufasaha ndipo utaona hayo maendeleo katika lile jambo ama kitu ufanyacho
Mfano halisi tunawaona Wachina wanavyojituma na kuwajibika katika uzalishaji wa vitu na ubunifu wa vitu na kukuza uchumi wa Nchi yao, je, wako wapi sasa? Je, hawajatoka na kupanda ngazi kiuchumi? Wameenea sana duniani na mali zao zipo nchi mbalimbali. Kuwajibika kwao kumepelekea kukua kwa kasi kwa uchumi wa Taifa lao. Wangekuwa watu wa porojo na uvivu je wangefika pale walipo? La hasha KUJITUMA, KUWAJIBIKA, NA KUNIA ndiko kumewapelekea pale waliopo sasa.
WEKA NIA NA JITIHADA MAHUSUSI KATIKA SHUGHULI UFANYAYO.
Huna budi kujituma kwa nguvu na bidii ndipo utaona uchumi, wako na wa nchi ukikua kwa kasi maneno matupu hayajengi bali vitendo ndivyo vinavyoleta chachu ya maendeleo
HITIMISHO
Tujijengee dhana ya kuwajibika mahali tuliopo ndipo tutaona uchumi wetu ukikua kwa kasi
Ningewaomba watendaji wa ofisi za umma, sekta binafsi, na mtu mmoja mmoja tusiwe watu walegevu, wababaifu, wavivu, wenye kupenda porojo pasipo kujituma, tuwe chachu ya maendeleo kwa Taifa letu ndipo tutaona maendeleo kwenye sekta zetu zikikua kwa kasi, na Taifa letu kupanda daraja la uchumi wa juu, tusibweteke na kuridhika hapa tulipo wakati rasilimali tunazo, misitu tunayo, maziwa na mito tunayo, kwanini waje watu wabebe mali zetu kienyeji wakati wenyewe tupo ambao tuna nguvu, za kufanya na kuwajibika.
Niwaombe viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza wawe chachu ya maendeleo ya ustawi wa nchi yetu wafanye jitahada madhubuti ambazo zitafanya kila mtanzania au watu kujituma na kuwajibika kwenye eneo, au taasisi aliyopo pasipo kulala wala kuzembea, wao wakionyesha nia na hali ya kujituma ndipo watasababisha hata mtu wa chini kujituma pia. kingine tusijilimbikizie mali bali tuwe watu ambao tutawajibika kwa ajili ya Taifa letu ndipo tutaona Taifa letu likikua kwa kasi kama Mtaifa mengine na kupanda daraja la uchumi wa juu
Neno: Mataifa mengine yanajituma, yanawajibika, yanakomaa je sisi tunashindwaje? nini kilichotufanya tuwe bweteke wakati Taifa letu lia utajiri wa kutosha, ardhi yenye rutuba, madini kama yote, mito na maziwa hali ya hewa njema.
TUJITUME NA TUWAJIBIKE TUTAONA MSTAKABALI WA UCHUMI WETU KUKUA KWA KASI.
Wasalaam,
Ladyf.
Naomba mnipigie kura wadau wangu kwa wingi nami niingie kwenye kinyang'anyiro cha ushindi andiko langu.
Aksanteni sana.

Upvote
6